Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Tuesday, November 13, 2012

GREEN WORLD HEALTH

Watalamu wa Tiba mbadala kwa matatizo ya kiafya yanayo sababishwa na  maisha ya kila siku pamoja  na lishe tunayo sasa   kuwasili jijini tanga kwajili ya kukupatia ufumbuzi wa matatizo yako yanayo kusumbua .

BLOG YA KIKWATOJR.BLOGSPOT.COM ITAENDELEA KUKUPA TARIFA ZAIDI JUU YA WAPI KWA KUWAPATA NA KAZI ZAO WANZO ZIFANYA KWA SASA WAKIWA JIJINI TANGA

Sunday, November 11, 2012

KUTAMBIANA KWA WASHABIKI WA COAST UNION NA YANGA

Yanga leo hawatoki...! Shabiki maarufu wa klabu ya Coastal Union, Ibrahim 'Ibra' akionekana katika Barabara ya 8 jijini Tanga mchana huu baada ya kukamilisha michoro yake mwilini akiwachiomba mkwara Yanga kabla ya kwenda uwanjani kuishangilia timu yake itakayocheza jioni ya leo dhidi ya Yanga kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Novemba 11, 2012. 

Mashabiki wa Yanga wakiandamana na vigoma na vuvuzela katikam maeneo ya stendi kuu ya mabasi jijini Tanga leo ikiwa ni mikwara yao kabla ya kuwavaa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jioni.

Mechi kali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayokuwa ya kumalizia mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kati ya wenyeji Coastal Union na Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo jioni imeandika rekodi baad ya tiketi zake kuuzwa kwa bei 'mbaya' kuliko mechi zote za msimu huu ikiwamo ya mabingwa watetezi, Simba dhidi ya wenyeji hao (Coastal).

Mauzo ya tiketi hizo leo ni Sh. 5,000 kwa kiingilio cha chini (ambazo kufikia saa 9:00 watu walikuwa wakizilangua kwa Sh. 7,000), Sh. 10,000 na Sh. 15,000 kwa kiingilio cha juu wakati katika mechi nyingine zenye mvuto zaidi ikiwamo ya Simba dhidi ya Coastal, viingilio vilikuwa Sh. 4,000, Sh. 7,000 na Sh. 10,000.

Licha ya viingilio hivyo vikubwa, mashabiki walionekana wakichangamkia tiketi hizo kwa wingi, wengine wakitokea jijini Dar es Salaam na baadhi katika maeneo ya jirani ya jiji la Tanga kama Kabuku, Mwakidila, Duga Maforoni, Pangani, Muheza, Korogwe na kwingineko


Saturday, November 10, 2012

mdau kuchukua gamba lake la levo ya diploma ya jounalism Arusha hongera sana

mdau wa blog ya kikwatojr.blogspot.com Beatrice  ishengoma akiwa katika tabasamu safiii
hapa wakiwa katika bozi la kupata pichaBeatrice  ishengoma pamoja na mdau Hepy msemwa baada ya kupada diploma yao ya maswala ya uandishi wa habari na utangazaji.
hawa nao ni miongoni mwa wahitimu wa jounalism katika cho cha Arusha Jounalism Training Collage kilichopo jijini arusha maeneo ya mbauda kwamrombo.
Mdau huyu bwana Amani James akiwa katika masikitiko makubwa baada ya wezake kuweza kumaliza katika chuo hicho nae anachukua levo ya diploma ya jounalizm . blog ya kikwatojr.blogspot.com inawatakia mafanikio mema katika kazi zao za mikono.

Thursday, November 8, 2012

tarime sasa kwaendelea kuchafuka







ARIME.habari na mwandi wa blog kutoka tarime Ahmad nandonde


SERIKALI imetakiwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa mtaa wa Msati kata ya Nyamisangura na Jeshi la wananchi JWTZ Nyandoto Wilayani Tarime ili kuepuka athari zinazojitokeza na kwamba endapo mgogogro huo usipotatuliwa unaweza kuvunja mahusiano mazuri kati ya Wanajeshi na wananchi.



Akiongea na waandishi wa habari  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Sirari Amos Sagara ( CCM) alisema kuwa  Novemba 7 majira ya alfajiri baadhi ya mashamba ya viongozi wa Chadema na wananchi wengine yanadaiwa   kufekwa na wananjeshi wa JWTZ Nyandoto kwa mujibu wa maelezo ya wananchi.



Sagara alisema kuwa kwa sasa wanafatilia  ili kupata ukweli wa watu waliohusika kuharibu na kufeka mazao ambapo pia alisema kitendo cha kufeka mazao ni kukaribisha njaa kwa wananchi hasa waliofekewa mazao ambapo alilaani kitendo hicho kuwa kina rudisha nyuma maendeleo.



