Blogger Widgets September 2013 | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, September 14, 2013

MAMA MANGWEA AJITOSA KUMTETEA MWANA FA...!!

Mama wa MwanaHip Hop aliyewahi kuaminika kuwa bingwa wa mitindo huru, Albert Mangwea aliyefariki mwezi Mei mwaka huu, Denisia Costantine Mangwea ameibuka na kumtetea mwanamuziki wa kizazi kipya Hamis Mwin’juma ambaye anatuhumiwa kuahidi pesa kwa mama huyo na kuingia mitini.


  
Sakata hilo ambalo limekuwa likiripotiwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, linatokana na kitendo cha mwanamuziki huyo (MwanaFA) ambaye aliwahi kuahirisha onesho lake, baada ya kifo cha msanii mwenzake (Albert Mangwea), kutokuweka hadharani hitimisho la ahadi aliyoitoa kwa familia ya marehemu.
Tarehe 31 ya mwaka huu ilikuwa ni tarehe ya onesho la The Finest ambalo MwanaFA alikuwa akitimiza miaka 13 ya muziki wake, akawa na lengo pia na kuugeuza muziki wa Hip Hop uwe na sura ya kistaarabu na kibiashara pia ili kuuongezea aina ya mashabiki.
Siku moja kabla ya onesho, msiba wa Albert Mangwea ukatokea, na hapo ikamlazimu mwanamuziki huyo kuahirisha onesho lake, na kulisogeza wiki mbili mbele huku akiahidi asilimia 15 ya faida atakayopata, angeipeleka kwa familia ya Albert Mangwea.
Baada ya mazishi, Onesho la The Finest lilifanyika Juni 14, na baada ya hapo, MwanaFA hakuonekana akisema kwenye mitandao wala kwenye redio kuhusiana na mapato yake kwenye onesho hilo na kiasi gani alipeleka kwa Mama Mangwea. Tangu onesho hilo, huu ni mwezi wa tatu na ndipo gazeti moja la kila wiki likaandika kuhusiana na suala hilo, jambo ambalo linaendelea kuzungumzwa kila kukicha kwenye vyombo vya habari. Na ndipo gazeti hili liliamua kwanza kumtafuta Mwana FA na kuongea naye.
Kauli ya MwanaFA
Akiongea na Mwananchi, MwanaFA alikiri kuahidi kutoa fedha hizo na aliahidi asilimia 15 ya faida  itakayotokana na mapato ya onesho la The Finest.
“Nakiri kukosea jambo moja, nilipoahidi, niliongea na wanahabari lakini wakati wa kutoa, nilitoa bila kutangaza, na hii kutoa jamani ni moyo, haina haja kumtangaza mtu kwa kuwa umemsaidia au umempa pole”, alifafanua MwanaFA
Alisema katika mapato aliyoyapata kutokana na onesho hilo ambayo yalikuwa ni jumla ya shilingi 19.5 milioni, alitoa milioni tatu na kuzikabidhi kwa mama huyo, ingawa si taslimu, aliziingiza kwenye akaunti yake, katika benki ya Exim. Alifafanua kwamba alilifanya hili kwa moyo na hakuwa na nia ya  kujitangaza kwa hiyo alilimaliza akawa anaendelea na shughuli zake. Baada ya kauli hii, Mwananchi likapiga mguu mpaka Kihonda kwa mama yake Mangwea, Bi Denisia Costantine Mangwea
Mama Mangwea ashangaa!
Alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo Mama Mangwea alikiri kwamba ameumia sana moyo baada ya kusikia ripoti ya kwamba MwanaFA anadaiwa hakutoa hizo pesa kwani alitoa kipindi kile kile cha msiba.
Kabla hata ya arobaini, aliweka benki kisha akaja na mwenyewe, hakuna na waandishi kama wanavyofanya wenzake, alikuja mwenyewe tukaongea, na mara kwa mara tunawasiliana, wanataka kumtia doa kijana wa watu ni muungwana sana”, alifafanua mama Mangwea.

MTUHUMIWA WA UBAKAJI AHENYESHA POLISI...



KATIKA hali isiyo ya kawaida, kijana Faizi Haji Juma (22), mkazi wa Mchanga wa Kwale Wilaya ya Chakechake, Pemba aliwashangaza wananchi baada ya kuwatoroka askari waliokuwa wamemdhibiti ndani ya jengo la mahakama ya wilaya hiyo.
Kijana huyo anayekabiliwa na makosa mawili katika mahakama mbili tofauti, likiwemo la ubakaji na shambulio la mwili kwa lengo la kutaka kubaka, aliwachomoka askari na kukimbilia baharini katika Soko la Katari.
Baada ya kukimbia kwa muda, askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Agustino Awe na Koplo Mohamed Hamza, walilazimika kumkimbiza kwenye matope na kuhakikisha wanamtia mikononi mtuhumiwa huyo na kumrudisha mahakamani.
Baada ya kurudishwa ndani ya viunga vya mahakama ya wilaya, mtuhumiwa huyo alitakiwa kuieleza korti sababu zilizomfanya akimbie lakini akaishia kubabaika.
Hakimu Omar Mcha Hamza alihamaki baada ya kushuhudia tukio hilo ambapo aliporejeshwa, aliamuru mtuhumiwa huyo kurudishwa rumande.



PICHA:RAIS SHEIN AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI MJINI UNGUJA..




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,Mjini Unguja,baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao 
 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa  Tindikali jana na watu wasiojulikanwa,katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu.
 
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa  na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikanwa jana jioni Mtaa waMlandege Mjni
 
 Mmoja wa Ngugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa  kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo
 
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifafanua jambo wakati akiwafariji jamaa na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika kumuangalia Padri huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasijulikanwa jana jioni katika Mtaa wa Mlandege Mjini Unguja
Powered by Blogger.