Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, October 6, 2012


na mwanahabri ahmadi nandonde
HALMASHURI YA MKOA WA MARA IMETAKIWA KUEPUKA KUTEGEMEA HARAMBEE KUTOKA MIKOA YA MBALI KAMA VILE DAR ES SALAAM BADALA YAKE WATUMIE WANANCHI WAISHIO MKOA HUO NA WADAU MBALIMBALI WA MAENDELEO  ILI KUCHANGIA  HARAMBEE YA MUENDELEZO WA UJENZI WA HOSPITAL YA KWANGWA AMBAYO ITAITWA MWALIMU NYERERE MEMORIAL HOSPITAL.

HAYO YAMESEMWA  MJINI MUSOMA KATIKA KIKAO CHA USHAURI CHA MKOA RCC KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI  WA MKOA  HUO  AMBAPO KIASI CHA SHILINGI BILIONI TANO ZINAHITAJIKA ILI KUAKAMILISHA UJENZI HUO NA TAYARI SERIKALI IMETENGA SHILINGI BILIONI MBILI  KWA AJIRI YA UJENZI HUO HIVYO KUWEPO NA UPUNGUFU WA SHILINGI BILIONI TATU AMBAZO NDIZO ZITAKAZOFANYIWA HARAMBEE.
 
UJENZI  NA HARAMBEE HIYO  UNATARAJIWA KUANZA RASMI  HIVI KARIBUNI  NA HII IMEKUJA SIKU CHACHE BAADA YA TAARIFA YA MKAKATI WA MKOA WA MARA WA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA ZA RUFAA KATIKA NGAZI YA MKOA ILIYOTOLEWA NA MGANGA MKUU WA MKOA, NA KUJADILIWA NA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA RCC AMBAPO WAJUMBE MBALI MBALI WALIPENDEKEZA HOJA  ZITAKAZO HAKIKISHA KUWA UJENZI HUO UNAANZA RASMI IKIWA NI PAMOJA NA UKUSANYAJI WA FEDHA ZA KUENDESHEA HOSPITALI.

SANJARI NA HAYO WAJUMBE PIA WALIOMBA KUUNDWA KWA BODI YA HOSPITAL YA MKOA AMBAYO ITATOA MSAADA MKUBWA KATIKA KUENDELEZA HUDUMA ZA TIBA,VILEVILE UCHANGIAJI WA UENDESHAJI WA HOSPITAL  YA KWANGWA UNATARAJIA KUFANYIKA JIJINI DAR  ES SALAAM NA MJINI MUSOMA ,AMBAPO MKUU WA MKOA  WA MARA MHE JOHN TUPPA AMEMTAJA MHE RAIS KUWA MGENI RASMI KATIKA HARAMBEE IYO.

KADHAIKA WAJUMBE WAmeOMBA TATHMINI YA FIDIA KWA WATAKAOATHIRIKA NA UENDELEZAJI WA HOSPITALI IYO YA KWANGWA IFANYIKE NA UKAMILKE MAPEMA NA PIA TATHMINI IONYESHE KUWA NI KAYA NGAPI ZITALIPW

Wednesday, October 3, 2012

huku ya rufaa ya lema yapigwa kalenda

kesi ya kuvuliva ubunge inayo mhusu mbunge wa arusha mjini Godbles lema imehairshwa na majaji waliokuwa wakiisikiliza kesi hiyo katika mahakama ya rufaa jijini arusha

makubwa hayo lakini Ujumbe umefika!


Hiyo lazima wataikubali tu watake wasitake tafakari na utoe maoni yako kuhusu hili ni hakiii

