Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Monday, October 15, 2012

bunge la nchi ya libya lamchagua waziri mkuu mpya

Bunge la taifa la Libya jana lilimchagua Waziri Mkuu Mpya, huyo akiwa Waziri Mkuu Mpya wa pili kuwahi kuchaguliwa katika muda wa mwezi mmoja ambaye atakabiliana na changamoto za kuunda serikali itakayokubaliwa na mirengo mingi ya nchi hiyo. Ali Zeidan mwanadiplomasia wa zamani ambaye alielekea uhamishoni mwaka 1980 na kuwa mkosoaji wa Muammar Gaddafi kiongozi wa zamani wa Libya amechaguliwa wiki moja tu baada ya Waziri Mkuu aliyemtangulia kuachishwa kazi baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye. Musatafa Abu Shagur alifutwa kazi baada ya orodha yake ya mawaziri aliowapendekeza kukabiliwa na upinzani wa bunge na nje ya taasisi hiyo.

mapigano kongo sasa basi?


Wapinzani nchini Kongo wametaka kukomeshwa vita huko mashariki mwa nchi hiyo kufuatia kuendelea mapigano katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini.  Lucien Mbusa Katibu Mkuu wa Harakati ya Ukombozi wa Kongo amesisitiza kwamba wapinzani nchini Kongo wanataraji kuwa Ufaransa itatumia ushawishi ilionao katika taasisi za kimataifa na hivyo kufanya juhudi za kumaliza mapigano mashariki mwa nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lucien Mbusa ambaye ni mjumbe wa wapinzani katika bunge la Kongo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Francois Hollande wa Ufaransa mwishoni mwa kikao cha Francophone mjini Kinshasa.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ukombozi wa Kongo amesifu matamshi ya Rais wa Ufaransa  kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo ni yenye kutia shaka,  kwamba kuna ukiukaji wa haki za binadamu na pia raia wa Kongo wanafungwa jela bila ya kuhukumiwa.

AWASIFIA Rooney, Van Persie kuwa WAJANJA KISOKA!


Beki wa Arsenal Laurent Koscielny amemshambulia Straika wa Liverpool Luis Suarez na kumwita ni mdanganyifu anaejidondosha kwa kusudi ili ahadae Marefa na kupata Penati.
Katika Wiki za hivi karibuni Suarez amekuwa akishambuliwa kutoka kila kona kuanzia kwa Meneja wa Stoke City Tony Pulis ambae mwanzoni mwa Mwezi huu alitaka Chama cha Soka England, FA, kimwadhibu Straika huyo kutoka Uruguay kwa udanganyifu.
FIFA nao, kupitia Makamu wao wa Rais, Jim Boyce, wakaingia kundini wakitaka mabadiliko ya Sheria ili FA iweze kuadhibu kwa vitendo kama hivyo baada ya kuviita ni ‘kansa katika gemu.’
Lakini Suarez hakukaa kimya na nae akajibu huku UAF, Chama cha Soka cha Uruguay, kikiingilia na kuitaka Kamati ya Maadili ya FIFA imchunguze Jim Boyce kwa kauli yake kuhusu Suarez lakini sasa nae Laurent Koscielny kabeba bango kumtuhumu Suarez.
Akiongea na Gazeti la Ufaransa L'Equipe, Koscielny alihoji: “Nani ni Fowadi ninaemchukia? Suarez. Anachosha kulinda kwa sababu ni mdanganyifu. Atakuvuta Jezi, atakupiga. Wakati wote unataka kumfyatua teke lakini unaogopa Kadi Nyekundu.”
Koscielny amekiri kuwa aliekuwa Straika wa Chelsea Didier Drogba ndie alikuwa akimvutia kwa Mastraika na amesema: “Alikuwa na nguvu, anacheza vizuri akilipa mgongo goli, mpiga vichwa mzuri na mwepesi kutafuta upenyo. Vilevile, yeye ni mlinzi wa kwanza kama tulivyoona alipowasimamisha Barcelona.”
Alipoulizwa kuhusu Wayne Rooney, Koscielny alisema: “Ni mjanja sana ingawa Robin van Persie ni mjanja zaidi. Lakini Rooney mara nyingi anashuka kwenye Kiungo. Rooney anapenda mpira na kutoa misaada kwa pasi.”

hussein-machozi-kutoa-nyimbo-mpya.


NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein Rashid ‘Hussen Machozi’ amesema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao chake kipya ambacho bado hajakipatia jina.
Akizungumza jijini Dar es Salaam alisema kutokana na ubora wa wimbo huo anapata tabu kujua aupe jina gani na anaimani mwisho wa mwezi huu utaanza kusikika redioni.
“Unajua kazi ikiwa freshi inakua tabu kutafuta jina la wimbo, hivyo nipo kwenye mchakato wa kutafuta ikibidi nitaomba ushauri kwa wasanii wengine,” alisema Hessein Machazi.
Alisema kikubwa kinachotakiwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki na kwamba wasicheze mbali na yeye kuna vitu vingi ambavyo amewaandalia.
Mbali na kibao hicho, Hussen Machozi kwa sasa anatamba n akibao chake cha ‘Addicted’ ambacho kinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.

Saturday, October 13, 2012

COASTAL UNION YAWAVUTA NDEVU MSIMBAZI

Wagosi wakaya kutoka jiji tanga Coastal union hii leo wameweza kuutumia vilivyoo uwanja wao wa nyumbani kwa kuweza kuwadindia mnyma Simba aliye funga safari kutoka jijini dar es salam kwa kuweza kutoka suluhu ya bila bila katika muendelezo wa ligi ya voda kom
pichani wa kwanza kushoto  ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ya simba wakatikati ni afisa habari wa kilabu ya msimbazi ezekieli kamwaga na wamwisho ni mfanyakazi kutoka vodakom ambao ndio wazamini wa ligi hiyo wakijadiliana jambo kabla ya mechi kuanza katika uwanja wa mkwamkwani jijini tanga.
umati wa mashabiki mbali  walifurika katika uwanja wa mkwakwani kuweza kucheki burudani baina ya wagosi wa kaya na mnyama simba ambapo hadi kipenga kinapulizwa kuashiria tamati ya mechi hakuna mbabe katika mechi hiyo.
picha na mwandishi wa blog oscar asenga toka tanga)

inspekta-jenerali-wa-polisi-said-a-mwema-atoa-taarifa-kuhusu-mauaji-ya-aliyekuwa-kamanda-wa-polisi-mkoa-wa-mwanza-

MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA (IGP) SAID.A.MWEMA AKITOA TAARIFA YA KIFO CHA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) LIBERATUS BARLOW KILICHOSABABISHWA NA KUPIGWA RISASI ENEO LA KITANGIRI MKOANI MWANZA.

Napenda kutumia fursa hii kuwapa taarifa kuhusu tukio la mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa Polisi Liberatus Barlow yaliyofanywa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo tarehe 13/10/2012 majira ya saa saba usiku Mkoani Mwanza.
 2. Tukio hilo limetokea wakati kamanda huyo akitokea kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake eneo la Frolida hotel Mwanza mjini, akiwa na ndugu yake waliyeongozana nae kutoka kwenye kikao hicho. Wakati akimshusha huyo ndugu yake eneo la Kitangiri Minazi Mitatu, walitokea watu wanaosadikika kuwa ni majambazi, na kumvamia na kuanza kumshambulia kwa risasi na kumuua papohapo.
 3. Ndugu wananchi, kufuatia tukio hilo, tayari nimemtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Robert Manumba kwenda mkoani Mwanza kwa lengo la kuimarisha ulinzi na upepelezi wa tukio hilo.
 4. Najua tukio hili limetushitua na kutuhuzunisha wote. Hivyo, wakati tukiendelea na taratibu zingine kuhusiana na tukio hilo, niwaombe wananchi wote kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, utakaowezesha kuwabaini wahalifu hao.
 5. Tutaendelea kuwapa taarifa za tukio hilo, kadri tutakavyoendelea kuzipata.

k-lyn ajifungua watoto mapacha

blog ya kikwatojr inampa hongera bibie k-lynn kwa kupata kinda
Powered by Blogger.