Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Thursday, September 6, 2012


Chama cha CUF Tanzania kimesema kupatiwa usajili wa kudumu kwa chama kipya cha ADC ambacho wanachama na viongozi ni wale waliotoka chama hicho cha CUF hakumaanishi ushawishi wa chama hicho sasa umefika mwisho wake.
Akizungumzia kusajiliwa kwa chama hicho mwenyekiti wachama cha wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba hata hivyo ametilia wasiwasi namnachama hicho kilivyopata usajili wa kudumu tofauti na inavyokuwa kwavyama vingine vya siasa.
      picha kwaniaba ya mpiga picha wangu suleimani kibugo ze kankaraaa

Viongozi mbalimbali wakichangia agenda mbalimbali katika kikao cha viongozi wa mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Tanga . mkuu wa mkoa wa tanga vakifungua kikao cha viongozi wa mkoa.

 picha ya juu ni ya mkuu wa wilaya ya muheza bi subila mgalu na picha ya chini ni ya mkuu wa wilaya ya kilindi bwana  sulemani liwowa

picha hapo juu ni baadhi ya wandishi wa habari ambao wamehudhuria katika mkutano huo mkubwa ulio wajumuisha viongozi mbalii mbali wa mkoa wa tanga ukiwa na lengo la kutoa tathimini kuhusu sensa katika mkoa wa tanga  na maendeleo mazima ya mkoa wa tanga .
    picha kwa niaba ya mpiga picha wa blog suleimani kibugoo ze kankaraaaaa.


Wednesday, September 5, 2012

IGP  KUTETA NA VIGOGO WA POLISI PAMOJA NA  VIONGOZI CHADEMA,HUKU DK NCHIMBI AKATISHA ZIARA AREJEA NCHINI
NA Waandishi WA Blog
TUKIO la kuuawa kwa mwandishi wa habari wakati polisi wakipambana na wafuasi wa Chadema mkoani Iringa, limelitikisa jeshi hilo na jana Mkuu wake (IGP), Said Mwema alilazimika kujifungia na vigogo wa polisi Mkoa wa Iringa kujadili suala hilo.

Wakati IGP Mwema akifanya mkutano huo, uliodumu kwa zaidi ya saa mbili na nusu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi amelazimika kukatisha ziara yake ya kikazi Afrika Kusini na kurejea nchini kushughulikia suala hilo.

Mwema alienda Iringa jana na kuitisha mkutano huo uliowahusisha pia viongozi wa Chadema, akiwamo Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa katika mazingira yaliyoelezwa kuwa na ulinzi mkali.
Hii ni mara ya kwanza IGP Mwema kwenda mwenyewe kwenye mikoa kunakotokea vurugu kati na vyama vya siasa na baadaye mauaji ya raia.

Julai 15, mwaka huu vurugu za aina hiyo zilitokea mkoani Singida ambako Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Ndago wilayani Iramba, Yohana Mpinga aliuawa kwa kupigwa na silaha za jadi.

Pia mkoani Morogoro, Ally Zona aliuawa katika vurugu zilizoibuka baina ya polisi na wafuasi wa Chadema katika haraka za jeshi hilo kuwasambaratisha wafuasi hao kwa kile ilichoeleza kuwa maandamano yao yalipigwa marufuku.
Katika vurugu zote hizo, IGP amekuwa akituma wawakilishi au kutumia polisi kwenye mkoa husika kushughulikia matatizo hayo.

Makubaliano ya kikao
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zimeeleza kuwa polisi imekubaliana na Chadema na Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kusitisha majadiliano yote yanayohusu kifo cha mwandishi huyo hadi mazishi yake yatakapokamilika.

Mwenyekiti wa UTPC, Kenneth Simbaya alisema baada ya mkutano huo kuwa wamekubaliana kuwa na mkutano mwingine baada ya shughuli za mazishi kukamilika.

“Tulichoomba kifanyike ni kwamba, tumzike mwenzetu halafu majadiliano mengine juu ya ilikuwaje kwa nini na nini kifanyike kwa siku za usoni yatakuja,” alisema Simbaya.
Alisema sasa wanasubiri mwili wa Mwangosi ufanyiwe uchunguzi na wataalamu kutoka Dar es Salaam kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Francis Godwin alisema uchunguzi wa awali wa IPC unapingana kwa asilimia zote na taarifa ya jeshi hilo kwa kuzingatia taarifa zilizotolewa na baadhi ya waandishi waliokuwapo katika tukio hilo.

