Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, October 20, 2012

YANGA YAIAZIBU RUVU SHOTING 3-2

Mchezaji wa timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii  jijini Dar es salaam, mpira umekwisha  timu ya Yanga imeifunga Ruvu Shooting  magoli 3-2, Goli la tatu la timu ya Yanga limepatikana katika kipindi cha pili cha mchezo huo baada ya kutoka uwanjani kwa mapumziko zikitoshana nguvu  kwa kufungana magoli mawili kwa mawili katika kipindi cha kwanza 
Mchezaji wa Yanga Jerrison Tegete akishangilia mara baada ya kufunga goli la pili katika mchezo huo na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika timu zikitoshana nguvu kwa magoli, mpaka kipindi cha pili ambapo Yanga iliongeza goli la tatu na kufanya matokeo hayo kuwa 3-2

Friday, October 19, 2012

HABARI NDO HIYO: AUNTY EZEKIEL AMEOLEWA..MLISEMA HAOLEWE SASA HAYO.!!!

                                                                              Mashallah bi Rahma kapendezajeee
               Haya habari ndo hiyo mliosema haolewi yako wapi? Bibie huyo mkwe wa Demonte.
                                                                Sheikh akimuyonyesha Aunty mahali pakuweka saini

waislamu wapiga stop kuandamana jijini dar es salam


Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekutana na kutoa tamko la kuzuia waislamu kuacha kuandamana mara moja.

Katika taarifa ya waliyoitoa mapema leo asubuhi wakuu na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo wa dini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick, (picha ya chini) aliwatoa hofu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani wamejipanga kulinda hali ya amani.

Akitoa tamko hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kumekuwapo na taarifa za waumini wa Kiislamu kuandamana na kufanya fujo mara baada ya swala ya Ijumaa na baadala yake amewataka kuacha kufanya hivyo na warejee majumbani kwa amani na suala hilo linashughulikiwa kisheria.

Hata hivyo kwa upande wao viongozi wa dini waliokutana na Mkuu wa mkoa  juu ya kutolea tamko hilo waliwaasa waumini wote kutoingia mitaani na kuandamana kwani wakifanya hivyo ni kukiuka misingi mbalimbali  ya kisheria iliyopo kihalali na watakapofanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi.

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa bin Salum amewataka wakuu wa misikiti mkoa wa Dar es Salaam kuwakataza waumini hao kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kukiuka misingi iliyopo.Aidha, aliwaomba waumini warejee majumbani  kwa amani.

Askofu  Makunda aliwataka watanzania kuendelea kufuata misingi ya kiimani bila chuki wala kufanya fujo.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova (pichani juu) alitoa onyo kali kwa waislamu kuacha kufanya hivyo hii leo kwani kwa atakaekiuka atachukuliwa hatua kali. Kova aliwataka waumini kurejea majumbani mwao kwa amani bila kufanya maandamano  na pia aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kupuuza tishio hilo la fujo kutoka kwa waislamu.

“Jeshi limejipanga kuakikisha hali ya amani na usalama inakuwepo hivyo taadhari kwa waislamu kuacha kufanya maandamano mara moja” alisema Kova kwenye kikao hicho ambacho kinaendelea hivi sasa.

Wakuu hao wamekutana kwa dharura baada ya kuwepo kwa taarifa za juu ya waumini hao kutishia kuandamana  na kufanya fujo.

waislamu wachache kuandamana dar lengo ni kutimba ikulu

wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi

hapa kiwa anaulizwa na jeshi la polisi imekuwaje wakafanya madhamano hayo mmoja wa wandamnaji
 Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu. 

WATU sita waliokuwa na nia ya  kuandamana kuelekea Ikulu wamekamatwa na Jeshi la Polisi.

kwa mujibu wa waandishi wa habari waliopiga kambi katika viunga vya Ikulu watu hao walifika mmoja mmoja kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano.

Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha.

Thursday, October 18, 2012

kiongozi wa polisi zanzibar anena na wandishi kuhusiana na vurugu


Kamishna wa Polisi Mussa Ali Mussa akifafanua jambo katika Mkutano na Waandishi wa Habari akielezea juu ya Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.
vurugu zilizofanywa na wananchi wachache, Waziri Mohamed Aboud alisema vikundi vya vijana vinavyosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Sheikh Farid Hadi walifanya vurugu hizo katika mitaa ya Darajani, Michenzani, Muembeladu,Magomeni,Amani wakidai Sheikh wao haonekani na kudhani amekamatwa na vyombo vya Dolan a kuwekwa ndani.
wakwanza kulia ni bwana mustapha musa moja kati ya wandishi wa habari waliohudhuria katika kikao hicho cha wandishi wa habari kilicho fanyika ziwani mjini unguja.
picha ni badhi ya maeneo ya jiji la zanzibara wakatio wa vurugu ya kikundi cha UAMSHO na polisi wa zanzibar

Tuesday, October 16, 2012

MWILI WA ALIEKUWA RPC MKOANI MWANZA ASCP LIBERATUS BARLOW WAAGWA LEO MKOANI HUMO



hapa akiwa anaingizwa katika viwanja vya nyamagana jijini Mwanza kwajili ya salamu za mwisho kwa waombolezaji

Hii ndio safari ya mwisho ya aliekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza ASCP Liberatus Barlow (53), alieuwawa juzi kwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ameacha mjane na watoto wa nne.




