Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Thursday, November 8, 2012

COASTAL UNION YANG'ARA NYUMBANI YAIBAMIZA POLISI MORO MOJA BILAMAJIBU


Fulltime-Mkwakwani Stadium Tanga
COASTAL UNION1-0 POLISI MOROGORO
Mfungaji ni Daniel Lyanga


Next match & last league MAtch
COASTAL UNION VS YOUNG AFRICANS(YANGA)
Venue-Mkwakwani Stadium


mkuu wa mkoa wa tanga kuongea na wananchi wa tanga kupitia redio mwambao fm leo asubuhi katika kipindi cha amka na mwambao

mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni Msitafu Chiku Galawa akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za redio mwambao fm mara baada ya kutoka kwenye kipindi.
picha mkuu wa mkoa akibadilishana mawazo na menegar wa redio mwambao fm bwana Hashimu Gulana ofisini .
picha ni mkuu wa mkoa wa Tanga bi Chiku Akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya membara wa redio mwambao fm

Thursday, November 1, 2012

mdau kutoka sweedeni kutembelea kituo cha matangazo cha redio Mwambao fm Tanga

Badhi ya wafanyakazi wa Redio mwambao fm iliyopo jijini Tanga wakiwa na katika picha ya pamoja na mdau kutoka nchini Sweedeni Baba na mama kamila kutoka Nchini Swedeni amabo kwa sasa wako jijini Tanga kwa PROJECT  mbalimbali.

Meneja wa kituo cha redio Mwambao Bwana Hashimu Gulana akibadilishana Mawazo na wageni hao ofisini hapo


Monday, October 29, 2012

Track| Nataka-Kulewa Diamond.



TFF YASAKA MILIONI 225 ZA KUIPELEKA MOROCCO SERENGETI BOYS


RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inahitaji zaidi ya Sh Milioni 225 kwa ajili ya kampeni yake iliyobakia ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya TFF, Ilala, Dar es Salaam, Tenga alisema kwamba shirikisho lake kwa sasa halina fedha hizo, kwa sababu hiyo haina mdhamini, zaidi ya kutegemea misaada ya wadau.
Tenga alisema tayari Kamati ya Vijana ya TFF imekwishakutana kuweka mikakati ya kuiwezesha Serengti kushiriki vema kampeni hizo, ikiwemo kuunda Kamati ya kuisaidia timu hiyo.
Hata hivyo, Tenga hakuitaja Kamati iliyoundwa kwa sababu bado hawajazungumza na Wajumbe walioteuliwa.
Alisema kocha wa timu hiyo, Mdenmark Jacob Michelsen ameomba mechi za kujipima nguvu kabla ya kucheza na Kongo Brazaville kuwania tiketi ya Morocco na Kamati ya Vijana inahangaikia suala hilo kwa sasa.
Alisema tayari kuna mwaliko kutoka Botswana wa Serengeti kwenda kucheza, lakini kutokana na ukosefu wa fedha wanashindwa hadi sasa kutoa jibu.
Kikosi cha wachezaji 25 cha Serengeti Boys kipo kambini mjini Dar es Salaam tangu Oktoba 21, mwaka huu kujiandaa na mechi hiyo, ya kwanza ikichezwa nyumbani Novemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.
Tanzania imefuzu bila jasho hadi kufika hatua hiyo, baada ya wapinzani wake wa awali, Kenya na Misri kujitoa katika Raundi ya Kwanza na ya Pili.
Kama Tanzania itafuzu kushiriki Fainali hizo za mwakani, itapoza machungu ya mwaka 2005 walipofuzu kucheza Fainali za Vijana wa umri huo kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, lakini baadaye kwa sababu ya ‘kufoji’ umri wa Nurdin Bakari, ikaondolewa mashindanoni.
Zaidi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 1980 na CHAN 2009, katika soka ya wanaume, Tanzania haijashiriki fainali nyingine zozote za Afrika tangu iingie kwenye soka ya kimataifa.

mama chiku Gallawa kuwa mgeni rasmi taifa cup Tanga


MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mama Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michuano ya Kombe la Taifa ya mpira wa Kikapu, Taifa Cup mwaka 2012 yanayotarajiwa kuanza kesho kwenye viwanja vya Mkwakwani na Harbours Club vilivyo jijini Tanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanga (TRBA), Hamisi Jaffary alisema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na waamuzi kumi na mbili ambao watachezesha mashindano hayo tayari wameshawasili jijini hapa tokea mwishoni mwa wiki.
Jaffary alisema mashindano hayo yataanza Octoba 29 na kufikia tamati Novemba 5 mwaka huu na kushirikisha  mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo mpaka juzi mikoa kumi na sita ilikwisha kuthibitisha kushiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti huyo aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar ,Arusha,Moshi,Iringa, Mbeya,Mara, Lindi,Shinyanga,Tabora,Dodoma  na Tanga ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo ambapo alisema timu nyengine huenda zitathibitisha katika shirikisho la mipira wa kikapu Taifa ikiwemo Zanzibar ,Unguja na Pemba.
Alisema mkoa  wa Kigoma walijitoa dakika za mwishoni kushiriki mashindano hayo ambayo msimu huu idadi ya washiriki imeongezeka kutokana na kuongezwa kwa idadi ya mikoa.
Mashindano hayo wa mara ya kwanza yalifanyika jijini Tanga 1989 na mara ya mwisho ili kuwa ni 2005 msimu huu shamra shamra zimeonekana kuwa ni muda kubwa kutokana na kuwa maandalizi ya maandalizi yanayofanywa na mikoa shiriki huku viwanja ambazo zitatumika mashindano zimefanyiwa ukarabati wa hali ya juu.
Mkoa wa Tanga unatarajiwa kuwa na wageni watapao 450 ikiwemo wachezaji na viongozi wa timu ambazo zitashiriki michuano hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo.
Aliongeza kuwa timu  zilianza  kuwasili jijini Tanga tokea Jumamosi na Jumapili ambapo kesho ndio ufunguzi rasmi wa mashindano hayo.

Sunday, October 28, 2012

mama wa mtoto aliye kojolea kitabu takatibu cha Qurani aomba razi kwa waisilamu


Mama wa kijana aliyekojolea kitabu kitukufu cha Quran  na kusababisha tafrani kubwa hapa nchini  hatimaye amejitikeza na kuomba radhi i kwa kitendo hicho na kusema  hakikupaswa kufanywa na jamii yoyote ulimwenguni.

Katika mahojiano maalumu aliyofanya na gazeti moja siku ya jumamosi bi Teresia Josephat  amesema hakuwa kutegemea kama kitendo hicho kingelifanywa na mwanae Emmanuel Josephat (14
kwa kuwa hakumkuza katika malezi aina hiyo

Wiki mbili zilizopita ,katika mabishano ya rika kati ya kijana huyo na wenzake  yalimfanya kijana huyo kukidhihaki kitabu kiutufu cha kuruani  kwa marai kwamba angelifanywa hivyo angeweza kugeuka  mnyama

Kitendo ambacho kilisababisha mlolongo ghasia  kati ya vijana wa kiislamu na polisi na kukupelekea kuharibiwa kwa mali pamoja na uchomaji wa makanisa katika eneo la Mbagala jijini dar es salaam

Powered by Blogger.