VIDUME YANGA TAYARI KUIVAA SIMBA

Kocha mkuu wa Mabingwa wa klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, timu ya Young Africans Sports Club Mholanzi Ernie Brandts amesema kikosi chake kipo tayari kuikabili timu ya Simba sc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom hapo kesho uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz. leo asubuhi katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika shule ya sekondari Loyola, amesema wachezaji wake wote wapo safi, wana ari ya mchezo na ushindi, hivyo anaamini mchezaji yoyote atakayempanga atafanya vizuri.
Yanga mabingwa watetezi wa kombe la Kagame mara mbili mfululizo, wataingia uwanjani kusaka point 3 muhimu ambazo zitaipelekea kusogea katika nafasi nzuri ya kutwaa Ubingwa msimu wa 2012/2013.
Katika mazoezi yaliyofanyika leo asubuhi, kocha Brandts aliweza kuwatumia wachezaji wote waliosajiliwa katika msimu huu wa ligi, isipokuwa Salum Telela pekee ndio mchezaji majeruhi .
Kocha Brandts amesema amefurahi kwa wachezaji wake wote kuwa fit, kiakili, kimwili na kifikra kwa ajili ya mchezo wa kesho, na hivyo anawaahid wapenzi na wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kuona soka safi na la kuvutia.
Mchezo utaanza majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na utaonyeshwa moja kwa moja dunia nzima  na kituo cha runinga cha Supersport cha nchini Afrika Kusini.
'MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI YOUNG AFRICANS'
KIKWATOJR ANAWAPA MOYO MASHABIKI WOTE WA YANGA ULIMWENGUNI

Mbunge Marry Mwanjelwa (CCM-Mbeya) apata ajali, na gari lake kuteketea lotekwa moto

 
Masalia ya gari yenye namba za usajili T. 671 ABM aina ya Toyota Ranger mali ya mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa baada ya kuteketea kwa moto kufuatia ajali iliyotokea eneo la Mbalizi kwa kugongana na basi la abiria.
 
Mabaki ya gari la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Mary Mwanjelwa, aliyenusurika katika ajali iliyotokea mjini Mbeya kwa kuhusisha magari manne jana.
 
Mbunge wa Viti maalumu (CCM) Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa, akiwa amepumzishwa katika Hospitali teule ya Ifisi iliyopo Songwe wilayani Mbeya vijijini, baada ya kupata ajali akiwa katikia gari lake lililogongana na Basi la abiria na kupapata ajali eneo la Mbalizi jana na kuuwa jumla ya watu 10 na wengine kujeruhiwa.
  
PICHA KWA NIABA YA IPP MEDIA

mnyama diamond sasa kula bata na kampuni!

Huku nota yake ikendelea kung'aa kila pembe, msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios kwa ajili ya kusimamia kazi zake zote kwa muda wa miaka 2.
Taarifa iliyoifikia darhotwire kwa barua pepe, ilisema kuwa  I-View itasimamia mikataba yote ya kazi zote za msanii huyo na yeyote atakayetaka kufanya kazi na Diamond kwa sasa itabidi awasiliane I-View.

chupu chupu kufa

ABIRIA waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Dar Express  aina ya
Scania  wamenusurika kufa baada gari hilo kuteketea kwa kuungua na
moto wakati likiwa kwenye mwendo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Constantine Massawe amesema
kuwa ajali hiyo ilitokea jana jumatatu saa 5.30 asubuhi katika
barabara ya Segera –Chalinze eneo la Kijiji cha Segera Wilayani hapa.

Amesema gari hilo aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na dereva
aliyetambulika kwa jina la John Mwakihaba (41) lilikuwa likitokea
Rombo Mkoani Kilimanjaro kuelekea Jijini Dar es salaam.

Kamanda huyo amesema lilianza kwa kutoa moshi upande wa mbele karibu
na mlango wa dereva ndipo akasimamisha na kuwaamuru abiria wote
kusalimisha maisha yao kwa kutoka nje.

Amesema baada ya kutoa taarifa polisi ndipo ikawasiliana na kikosi cha
zimamoto cha Mji wa Korogwe ambacho kilipeleka gari lake na kufanya
jitihada za kuuzima moto kazi iliyowachukua muda wa saa moja kuizima.

Hata hivyo abiria wa basi hilo hawakupata majeraha wala hakikutokea
kifo kwani abiria walipoelezwa walitoka ndani ya basin a kukaa kando
wakilishuhudia likiteketea licha ya kwamba gari hilo liliteketea lote.

“Ni jambo la kushukuru kwani hakuna majeruhi wala kifo katika ajali
hiyo kwani abiria waliweza kutii amri ya dereva aliywataka kutoka ili
kunusuru maisha yao.
Powered by Blogger.