Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Tuesday, November 27, 2012

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI



MSANII WA VICHEKESHO NA MUZKI SHARO

 

MILIONEA  AMEFARIKI LEO HUKO MUHEZA

 

TANGA KWA AJALI YA GARI AMBAPO NDUGU


 YAKE WA KARIBU SNURA MUSHI 


AMETHIBITISHA  TUKIO HILO  KWA NJIA YA 


SIMU .....

 

Naye Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Afande Constatine Masawe, amethibitisha  kutokea kwa  kifo cha  wa Sharobaro, kufuatia  ajali ya gari  katika kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga  ambako ndio nyumbani kwao.......

 

MPAKA SASA MWILI UPO  HOSPITALI TEULE   YA MUHEZA ,TANGA


kikwatojr.blogspot.com imepokea habari hizi kwa mstuko na masikitiko makubwa kwani nyota ya Sharo Milionea ndiyo ilikuwa inaanza kung'ara katika anga za muziki pamoja na matangazo ya biashara, akiwa kayapumulia pumzi mpya wa ubunifu na weledi katika kupeleka ujumbe kwa watazamaji ambao wakubwa na wadogo walimpenda.

Tunaamini katika tasini ya filam na vichekesho kutakuwa na pengo kubwa sana kwani alikuwa ni mchekeshaji marufu sana na hata katika tasnia ya bongo freva pia kutakuwa na aliweza kufanya kazi kubwa na nzuri na wasanii wa hapa nchini pamoja na wasanii wa nnje na nyimbo yake ya mwisho inafahamika kama kizunguzungu akiwa amemshirikisha msanii alikiba na inafanya vizuri kwa sasa .

   Wote kwa pamoja na blog hii ina wapapole mashabiki na wapenzi wote wa Sharo milionea Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi amen.

Thursday, November 22, 2012

IMEELEZWA YAKUWA LAPTOP KUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME NA NA KUHARIBU MBEGU ZA UZAZI

Imedhibitiswa kitalamu kwamba joto linalo tolewa na lap top inapotumika ikiwa mapajani hupelekea kuhalibika kwa mbegu za kiume na kuwafanya wanaume kushindwa kupata watoto kwa wapenzi wao pindi tuu wanapo hitaji kufanya hivyo na kupelekea kutafuta machawi ni nani katika familia.

Scott Reed alifikiria kwenda na mkewe hospitali kujaribu njia ya kupandikiza mimba baada ya kuhangaika muda mrefu kujaribu kupata mtoto bila mafanikio.

Kitu ambacho Scott hakuweza kukifikiria ni pale alipoambiwa na madaktari kuwa laptop yake anayoitumia mara kwa mara akiwa ameiweka mapajani ndio chanzo cha tatizo lake la kutopata mtoto.

Madaktari walimuambia kuwa joto linalotokana na laptop yake inapotumika ikiwa mapajani husababisha kuharibika kwa mbegu za kiume na hivyo kumfanya ashindwe kupata mtoto.

Scott mwenye umri wa miaka 30 aliamua kuanza kuitumia laptop yake akiwa ameiweka kwenye meza na matunda yake yalijionyesha baada ya miezi mitatu ambapo mkewe Laura ambaye naye ana umri wa miaka 30 alipopata ujauzito.

Hivi sasa ikiwa ni miezi 10 baada ya kuzaliwa kwa mtoto wao wa kike Taryn, Scott na mkewe ambao wanaishi kwenye mji wa Clanfield, Hants, bado hawaamini jibu la tatizo lao kuwa lilikuwa ni laptop.

"Sikuwahi kusikia kuhusiana na laptop kuharibu mbegu za kiume, nilishtuka sana", alisema Laura.

"Scott alikuwa akiitumia laptop yake kila siku jioni kwa masaa kadhaa akiwa ameiweka mapajani huku tukiangalia TV, hatukuwahi kufikiria kuwa ilikuwa na madhara na ilikuwa ikiharibu mbegu zake za kiume", aliongeza Laura.

Naye daktari bingwa wa masuala ya uzazi Sue Kenworthy alithibitisha madhara ya laptop kwa kusema kuwa wanaume inabidi watumie laptop wakiwa wameiweka kwenye meza badala ya kuiweka mapajani.

UAMSHO SASA WAPUNGUZIWA UNAFUU WA KUWEZA KUPATA ZAMANA


Kutokana kwa kushindwa kuhimili ma shariti ya zamana yaliyo tolewa awali na mahakama ya Mwana kwereke iliyopo visiwani Zanzibara Mahakama hiyo imependekeza kupunguza kwa viongozi hao wa jumuiya ya uamsho zanzibar

Hiyo imetokana na watumishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kushindwa kujitokeza kuwadhamini washitakiwa hao

Awali washitakiwa hao walitakiwa kuwasilisha wadhamini wawili wanaofanya kazi serikalini ikiwa na kusaini hati ya milioni moja kila mmoja sharti ambalo limeonekana kuwa kikwazo kwao

Hivyo Hakimu Msaraka Ame Pinja alikubali kupunguza masharti hayo kutokan na wakili wa upande wa utetezi, Salum Tawfq kuomba kupunguzwa na kuangaliwa upya masharti ya dhamana kwa wateja wake

Hivyo walitakiwa kila mshitakiwa kusaini dhamana ya fedha taslimu Sh. 500,000 za kitanzania na awe na wadhamini wawili na kupunguza mmoja ambao pia ni lazima wawe watumishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mh Sugu, Fid Q ndani ya BONGO MOVIE!


Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya  mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameshiriki katika filamu inayoitwa Bifu akiwa pamoja na mwanahiphop mwenzake Fid Q.

Filamu  hiyo inaelezea maisha ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiongelea maisha yao pamoja na changamoto wanazokutana nazo kila siku.

Ukiachilia mbali wasanii kama  Fid Q na Sugu yupo pia mwanadada muigizaji wa siku nyingi Christina John maarufu kwa jina la Sintah.

Thursday, November 15, 2012

green-world-health kuwatibu wakazi wa jiji la tanga matatizo mbali mbali

watalamu wa kutoa huduma ya tiba mbadala kwa kutumia virutubisho  marufu kama dawa liche huduma hizo ambazo hupatikana jijini Arusha na Dodoma amapo kwa sasa wako jijini tanga kwa jijini Arusha  wanafahamika kama ARUSHA THERAPEUTIC CLINIC ambapo wapo SAFARI HOTEL BUILDING  gorofa ya 2 chumba namba 203 kwa Dododma wanafahamika kwama THE GREEN HOUSE OF HEALTH wanapatikana Area C karibu na SIMBA HOTEL .
   kwa mawasilianao waweza kuwasiliana nao watalamu hao wa afya uweze kupatiwa tiba lishe kitaalamu kwa simu no 0717 2226566 ama 0767 226566

picha ni aina ya dawa mbali mbali ambazo hutumika kutibu maradhi mbali mbali yatokanayo na lishe ambayotunazo kula na dawa hizo hazina kemikali kwani hutokana na matunda na mboga mbago na michanaganyiko mbali mbali.
wakiwa ziarani jijini tanga wakiwapatia huduma ya tiba wakazi wa jiji la Eanga picha ni moja kati ya wateja ambao blog ya kikwatojr.blogspot.com iliwashuhudia wakipatia tiba kwa kutumia vifaa vya kisayansi zaidi.
picha ni mashine inayotumika kufanyia uchunguzi wa magonjwa mbali mbali yaliyopo katika mwili wa mwanadam inayo julikana kwa jina la kitalam QUANTUM

Pichani ni ndoo ya maji meupe kabisa yakiwa na kifaa kinacho tumika kitolea sumu mwilini kabla ya mgonjwa haja dumbukiza miguu humo ndani.
moja kati ya wateja waliohudhuria katika matibabu hayo akiwa ametumbukiza miguu ndani ya ndoo ya majii kwajili ya kutolewa sumu mwilini kwa kutumia mashine malum.
 picha hii inaonesha jinsi maji yalivyoo badilika kutoka kwenye weupe hadikuwa na rangi hiyoo unayo  jionesha hapo na hiyo ni sumu zilizopo mwilini ambao hutokana ma mavyakula tunayokula na matatizo mengine ya kibina damu.
 KWA MAWASILIANA ZAIDI WAWEZA WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0717 2226566 ama 0767 226566

Tuesday, November 13, 2012

GREEN WORLD HEALTH

Watalamu wa Tiba mbadala kwa matatizo ya kiafya yanayo sababishwa na  maisha ya kila siku pamoja  na lishe tunayo sasa   kuwasili jijini tanga kwajili ya kukupatia ufumbuzi wa matatizo yako yanayo kusumbua .

BLOG YA KIKWATOJR.BLOGSPOT.COM ITAENDELEA KUKUPA TARIFA ZAIDI JUU YA WAPI KWA KUWAPATA NA KAZI ZAO WANZO ZIFANYA KWA SASA WAKIWA JIJINI TANGA

Sunday, November 11, 2012

KUTAMBIANA KWA WASHABIKI WA COAST UNION NA YANGA

Yanga leo hawatoki...! Shabiki maarufu wa klabu ya Coastal Union, Ibrahim 'Ibra' akionekana katika Barabara ya 8 jijini Tanga mchana huu baada ya kukamilisha michoro yake mwilini akiwachiomba mkwara Yanga kabla ya kwenda uwanjani kuishangilia timu yake itakayocheza jioni ya leo dhidi ya Yanga kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Novemba 11, 2012. 

Mashabiki wa Yanga wakiandamana na vigoma na vuvuzela katikam maeneo ya stendi kuu ya mabasi jijini Tanga leo ikiwa ni mikwara yao kabla ya kuwavaa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jioni.

Mechi kali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayokuwa ya kumalizia mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kati ya wenyeji Coastal Union na Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo jioni imeandika rekodi baad ya tiketi zake kuuzwa kwa bei 'mbaya' kuliko mechi zote za msimu huu ikiwamo ya mabingwa watetezi, Simba dhidi ya wenyeji hao (Coastal).

Mauzo ya tiketi hizo leo ni Sh. 5,000 kwa kiingilio cha chini (ambazo kufikia saa 9:00 watu walikuwa wakizilangua kwa Sh. 7,000), Sh. 10,000 na Sh. 15,000 kwa kiingilio cha juu wakati katika mechi nyingine zenye mvuto zaidi ikiwamo ya Simba dhidi ya Coastal, viingilio vilikuwa Sh. 4,000, Sh. 7,000 na Sh. 10,000.

Licha ya viingilio hivyo vikubwa, mashabiki walionekana wakichangamkia tiketi hizo kwa wingi, wengine wakitokea jijini Dar es Salaam na baadhi katika maeneo ya jirani ya jiji la Tanga kama Kabuku, Mwakidila, Duga Maforoni, Pangani, Muheza, Korogwe na kwingineko


Powered by Blogger.