Shughuli ya kuuaga mwili wake ilifanyika leo kuanzia saa Nne asubuhi hadi saa Kumi jioni katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza, ikihudhuriwa na mamia ya watu kutoka jiji hilo na viunga vyake pamoja na watu kutoka mikoa ya jirani.

warembo wa bongo muvi wajichafua ili wajisafishe

wema sepetu akiwa na mwenzake ant ezekiel mbele ya wandishi wa habari wakiomba razi kwa picha zao za kuonesha hali ya utupu  walizo pigwa wakati wa tamasha la serengeti fiesta


Awali ya yote tunawapongeza kwa jitihada zenu za kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu kazi zetu za Filamu na Sanaa kwa ujumla.
Kiukweli sisi tukiwa sehemu ya wahusika  katika Wahusika wengi ndani ya tasnia ya Filamu Tanzania, hatuna hiari isipokuwa ni lazima kuwapongeza na kuwashukuru katika harakati na kwa mchango wenu wa kukuza tasnia ya filamu kupitia  habari mbalimbali zinazohusu tasnia ya hii pamoja na kwamba ni wajibu wenu.
 Lakini Pongezi zaidi za dhati tunaziwasilisha kwenu  leo hii (15 .10.2012) moja kwa moja ,kwamba kazi yenu  ya uandishi imetusaidia kwa kiasi kikubwa kufikia maendeleo haya machache  tuliyo nayo, lakini mchango wenu pia si umetusaidia kupata mafaniko tu lakini pia umetusaidia kujifunza mambo  mbalimbali kuhusu filamu za wenzetu na pia kutuonya katika mambo mbalimbali  .
 Ndugu Waandishi wa Habari, tasnia ya filamu ni moja kati ya fani zinazokuwa kwa kasi na kuleta mafanikio  na maendeleo ya baadhi ya vijana wengi wa Tanzania, kutokana na hilo tasnia imekuwa ni moja kati ya maeneo mapya ya ajira kwa raia wa Tanzania na serikali yao kwa ujumla, ni eneo ambalo kwa kiasi kikubwa limechukua rika na jinsia zenye elimu tofauti kwa kusudio la uzalishaji wa filamu bila ya kuzingatia elimu ya muhusika .
 Ndugu Waandishi kutokana na kukua huko, tasnia hii imezalisha Wasanii wa Tanzania ambao sasa wana majina yanayosikika  kila pembe ya nchi yetu, hali hii  imesababisha kuvutia vyombo vya habari kutaka kujua Wasanii wetu wanafanya nini sehemu mbalimbali walizopo.
 Ndugu  Waandishi  mtakumbuka  kwamba  hivi  karibuni kulikuwa tamasha la muziki lililojulikana Serengeti Fiesta ambalo liliandaliwa  na kampuni ya Prime Time Promotion kwa pamoja na Clouds Entertainment za mjini Dar es Salaam,
 Katika matamasha hayo Wasanii kutoka Bongo Movie Club tulialikwa kama wasindikizaji ili kupamba matamsha hayo katika sehemu yalikofanyika. Katika tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika Dodoma baadhi  ya  Waandishi  ambao walihudhuria tamasha lile walifanikiwa kupiga Picha tofauti tukiwa jukwaani.
Baadhi ya picha zilizopigwa katika tamasha lile hazikuwa nzuri kuoneshwa katika hadhara za watu iwe nyumbani au katika vyombo vya habari. Lakini katika hali isiyotarajiwa picha zile zilisambazwa katika mitandao mbalimbali pamoja na kutolewa  katika baadhi ya magazetNdugu Waandishi tunapenda kujulisha umma wa Tanzania kwamba hatujakusudia kupiga tukiwa vile isipokuwa ni mambo ya kiutaalamu katika upigaji wa picha ambapo imechangia kuonekana vile lakini pamoja na upigaji wa picha kuwa wa kiutaalamu zaidi , kwa sababu nyingine ni ya jukwaa lenyewe lilikuwa  refu  zaidi sana.
 Nasi tumeumia sana mioyoni mwetu baada ya kuonekana kwa picha zile kwa sababu sisi kama Wanawake katika jamii tuna Wazazi, ndugu, jamaa , marafiki pamoja mashabiki  mbalimbali wa kazi zetu ambao wanatuheshimu kuliko baadhi ya watu wanavyofikiria , kiukweli hatujafurahia na tumeumia  sana.
 Ndugu Waandishi  wa habari pamoja na yote yaliyo tokea tunachukua nafasi hii kuomba msamaha  kwa Wizara Habari Utamaduni Vijana na Michezo  na taasisi zake , Shirikisho la Filamu Tanzania,Bongo Movie Club na Wadau wake, Familia zetu  na jamii kwa ujumla kutokana na picha zilizopigwa tukiwa katika onesho  la fiesta  ambazo zimesambazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali.
Watanzania  na hasa Wanawake wenzetu kwa kadhia hiyo na tunaahidi kwamba jambo hilo halitajirudia tena  aidha pia tunaomba waandishi sasa waanze kutazama mambo mazuri tuliyoyafanya  na si kutuwinda kwa mabaya kwani sisi ni binadamu na wala si malaika .
 Lakini pia tunapenda kutumia nafasi hii kuvijulisha vyombo vya habari kwamba kuanzia leo tunataka visitumie tena picha hizo na kuziondoa katika mitandao yao  kwa sababu tunaamini kwamba hazileti  mafunzo yoyote katika jamii zaidi tu kwamba zinazidi kupotosha jamii, na ukizingatia lengo kuu la vyombo vya habari kuelimisha na kuburudisha pia.
 Mwisho ni matumaini yetu kwamba tutapewa ushirikiano katika mambo mbalimbali yanayotuhusu na tasnia ya filamu kwa ujumla.
Powered by Blogger.