Blogger Widgets February 2013 | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, February 23, 2013

matokeo kidato cha nne wawili wajiua, wawili wanusurika

KUFUATIA kupata matokeo mabaya ya matokeo yao ya kidato cha nne yaliyotangazwa wiki iliyopita jumla ya wahitimu wawili tayari wameshapoteza maisha kwa kujinyonga huku wawili wakiwa wameokolewa wakiwa katika harakati za kujiua 

Kati ya waliojinyonga ni Barnaba Venant [18] mkazi wa Mbagala ambaye alihitimu katika shule ya Sekondari ya Debrabant Mbagala ya jijini Dar es Salaam Akielezea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiyondo, alisema tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa 4 asubuhi huko maeneo ya Nzasa, Mbagala

Amefafanua kuwa, marehemu huyo alichukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na matokeo yake ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalibainishwa alipata daraja la nne point 27 kinyume na matarajio yake

Amesema kijana huyo alijinyonga kwa kutumia kamba ya manila, aliyokuwa ameitundika kwenye dari ndani ya stoo ya nyumba yao. Katika tukio lingine la aina hiyo, Michael Fidelis[19] aliyehitimu Shule ya Sekondari ya Kanyenye mjini Tabora

Imedaiwa kuwa, mhitimu huyo alipogundua amepata daraja sifuri aliporudi nyumbani alichukua maamuzi ya kujinyonga hadi kufa akiwa chumbani kwake kwa kutumia kamba ya manila.

Na kuacha ujumbe uliosomeka “Mama usitafute mchawi, uamuzi niliouchukua ni sababu ya matokeo yangu mabaya, nakutakia maisha mema, nisamehe sana mama.”

Kufuatia matokeo hayo mabaya yaliyoleta historia vijana wengine wawili mmoja mkazi wa Kimara Temboni jijini Dar es salaam amenusurika kutoa uhai wake kwa kutoridhishwa na matokeo hayo

Mwingine aliyefahamika wka jina la Hoseph Hoseah [18] mkazi wa mkoani Pwani alikimbizwa zahanati akwia aktika jaribio la kutoa uhai wake baada ya matokeo yake kuonyesha amepata daraja la nne jambo ambalo lilimfanya asiwe na raha tokea apokee matokeo hayo

Imedaiwa na mmoja wa ndugu wa kijana huyo kuwa ndugu yao huyo alikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi watano ambao shule ilikuwa ikiwatarajia wataleta sifa kwa kuleta daraja la kwanza shuleni hapo

Matokeo yaliyotangazwa mwanzoni mwa wiki hii na Waziri wa Elimu yanaendelea kuleta migogoro kwa wadau huku waziri huyo akitakiwa kujiuzuru

msanii Ragga Dee adondosha kichupa kipya

Akiwa ni msanii mwenye nidhamu na heshima katika kazi yake kiasi cha kupata heshima kubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wa muziki nchini Uganda, msanii Ragga Dee adondosha kichupa kipya alichokibatiza jina 'Katonda Kyasalawo'

Ragga Dee ameelezea kuwa hivi sasa anaongeza nguvu akijikita zaidi katika miondoko ya Zouk na Soukous akitumia sana lugha ya kiLuganda, kiingereza na Lingala.
kicheki kichupa chake kipwa hapa 

ideaja na ujio mpya na mzee mzima Prof Jay

Baada ya miaka mingi kupita tangu gwiji wa miondoko ya Hip Hop na Bongofleva, Joseph Haule  aka Prof. Jay kufanya kolabo na mwanashosti Judith Wambura aka Lady Jaydee, hatimaye wawili hao wamefungua mwaka kwa kuwapa mashabiki habari njema juu ya ujio wao wa pamoja.

Profesa Jay ameonyesha fuaraha yake hiyo kutokana na wawili hao kuiteka tasnia hii ya muziki kwa miaka mingi ambapo pia mwanashosti Jay Dee anatarajia kurekodi albamu yake mpya itakayokuwa ni ya sita kutoka kwa mwaka huu.

Saturday, February 2, 2013

Sugu aiponda Bongoflava



 Mr 2 a.k.a Sugu jamaa aliyeanza muziki kitambo sana na ambaye siku hizi pia ni mbunge wa jimbo la Mbeya mjini kwa jina halisi anajulikana kama Joseph Mbilinyi, aliwaponda wasanii wa bongoflava kwa kuongelea vitu visivyokuwepo.
 
“Mi mara nyingi huwa sisikilizi muziki wa bongoflava maana hawaimbi mambo yanayotokea sasa katika jamii wala mambo yanayoigusa jamii. Kuna mambo mengi sana ambayo unaweza ukaimba na ukaigusa jamii, sio kila siku kuimba nyimbo za aina zisizoeleweka hata jamii inashindwa kukuelwa”. Alisema Sugu.
 
Kuliko kusikiliza muziki wa bongoflava Mr Sugu alisema ni heri kumsikiliza msanii Koffi  Olomide wa Kongo maana nyimbo zake japo ni za kucheza ila zina ujumbe unaoendana na jamii ya leo na hata unapousikiliza masikioni hauchoshi mapema.

Watanashati Yaboreshwa Zaidi

NewsImages/6787526.jpg   
Kampuni ya Mtanashati Entertainment inayo milikiwa na Ostazi Juma namusoma, inayojihusisha na burudani, sasa imeboreshwa zaidi na kuaza kutengeneza Nguo mbalambali zikiwemo za watoto
 kampuni ya Mtanashati Entertaiment yenye makazi yake maeneo ya Magomeni Mapipa mtaa wa Idirisa jijini Dar es salaam, imeaza kutengeneza mavazi mbalimbali yakiwemo ya watoto.

Kampuni ya Mtanashati Entertainment imeudhihirishiwa watanzania kuwa ipo kikazi zaidi, baada ya baada ya kuwanzisha utengenezaji wa nguo na vifaa mbalimbali kama vile miganda na mabegi.

kampuni hiyo, ambayo inamiliki wasanii wa bongo flava waonaofanya vizuri kwa sasa katika anga ya muziki wa Tanzania, miongoni mwa wasanii waliyopo chini ya kampuni hiyo, ni P.N.C, Dogo Janja, J FIL DAV, HAPPY BALICE NA AMAZON.

Msanii P.N.C kwa sasa anatamba na wimbo wake imebuma huku msanii Dogo janja ameonesha kuwatishia wasanii wengi wakubwa baada ya kujiunga katika kundi hilo na kutoa singo yake aliyomshirikisha msanii mwenzake P.N.C katika Single yake mpya inayokwenda kwajina la Ya moyoni.

Kampuni hiyo ilianzishwa 19/2009 na kuzinduliwa rasmi tarehe 9/9/2012 ndani ya Clab Bilcanas, toka kuzinduliwa kwa kampuni imeleta mapinduzi makubwa katika mziki wa Tanzania
Powered by Blogger.