Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Monday, September 3, 2012

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA CHATOA POLE KWA WANDISHI HABARI .
Katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo wilaya ya tanga mjini Khalid Rashid wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake zilizopo Maeneo ya Barabara ya 14 Jijini Tanga akizungumza kuhusiana na mauaji ya mwandishi wa habaya yaliyo tokea mjini Iringa huku pia akigusia kuhusiana na kusogezwa mbele kwa mikutano ya chama hico kupicha zoezi la sensa

pichani ni wandishi wa habari wakiwa wanasikiliza kwa makini maelezo ynayotolewa na katibu wa chama hicho kulia ni bwana Mbaruku yusufu na kushoto kwake ni Bwana oscar asenga .picha zote kwaniaba ya mpiga picha wangu bwana Selemani Kibuko
Vurugu Baina ya Wafuasi wa Chadema na Polisi katika kijiji cha Nyololo , Mufindi zasababisha kifo cha Mhandishi wa habari wa Chanel 10

gari la viongozi wa chadema likiwa linaelekea mahakamani
bwana daudi mwangosi kulia enzi za uhai wake

mwili wa marehemu daudi mwangosi ukiwa unapitwa na polisi kama takataka bada ya mauti yake kumkuta

 hili ni bango la kikosi cha kuzuia ghasia likiwa linaonyesha hali ya hatari katika mkutano huo

Sunday, September 2, 2012


Gadna G Habash kaputen sasa atua Times FM .


KITUO cha Redio Times FM, kinachokuja kwa kasi nchini jana kimemtangaza rasmi mtangazaji maarufu nchini, Gadna G. Habash marufu kaka kaputeniii kwa enzi hizooo sasa  kujiunga nao baada ya kukaa nje ya ulingo kwa muda mrefu.


Gadna kabla ya kujiunga na kituo hicho, miaka miwili iliyopita alikuwa mtangazaji mahiri katika kituo cha Clouds FM, ambako alipata maarufu kwenye kipindi cha Jahazi kinachorushwa kila siku jioni.

Akizungumza Dar es Salaam jana katika hafla ya kumtambulisha mtangazaji huyo Mhariri Mkuu wa Redio Times, Scolla Mazula, alisema Habash katika kituo hicho atatangaza kipindi maalumu cha Maskani kitakachokuwa kikirushwa kila siku saa 10 jioni hadi saa 1 usiku.

Habash ametambulishwa rasmi kuhamia Radio Times FM, baada ya kuwa nje ya kazi kwa takriban miaka miwili, tangu alipoondoka Clouds FM.

Naye Habash ambaye ni mume wake msanii mahiri nchini Judith Wambura Jay Dee, alisema kipindi chake kitazungumzia mambo mbalimbali ya jamii pamoja na burudani na michezo kila siku.

NOP KAMA MZAZI AJA NA MZIGO MPYA BAADA YA KAMILIGADO


Saturday, September 1, 2012

JAJI WARIOBA AWAONYA WANAOWAFUNDISHA WANANCHI JINSI YA KUCHANGIA KATIBA MPYA 



MWENYEKITI wa Tume ya Katiba mpya hapa nchini Jaji Joseph Sinde Warioba amezitaka baadhi ya Taasisi ambazo zinawafundisha wananchi jinsi ya kuchangia maoni katika mchakato wa Katiba Mpya kuacha mara moja na badala yake wananchi wenyewe wachangia mawazo yao kulingana na Uitaji wa Jamii zao.

Jaji Warioba aliyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa Nusu mwaka kwa wanachama wa chama cha wanasheria hapa Nchini (Tanganyika Law Society).

Aidha Jaji Warioba alisema kuwa kwa sasa wapo baadhi ya watu ambao wanawafundisha wananchi jinsi ya kuchangia mawazo yao kwenye tume hiyo ilihali wananchi hao bado wanakabiliwa na changamoto ambazo ni muhimu sana kuwepo kwenye mchakato huo wa Katiba mpya.

Alifafanua kuwa hali hiyo ni ya ukandamizaji sana kwani wananchi wanakosa Uhuru wao na badala yake wanasema na kujadili kile ambacho baadho ya Taasisi na Mashirika wanachokitaka tofauti na Makusudio ya Tume hiyo.

