ARIME.habari na mwandi wa blog kutoka tarime Ahmad nandonde
SERIKALI imetakiwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa mtaa wa Msati kata ya Nyamisangura na Jeshi la wananchi JWTZ Nyandoto Wilayani Tarime ili kuepuka athari zinazojitokeza na kwamba endapo mgogogro huo usipotatuliwa unaweza kuvunja mahusiano mazuri kati ya Wanajeshi na wananchi.
Akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Sirari Amos Sagara ( CCM) alisema kuwa Novemba 7 majira ya alfajiri baadhi ya mashamba ya viongozi wa Chadema na wananchi wengine yanadaiwa kufekwa na wananjeshi wa JWTZ Nyandoto kwa mujibu wa maelezo ya wananchi.
Sagara alisema kuwa kwa sasa wanafatilia ili kupata ukweli wa watu waliohusika kuharibu na kufeka mazao ambapo pia alisema kitendo cha kufeka mazao ni kukaribisha njaa kwa wananchi hasa waliofekewa mazao ambapo alilaani kitendo hicho kuwa kina rudisha nyuma maendeleo.
Aliongeza kuwa kwa maelezo ya wananchi wanadai kuwa chanzo cha mazao yao kufekwa kinatokana na mgogoro wa ardhi na mipaka kati ya wananchi na wanajeshi ambapo wanajeshi wanadai kuwa wananchi wamevamia na kuishi maeneo ya jeshi huku wananchi nao wakidai wao ndio wamiliki halali wa ardhi.
Sagara alisema kuwa endapo Serikali itatatua mgogoro huo kwa kuzingatia taratibu za sheria za ardhi itasaidia kuondoa mgogoro huo wa wanajeshi na wananchi kwani itaonyesha nani mmiliki halali wa ardhi na kwamba endapo eneo ni lajeshi kuna haja ya Serikali kuwatafutia maeneo wananchi maeneo mengine ya kuishi.
Mashamba yanayodaiwa kufwekwa na jeshi la JWTZ Nyandoto ni shamba la Diwani wa kata ya Nyamisangura Thobias Ghat,Mwenyekiti wa mtaaa wa msati kata ya Nyamisangura Zacharia Ghati,mwingine ni Machango Gebeno.
Rorya.
DIWANI wa kata ya Ikoma Wilayani Rorya Mkoani Mara Laurent Adriano( CCM ) amewataka wananchi wa kijiji cha Ikoma kuachana na ukabila badala yake wafanye maendeleo kwa madai kuwa kuna ukabila kati ya Waluo na Wakurya jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya kijiji.
Adriano alisema kuwa kijiji cha Ikoma kina mgogoro wa ardhi kati ya watu wa kabila la wakurya na Wajaruo ambao chanzo chake kianatokana na kutofanyika kwa uhakiki na usajiri kwa Wakurya waliohesabiwa kuwa wana Ikoma Rorya ili wananchi wa Ikoma wawatambuwe lakini hadi sasa haujafanyika usajiri.
Hayo aliyasema wakati wa mkutano wa wananchi wa Ikoma uliokuwa ukizungumzia usajiri wa Watu ambao ni Wakurya ambao walikuwa wakijihesabu kuwa ni Wana Tarime Richa yakuwa Serikali wakati ilipotenganisha Wilaya ya Rorya na Tarime waliweka mipaka ambapo wananchi wa kitongoji cha Nyamuhunda ambao ni wakurya walihesabiwa kuwa wana Ikoma –Rorya.
“Kuna ukabila hapa Ikoma wakati serikali imeweka mpaka wakurya wa nyamuhunda walihesabiwa kuwa Rorya wakaambiwa wanatakiwa kufanya maendeleo Rorya lakini nasikitika inapofanyika mikutano ya wananchi hawahudhulii na wala hawafanyi maendeleo ya kijiji lakini mashamba wanayolima ni ya wanaikoma ambayo walipewa na Mwenyekiti wa kijiji na aliyekuwa Mtendaji wa kijiji na wa kata ambao kwa sasa watendaji hao wamehamishwa”alisema Adriano.
Adriano alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa aliagiza Halmashauri ya Rorya kufanya usajiri kwa watu wa Kitongoji cha Nyamuhunda ambao walihesabiwa kuwa wanaikoma ili waweze kufanya maendeleo Rorya nakwamba nivema sasa usajiri wa watu wa nyamuhunda ukafanyika ili kuweza kutambuliwa na wananchi wa Ikoma na waweze kufanya maendeleo kwa kile kilichoelezwa kuwa tayali watakuwa wanafahamika kwa wanaikoma.