PALACE HOTEL
Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218
Monday, October 29, 2012
TFF YASAKA MILIONI 225 ZA KUIPELEKA MOROCCO SERENGETI BOYS
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inahitaji zaidi ya Sh Milioni 225 kwa ajili ya kampeni yake iliyobakia ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya TFF, Ilala, Dar es Salaam, Tenga alisema kwamba shirikisho lake kwa sasa halina fedha hizo, kwa sababu hiyo haina mdhamini, zaidi ya kutegemea misaada ya wadau.
Tenga alisema tayari Kamati ya Vijana ya TFF imekwishakutana kuweka mikakati ya kuiwezesha Serengti kushiriki vema kampeni hizo, ikiwemo kuunda Kamati ya kuisaidia timu hiyo.
Hata hivyo, Tenga hakuitaja Kamati iliyoundwa kwa sababu bado hawajazungumza na Wajumbe walioteuliwa.
Alisema kocha wa timu hiyo, Mdenmark Jacob Michelsen ameomba mechi za kujipima nguvu kabla ya kucheza na Kongo Brazaville kuwania tiketi ya Morocco na Kamati ya Vijana inahangaikia suala hilo kwa sasa.
Alisema tayari kuna mwaliko kutoka Botswana wa Serengeti kwenda kucheza, lakini kutokana na ukosefu wa fedha wanashindwa hadi sasa kutoa jibu.
Kikosi cha wachezaji 25 cha Serengeti Boys kipo kambini mjini Dar es Salaam tangu Oktoba 21, mwaka huu kujiandaa na mechi hiyo, ya kwanza ikichezwa nyumbani Novemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.
Tanzania imefuzu bila jasho hadi kufika hatua hiyo, baada ya wapinzani wake wa awali, Kenya na Misri kujitoa katika Raundi ya Kwanza na ya Pili.
Kama Tanzania itafuzu kushiriki Fainali hizo za mwakani, itapoza machungu ya mwaka 2005 walipofuzu kucheza Fainali za Vijana wa umri huo kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, lakini baadaye kwa sababu ya ‘kufoji’ umri wa Nurdin Bakari, ikaondolewa mashindanoni.
Zaidi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 1980 na CHAN 2009, katika soka ya wanaume, Tanzania haijashiriki fainali nyingine zozote za Afrika tangu iingie kwenye soka ya kimataifa.
mama chiku Gallawa kuwa mgeni rasmi taifa cup Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mama Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michuano ya Kombe la Taifa ya mpira wa Kikapu, Taifa Cup mwaka 2012 yanayotarajiwa kuanza kesho kwenye viwanja vya Mkwakwani na Harbours Club vilivyo jijini Tanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanga (TRBA), Hamisi Jaffary alisema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na waamuzi kumi na mbili ambao watachezesha mashindano hayo tayari wameshawasili jijini hapa tokea mwishoni mwa wiki.
Jaffary alisema mashindano hayo yataanza Octoba 29 na kufikia tamati Novemba 5 mwaka huu na kushirikisha mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo mpaka juzi mikoa kumi na sita ilikwisha kuthibitisha kushiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti huyo aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar ,Arusha,Moshi,Iringa, Mbeya,Mara, Lindi,Shinyanga,Tabora,Dodoma na Tanga ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo ambapo alisema timu nyengine huenda zitathibitisha katika shirikisho la mipira wa kikapu Taifa ikiwemo Zanzibar ,Unguja na Pemba.
Alisema mkoa wa Kigoma walijitoa dakika za mwishoni kushiriki mashindano hayo ambayo msimu huu idadi ya washiriki imeongezeka kutokana na kuongezwa kwa idadi ya mikoa.
Mashindano hayo wa mara ya kwanza yalifanyika jijini Tanga 1989 na mara ya mwisho ili kuwa ni 2005 msimu huu shamra shamra zimeonekana kuwa ni muda kubwa kutokana na kuwa maandalizi ya maandalizi yanayofanywa na mikoa shiriki huku viwanja ambazo zitatumika mashindano zimefanyiwa ukarabati wa hali ya juu.
Mkoa wa Tanga unatarajiwa kuwa na wageni watapao 450 ikiwemo wachezaji na viongozi wa timu ambazo zitashiriki michuano hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo.