Aliongeza kuwa kwa maelezo ya wananchi  wanadai  kuwa chanzo cha mazao  yao kufekwa kinatokana na mgogoro wa ardhi na mipaka kati ya wananchi na wanajeshi ambapo wanajeshi  wanadai kuwa wananchi wamevamia  na kuishi maeneo ya jeshi huku wananchi nao wakidai wao ndio wamiliki halali wa ardhi.



Sagara alisema kuwa endapo Serikali itatatua mgogoro huo kwa kuzingatia taratibu za sheria za ardhi itasaidia kuondoa mgogoro huo wa wanajeshi na wananchi kwani itaonyesha nani mmiliki halali wa ardhi na kwamba endapo eneo  ni lajeshi  kuna haja ya Serikali kuwatafutia maeneo wananchi maeneo mengine ya kuishi.



Mashamba yanayodaiwa kufwekwa na jeshi la JWTZ Nyandoto ni  shamba la Diwani wa kata ya Nyamisangura Thobias Ghat,Mwenyekiti wa mtaaa wa msati kata ya Nyamisangura Zacharia Ghati,mwingine ni Machango Gebeno.
Rorya.



DIWANI wa kata ya Ikoma Wilayani Rorya Mkoani Mara Laurent Adriano( CCM ) amewataka wananchi wa kijiji cha Ikoma kuachana na ukabila badala yake  wafanye maendeleo kwa madai kuwa kuna ukabila kati ya Waluo na Wakurya jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya kijiji.



Adriano alisema  kuwa kijiji cha Ikoma kina mgogoro wa ardhi kati  ya watu wa kabila la wakurya na Wajaruo ambao chanzo chake kianatokana na kutofanyika kwa uhakiki na usajiri kwa Wakurya waliohesabiwa kuwa wana Ikoma Rorya  ili wananchi wa Ikoma wawatambuwe lakini hadi sasa haujafanyika usajiri.



Hayo aliyasema wakati wa mkutano wa wananchi wa Ikoma uliokuwa ukizungumzia usajiri wa Watu  ambao  ni Wakurya ambao walikuwa wakijihesabu kuwa ni Wana Tarime Richa yakuwa Serikali  wakati ilipotenganisha Wilaya ya Rorya na Tarime waliweka mipaka  ambapo wananchi wa kitongoji cha Nyamuhunda ambao ni wakurya walihesabiwa kuwa wana Ikoma –Rorya.

“Kuna ukabila hapa Ikoma  wakati serikali imeweka mpaka wakurya wa nyamuhunda walihesabiwa kuwa Rorya  wakaambiwa wanatakiwa kufanya maendeleo Rorya  lakini nasikitika inapofanyika mikutano ya wananchi hawahudhulii na wala hawafanyi maendeleo ya kijiji lakini mashamba wanayolima  ni ya wanaikoma ambayo walipewa na Mwenyekiti wa kijiji  na aliyekuwa Mtendaji  wa kijiji na wa kata ambao kwa sasa watendaji hao wamehamishwa”alisema Adriano.



Adriano alisema kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa aliagiza Halmashauri ya Rorya kufanya usajiri kwa watu wa Kitongoji cha Nyamuhunda ambao walihesabiwa kuwa wanaikoma  ili waweze kufanya maendeleo Rorya nakwamba nivema sasa usajiri wa watu wa nyamuhunda  ukafanyika ili kuweza kutambuliwa na wananchi wa Ikoma na waweze kufanya maendeleo  kwa kile kilichoelezwa kuwa tayali watakuwa wanafahamika kwa wanaikoma.

COASTAL UNION YANG'ARA NYUMBANI YAIBAMIZA POLISI MORO MOJA BILAMAJIBU


Fulltime-Mkwakwani Stadium Tanga
COASTAL UNION1-0 POLISI MOROGORO
Mfungaji ni Daniel Lyanga


Next match & last league MAtch
COASTAL UNION VS YOUNG AFRICANS(YANGA)
Venue-Mkwakwani Stadium


mkuu wa mkoa wa tanga kuongea na wananchi wa tanga kupitia redio mwambao fm leo asubuhi katika kipindi cha amka na mwambao

mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni Msitafu Chiku Galawa akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za redio mwambao fm mara baada ya kutoka kwenye kipindi.
picha mkuu wa mkoa akibadilishana mawazo na menegar wa redio mwambao fm bwana Hashimu Gulana ofisini .
picha ni mkuu wa mkoa wa Tanga bi Chiku Akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya membara wa redio mwambao fm

Thursday, November 1, 2012

mdau kutoka sweedeni kutembelea kituo cha matangazo cha redio Mwambao fm Tanga

Badhi ya wafanyakazi wa Redio mwambao fm iliyopo jijini Tanga wakiwa na katika picha ya pamoja na mdau kutoka nchini Sweedeni Baba na mama kamila kutoka Nchini Swedeni amabo kwa sasa wako jijini Tanga kwa PROJECT  mbalimbali.

Meneja wa kituo cha redio Mwambao Bwana Hashimu Gulana akibadilishana Mawazo na wageni hao ofisini hapo


Powered by Blogger.