“tunajua kuwa kwa sasa wapo baadhi ya wananchi ambao hawajui na hawatambui kabisa masuala haya ya Katiba kwa kuwa hawana elimu yake lakini bado wana nafasi kubwa sana ya kuweza kuchangia wanachokitaka kiwepo kwenye masuala hayo ya Katiba na sasa hawa watu, Taasisi, na wengineo wasitumie mwanya huo kuwashawishi watu waweze kutoa maoni wanayoyataka wao na kuacha yale ya msingi ambayo yapo ndani ya Jamii zao”aliongeza Jaji Warioba.

Pia alisema kuwa nao Wanasheria wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa mabalozi wazuri hasa katika kutangazia Umma umuhimu wa kushirikii na kuchangia Katiba mpya kwani Katiba na Sheria havipangani bali vinaendana kwa pamoja.

Awali Raisi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw Francis Stolla alisema kuwa ili kukabiliana na masuala mbalimbali ambayo yanajitokeza katika Katiba, wanachama wa chama hicho Watajadili kwa pamoja ambapo mara baada ya majadiliano watatoka na maazimio mbalimbali ambayo yatalenga kujenga na kuimarisha Mchakato mzima wa Katiba mpya.

Bw Stolla aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kulinda Umma wa Watanzania kutokana na hali hiyo wadau wa Sheria wana nafasi kubwa sana ya kuweza kusaidia Serikali hasa katika zoezi la Ukusanyaji wa Maoni yahususyo Katiba mpya.

“Sheria ya Chama chetu ni kusaidia Serikali juu ya masuala ya Sheria kwa hali hiyo hili pia ni letu na hivyo ni vema basi kama kila mdau ambaye anahusika na Sheria akahakikisha kuwa anatoa elimu zaidi hata kwa wale ambao hawana elimu juu ya umuhimu wa kutoa Maoni ya kuunda Katiba mpya ya Nchi”aliongeza Bw Stolla.

JAMANIII VIBAKAA NOMA WAKITAITIWAA CHEKII JAAA HUYOO ALIVYOO NASWA
hapo akiwa ananyanyuliwa na vijana wa kaziii

baada ya kupewa kichapoo kikali hapo midamuu kibaooooo.

 akiwa anatiwa katika karandinga la polisiiiii
TWITE APOKELEWA KAMA MFALIME JANGWANI


Beki wa kimataifa wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, Mbuyu Twite, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana wakati alipowasili akitokea Rwanda, tayari kwa kujiunga na timu yake ya Yanga baada ya gumzo la muda mrefu na mvutano wa hapa na pale wa Watani wa Jadi Yanga na Simba, ambao kila mmoja alikuwa kijinadi kuwa amemsajili mchezaji huyo huku mmoja akibaki kuambulia manyoya.

Akizungumza na mtandao huu kuhusu kutua nchini huku akiwa ametinga Jezi no 4, yenye jina la Mwenyekiti wa Simba Ismail Rage, beki huyo amesema kuwa yeye ni mchezaji kama walivyo wengine na anatambua kuwa ametua katika timu yenye upinzani mkubwa na mahasimu wao Simba, hivyo yeye ametua kuendeleza Utaji wa Jadi  baina ya timu hizo, na ndiyo maana ameamua kuvaa jezi yenye jina la Rage, ili kuonyesha maana halisi ya  utani huo pamoja na kutokea mtafaruku wa hapa na pale kati ya vilabu hivyo.

Aidha Twite, amesema kuwa ''Namuheshimu sana Rage, na namuomba aniache nifanye kazi niliyotumwa na Baba yangu kama alivyoniamini na kuniruhusu kuja kuitumikia Yanga na kuwarejeshea Faranga yao Simba'' alisema Twite kwa kiswahili kilichopindapinda.

Twite amewataka mashabiki wa Yanga kumuamini na kupuuza yanayoendelea kuenea juu yake kuwa huenda akikosa kuichezea timu hiyo kutokana na kuchanganya madawa na kusema kuwa yeye ni mchezaji halali wa Yanga timu ambayo imefuata taratibu zote zinazotakiwa.

Powered by Blogger.