Blogger Widgets August 2013 | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Thursday, August 8, 2013

MBUNGE wa kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ameibua madudu mapya katika sekta ya elimu

MBUNGE wa kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ameibua madudu mapya katika sekta ya elimu, ambao umebaini kwamba kwenye mitihani ya majaribio ya darasa la saba, baadhi ya maswali ya kuchagua, hayakuwa na majibu.

Mitihani hiyo ya majaribio ya programu maalum ya matokeo makubwa sasa, kwa mujibu wa Mbatia ilifanywa na wanafunzi wa darasa la saba hivi karibuni katika masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza katika wilaya 40 nchini.

Katika uozo huo ambao ameutaja kama kuwakatisha tamaa wanafunzi katika somo la Hisabati, Mbatia alisema maswali sita yalibainishwa na wataalamu wa Hesabu kuwa hayana majibu huku swali moja likiwashinda maprofesa waliofanya mtihani huo.

Alisema katika swali moja, namba 33 walimu wa hisabati katika shule kubwa za msingi walishindwa kulifanya na baadaye kubainika kuwa ni swali la mwanafunzi anayechukua fani ya uhandisi katika vyuo vya elimu ya juu.

Mabatia alisema katika mitihani hiyo, kunamakosa mbalimbali ya lugha pamoja na usahihi wa masuala mbalimbali, ikiwemo programu hiyo kuainishwa kama matokeo makubwa sasa huku jina la wizara likiandikwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Alisema katika mtihani huo wa hisabati,ambao wanafunzi wa darasa la saba walitakiwa kufanya kwa saa mbili, mtaalamu wa aligebra aliufanya kwa saa 2:10 na profesa saa 2:03 huku yeye akifanya kwa saa 2:19.

“Matokeo haya ni kuwakatisha tamaa na kuwaua wanafunzi kabla ya kufanya mitihani, ni lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuokoa mapigo haya ya moyo wa Taifa ambayo yakizimika, Taifa linakufa,” alisema.

Mbatia alitoa mapendekezo yake ili kuokoa janga hili la elimu ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Tume ya Kudumu ya Elimu, itakayoshughulikia kuhakikisha ubora wa elimu nchini. Tume hiyo kwa mujibu wa Mbatia, inatakiwa kuwa na mamlaka ya kuhakiki utendaji wa taasisi mbalimbali za elimu, ambazo hadi sasa zimeonekana kutotimiza vyema wajibu wake.

“Ninaamini kwamba,tume hiyo itakapoundwa itasaidia kubainisha wazi nini falsafa na malengo hasa ya utoaji wa elimu nchini, kulingana na wakati tulionao, jambo ambalo halitakuwa geni kwani katika uongozi wa awamu ya kwanza, kulitungwa falsafa na miongozo mbalimbali,”alisema

Alisema kwa mamlaka aliyonayo Rais na na kwa mujibu wa katiba na kwa kadri anavyoona inafaa, anaweza kuunda tume na kuipatia majukumu ya utendaji stahiki, ikiwemo kutoa idhini ya matumizi ya mitaala mingine.

Pia alipendekeza tume hiyo ihariri na kupitia vitabu vya kiada kwa shule nchini na kufanya utafiti za kisayansi kuhusu masuala mbalimbali ya elimu kwa lengo la kuinua ubora wa elimu.

Akizungumza na Blog hii , Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bunyanzu Ntambi alikiri kuwa jinala wizara limekosewa katika mitihani hiyo. Alipoulizwa kuhusu uozo uliopo katika mitihani hiyo ya majaribio, alisema atafuatilia na atatoa taarifa kwa gazeti hili baadaye.

Wednesday, August 7, 2013

WAZAZI WAKATAZA WALIMU WASIWAFUNDISHE WATOTO WAO JINSI YA KUTUMIA CONDOM

Imeelezwa kuwa Baadhi ya wazazi na walezi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamekuwa wakiwazuia walimu kutoa elimu ya njia ya kujikinga na ukimwi kwa watoto wao wa sule za msingi ikiwemo matumizi sahihi ya condom. 

Hayo yamebainika leo katika semina iliyoandaliwa na shirika la UNESCO iliyojumisha wakuu wa shule za msingi na sekondari pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika katika ukumbi wa Golden Valley Mjini Kahama.

Akichangia hoja katika semina hiyo Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Korogwe Bi Ashura Rugakingira amesema kuwa wamekutana na tatizo hilo toka kwa baadhi wazazi hao licha ya kuwa somo hilo lipo katika mtaala wa Serikali.

Rugakingira amesema kuwa changamoto hiyo inawafanya walimu wengi kukata tamaa ya kutoa elimu hiyo ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa wanafunzi hao.

Awali akifungua semina hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Bi Isabela Chilumba amewataka walimu hao kuvunja ukimya na kuwa wawazi kuzungumza na wanafunzi wao kuhusu Maambukizi ya virusi vya ukimwi na UKIMWI.

Sambamba na hayo Chilumba ametoa angalizo kwa wananchi kutodanganyika na takwimu za maandishi zinazotolewa na kwamba kila mtu awe mstari wa mbele kupima afya yake mwenyewe.

Naye Msimamizi wa mradi huo wa Elimu ya Afya ya UKIMWI, uzazi na maadili kwa vijana kutoka UNESCO Mathius Herman amesema lengo la mradi huo ni kujenga mahusiano rasmi kati ya Mashirika yasiyo ya serikali na shule.

Powered by Blogger.