Aliongeza kuwa timu zilianza kuwasili jijini Tanga tokea Jumamosi na Jumapili ambapo kesho ndio ufunguzi rasmi wa mashindano hayo.
Sunday, October 28, 2012
mama wa mtoto aliye kojolea kitabu takatibu cha Qurani aomba razi kwa waisilamu
Mama wa kijana aliyekojolea kitabu kitukufu cha Quran na kusababisha tafrani kubwa hapa nchini hatimaye amejitikeza na kuomba radhi i kwa kitendo hicho na kusema hakikupaswa kufanywa na jamii yoyote ulimwenguni.
Katika mahojiano maalumu aliyofanya na gazeti moja siku ya jumamosi bi Teresia Josephat amesema hakuwa kutegemea kama kitendo hicho kingelifanywa na mwanae Emmanuel Josephat (14
kwa kuwa hakumkuza katika malezi aina hiyo
Wiki mbili zilizopita ,katika mabishano ya rika kati ya kijana huyo na wenzake yalimfanya kijana huyo kukidhihaki kitabu kiutufu cha kuruani kwa marai kwamba angelifanywa hivyo angeweza kugeuka mnyama
Kitendo ambacho kilisababisha mlolongo ghasia kati ya vijana wa kiislamu na polisi na kukupelekea kuharibiwa kwa mali pamoja na uchomaji wa makanisa katika eneo la Mbagala jijini dar es salaam
Saturday, October 27, 2012
KAULI YA BWANA MISOSI KWAWOTE WANAOMPA USHIRIKIANO WAKATI HUU WAMSIBA WA KAKA YAKE MAREMU Emanuel Gabriel Rushahu!
Mambo
vipi ndugu zangu asanteni kwa kunifariji' najua wapo wengi wangependa
kuhudhuria mazishi ila kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao
watashindwa kuhudhuria mazishi leo siku ya ijumaa tar 26 oct, ila kwa rambi
rambi zao kwa marehemu kaka yangu Emanuel Gabriel Rushahu wanaweza
kutumia na hii M pesa 0763558855 nitaiwakilisha kwa familia katika daftari
la michango na mwili tutauaga hapahapa nyumbani kinyerezi mida ya saa
sita mchana pia misa ya mazishi ni saa nane mchana katika kanisa katoliki
segerea na tutampumzisha katika makaburi ya hapohapo segerea..
SIRI YANGU YA KUTUMIA LAFUDHI YA KIMASAI
HATIMAYE msaani maarufu wa vichekesho nchini, Gilliady Severine a.k.a Masai Nyotambofu, ametoa siri yake ya kutumia lafudhi ya jamii ya Kimasai katika kazi yake ya sanaa ya maigizo na vichekesho.
Akizungumza na blog hii jijini hapa juzi, Nyotambofu alisema kuwa, yeye aliamua kutumia lafudhi ya Kimasai baada ya kubaini kuwa ni ngumu na hata waliyokuwa wakijaribu kuitumia katika sanaa mbalimbali, hawakuweza kukidhi mahitaji ya lafudhi ya lugha hiyo. Msanii huyo amekuwa akisikika katika matangazo mbalimbali yanayorushwa na vituo vya radio hapa nchini, hasa ya uhmasishaji wa kuacha pombe, yaani ‘ulevi noma’ lilitolewa na Idara ya Ustawi wa Jamii wakishirikiana na Jeshi la Polisi. “Ndugu mwandishi, niliamua kutumia lafudhi ya Kimasai, kwani nilishafanya utafiti na kubani kuwa, lugha hii ni ngumu kuiga, pia niliangalia wasanii ambao walikwisha kujaribu kuitumikia lafudhi ya Kimasai, nikaona hawajakidhi kabisa ndipo nikaamuua kuitumia na mpaka sasa najivunia nimeweza,” alisema Masai Nyotambofu. “Hata hivyo, ilibidi niongeza juhudi na kujituma katika kuitumia lafudhi hii baada ya kupewa zawadi ya fimbo na mgolole na wazee katika Wilaya ya Ngorongoro, baada ya kuona nimeweza kuimudu lafudhi yao tofauti na wasanii waliokwisha kuwahi kuitumia katika maigizo na muziki,” alisema na kuongeza: “Kilichonitia moyo na kuongeza juhudi katika kutumia lafudhi hii, mwaka 2010 nilikwenda Ngorongoro kufanya onyesho na mwanamuziki Banana Zoro, ilikuwa sikukuu ya wafanyakazi, ndipo wazee wa Kimasai wakaridhika na kazi yangu wakanizawadia huo mgolole na fimbo, mpaka sasa ndivyo ninavyovitumia,” alisema Masai Nyotambofu. Msanii huyo maarufu, ambaye ni Muha kutoka Kigoma, yupo jijini Mbeya kwa ajili ya kurekodi vipindi vya ‘Vituko Show’ vinavyorushwa na kituo cha televesheni ya Channel Ten.