“Taarifa kutoka katika vyanzo vyetu zinaonyesha kwamba Mwangosi alipigwa kwa virungu kabla ya kulipuliwa na bomu hilo ambalo kwa vyovyote vile mhusika wake mkuu anaweza kuwa jeshi hilo na ili taarifa hiyo potofu isiendelee kuugubika umma, IPC imeamua kutoa tamko linalolenga kuviarifu vyombo huru viingilie kati uchunguzi,” alisema Godwin.

                                Nchimbi akatisha ziara

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi jana alilazimika kukatisha ziara yake ya kikazi, Afrika Kusini na kurudi nchini ambako pamoja na mambo mengine, atazungumza na waandishi wa habari leo kuhusu tukio hilo.
Nchimbi anarejea nchini wakati Naibu wake, Pereira Ame Silima akikataa kulizungumzia akisema uchunguzi umeshaanza.
Silima alisema tukio hilo linachunguzwa kwa pamoja kati ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba na IGP Mwema... “Mwema na Manumba wanaelekea Iringa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa tukio hilo na baadaye ndipo jeshi la polisi litaweza kueleza ni kitu gani hasa kimetokea.”
Alisema kwa sasa lolote litakalozungumzwa juu ya tukio hilo litakuwa ni hisia tu na ukweli utajulikana baada ya uchunguzi huo kukamilika.

Channel Ten yanena
Uongozi wa kampuni ya Africa Media Group ambao wanamiliki Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, umeitaka Serikali kuanzisha uchunguzi huru ili kubaini sababu na mazingira ya kuuawa kwa mwandishi huyo ambaye alijiunga na kampuni hiyo mwaka 2006.

Taarifa iliyotolewa na kampuni na kusainiwa na Mhariri Mkuu wa Channel Ten, Dina Chahali imetaka uchunguzi huru kufanyika na kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
“Tunalaani vikali tukio hili ambalo halikubaliki kwa jinsi yoyote ile, tunataka kuanzishwa uchunguzi huru na hatimaye nguvu za kisheria zitumike,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
           kutoka kwa kikwatojr.blogspot.com
|

Chadema sasa kumfikisha Nape mahakamani 


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeazimia kwenda mahakamani wiki hii kumshtaki Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye (pichani), baada ya kushindwa kukiomba radhi chama hicho pamoja na kutoa faini ya Shilingi bilioni tatu, baada ya kupita kwa muda aliopewa kufanya hivyo.


Akizungumza na kikwatojr.blogspot.com kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Chadema, Anton Komu, alisema chama hicho hivi sasa kinakamilisha taratibu za kisheria ili kwenda mahakamani.

Alisema "wakati wowote wiki hii tutakwenda mahakamani, leo jioni (jana) nitakutana na mawakili ambao wanashughulikia jambo hilo."

Komu alisema imelazimu suala hilo kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa Nape amekataa kuomba radhi kuhusu madai aliyoyatoa.

Chadema ilimtaka Nape aombe radhi baada ya kukituhumu kwamba kimekuwa kikichangisha fedha kwa wananchi katika mikutano yao wakati kinapokea mabilioni ya fedha kutoka nje ya nchi.

Nape alitoa tuhuma hizo Agosti 12 na kueleza kwamba anao ushahidi kuwa chama hicho kimekuwa kikiwahadaa wananchi kwa kuwachangisha fedha huku kikipokea mabilioni ya fedha kwa wafadhili kutoka nje na kwamba upo uwezekano wa chama hicho kupewa fedha hizo kwa mikataba yenye masharti ya kuiweka nchi rehani.

Baada ya kauli hiyo, bodi ya wadhamini wa Chadema iliagiza wanasheria wake wamwandikie Nape barua ya kumtaka kukiomba radhi chama, kwa kutumia vyombo vya habari.

Chadema inataka kuombwa radhi na fidia ya fedha ni kwa ajili ya fedheha na fundisho kwa kitendo cha uzushi na uongo kilichotolewa na Nape.

Monday, September 3, 2012




TAARIFA YA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF)

KWA VYOBO VYA HABARI

KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI


UTANGULIZI:
1. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limepokea kwa masikitiko makubwa kifo 
cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.

2. Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini jana, Septemba 2, 2012, wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

3.Tukio hili linaiingiza Tanzania katika historia mbaya ya ukiukwaji na ukandamizwaji wa uhuru wa habari, kwani ni kwa mara ya kwanza tunashuhudia mwandishi wa habari AKIUAWA WAKATI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIHABARI.

4. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti saa 9.30 alasiri katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio. Na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.

5. Kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania, TEF tumechukua hatua za haraka za kuunda timu ya uchunguzi wa suala hilo, ambayo itakwenda mkoani Iringa mapema kadri itakavyowezekana, ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Lengo la uchunguzi huo ni kuweka kumbukumbu sahihi (documentation) ya tukio hilo la aina yake katika historia ya nchi yetu.

6.Matokeo ya uchunguzi huo pamoja na mwingine unaofanywa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), ndiyo yatakayotoa mwelekeo wa hatua ambazo TEF inachukua dhidi ya Jeshi la Polisi katika siku chache zijazo.

MTIZAMO NA MSIMAMO WA TEF
Kwa kuzingatia taarifa kutoka Iringa na zile za vyombo vya habari vya jana (Jumapili, Septemba 02, 2012) na leo (Jumatatu, Septemba 03, 2012), TEF ina mtizamo na msimamo kama ifuatavyo:

1. Kwanza tunalaani vikali tukio la kupigwa, kisha kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi ambalo limeigusa tasnia ya habari kwamba sasa pengine waandishi wa habari ni malengo “target ya polisi” wanapokuwa kwenye kazi zao.

2.Ieleweke wazi kwamba matukio haya siyo yanaondoa imani ya waandishi wa habari kwa jeshi la polisi tu, bali yanaweza kuwa chanzo cha uhasama na ufa mkubwa ambao utawanyima wananchi nafasi ya kutumikiwa na pande mbili ambazo zinategemeana.

3. Kwa matukio ya aina hii, tunadhani wakati mwafaka kwa uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuwajibika, kuazia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa na uongozi wa Makao Mkuu, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema.

4.Tunasema hivi kwani kuna kila dalili kwamba polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine na tukio au/na matukio yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, kwani kitendo cha kumzingira tu na kumshambulia kinathibitisha kwamba hawakuwa na nia njema hata kidogo dhidi ya mwandishi huyu.

5.Taarifa ambazo TEF tunazo, pia  zinadai kwamba kulikuwa na mpango wa polisi wa “kuwashughulikia waandishi wa habari watatu” (Mwangosi) akiwa mmojawapo na hilo lilionekana likitekelezwa kwa polisi kumshambulia mwandishi huyo, baadaye alipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.

6. Hili linatiliwa nguvu na tukio jingine la polisi kumpiga na kumjeruhi  mwandishi mwingine, Godfrey Mushi ambaye ni mwakilishi wa gazeti la Nipashe mkoani Iringa. Mwandishi wa tatu ambaye hadi tunapoandika taarifa hiyo yumo katika mpango wa ‘kushughulikiwa na polisi’ ni Francis Godwin ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea.

7.Vitendo vya aina hii havivumiliki na havipaswi kuachwa kuendelea kwani ni hatari kwa ustawi wa demokrasia na uhuru wa habari nchini. Hatuwezi kuendelea katika mazingira ambayo polisi wanageuka kuwa chombo cha mauaji ya raia badala ya kuwa walinzi wa raia.

8. Kwa maana hiyo, mbali na uchunguzi ambao utafanywa na polisi, tunatoa wito kwa Serikali kuunda chombo huru, ambacho kitabaini ukweli, na matokeo yake yatangazwe kwa umma, huku wahusika wa aibu hiyo wakichukuliwa hatua za kisheria. Tunasema hivyo, tukifahamu kwamba tayari kuna jitihada za kuficha ukweli na kueneza propaganda za uongo kuhusu tukio zima.

9.Mwenendo wa aina hii wa chombo cha dola kuamua kutumia silaha kuua na baadaye kupanga mbinu chafu za kuficha ukweli ni hatari kwa Taifa, na unaiweka demokraisia ya nchi yetu njia panda, huku tukielekea katika hatari ya Taifa kutumbukia katika uovu.


IMETOLEWA NA:

NEVILLE MEENA,
KATIBU MKUU – JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)
SEPTEMBA 3, 2012
habarizote kwaniaba ya kikwatojr.blogspot.com
Powered by Blogger.