Tuesday, October 23, 2012
shirika la mfuko wa taifa wa bima ya afya lashauriwa kuongeza ufanisi katika kuboresha huduma zake
picha ni wakina mama washiriki wilayani Muheza wakiwa wanafatilia mafunzo kwa umakini
(hao pia ni mingoni mwa washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya unyanyasaji yanayoendeshwa kwa ufadhili wa Shirika la INUKA na SWAT )
SHIRIKA la Mfuko wa taifa wa Bima ya afya limeshauriwa kuongeza ufanisi kwa kuboresha huduma zake zaidi ili kuondoa usumbufu na malalamiko kwa wanachama wake.
(hao pia ni mingoni mwa washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya unyanyasaji yanayoendeshwa kwa ufadhili wa Shirika la INUKA na SWAT )
SHIRIKA la Mfuko wa taifa wa Bima ya afya limeshauriwa kuongeza ufanisi kwa kuboresha huduma zake zaidi ili kuondoa usumbufu na malalamiko kwa wanachama wake.
Hayo yalielezwa na washiriki
wa mafunzo ya siku tatu ya unyanyasaji yanayoendeshwa kwa ufadhili wa Shirika
la INUKA na SWAT na kufanyika kwenye ukumbi wa kanisa la Elimu
Pentacost la Masuguru Mjini Muheza.
Washiriki hao ambao wengi
wao ni walimu, walilalamika kuwa huduma za bima ya afya bado hazijatengemaa
vema na kwamba kuna haja kwa wahusika kujipanga na kuhakikisha kuwa wanachama
wake wanapata wanachotarajia ipasavyo.
Walidai kuwa licha ya
kukatwa fedha nyingi kila mwezi lakini fedha wanazotozwa haziendani
na huduma zinazotolewa jambo walilolieleza kuwa linawafanya wakate tama
na kujutia michango yao.
Kwamujibu wa washiriki hao
ni kwamba wanalazimika kutoa michango yao kila mwezi lakini hawapati huduma
wanayotarajia na badala yake wanapokwenda hospitali wanatakiwa kulipia
dawa na vipimo vingine na hivyo kupata gharama kubwa.
Mambo mengine yaliyojitokeza
kwenye mafunzo hayo ni pamoja na malalamiko zidi ya Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Muheza kudaiwa kutoa siri kwa
kuwataja kwa waharifu watu wanaojitoa kupeleka taarifa za makosa
hayo katika ofisi zao.
Aidha washiriki hao
walilalamikia unyanyasaji katika jeshi la polisi.Mahakama pamoja na
watendaji mbalimbali katika maofisi ya serikali na binafsi na kwamba
wamekuwa wakipata manyanyaso kwenye ajira kwa upendeleo wenye mazingira ya
rushwa.
Awali mkufunzi wa mafunzo
hayo Nestory Ngwega alitumia muda mwingi kueleza haki za msingi za binaadamu
ambazo zisipofuatwa ndipo tendo la unyanyasaji hutokea na kwamba haki hizo zipo
kwenye makundi mawili ambayo ni haki ya kikatiba na ile ya kibinaadamu ambayo
haiondolewi na mtu yeyote Yule kwa nafasi yake ama uwezo wa kifedha.
Mengine yaliyojadiliwa
katika mafunzo hayo ni unyanyasaji ndani ya familia na kwa wanandoa
pamoja na vyanzo vyake na jinsi ya kukabiliana navyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Powered by Blogger.






