Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Thursday, August 8, 2013

MBUNGE wa kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ameibua madudu mapya katika sekta ya elimu

MBUNGE wa kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ameibua madudu mapya katika sekta ya elimu, ambao umebaini kwamba kwenye mitihani ya majaribio ya darasa la saba, baadhi ya maswali ya kuchagua, hayakuwa na majibu.

Mitihani hiyo ya majaribio ya programu maalum ya matokeo makubwa sasa, kwa mujibu wa Mbatia ilifanywa na wanafunzi wa darasa la saba hivi karibuni katika masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza katika wilaya 40 nchini.

Katika uozo huo ambao ameutaja kama kuwakatisha tamaa wanafunzi katika somo la Hisabati, Mbatia alisema maswali sita yalibainishwa na wataalamu wa Hesabu kuwa hayana majibu huku swali moja likiwashinda maprofesa waliofanya mtihani huo.

Alisema katika swali moja, namba 33 walimu wa hisabati katika shule kubwa za msingi walishindwa kulifanya na baadaye kubainika kuwa ni swali la mwanafunzi anayechukua fani ya uhandisi katika vyuo vya elimu ya juu.

Mabatia alisema katika mitihani hiyo, kunamakosa mbalimbali ya lugha pamoja na usahihi wa masuala mbalimbali, ikiwemo programu hiyo kuainishwa kama matokeo makubwa sasa huku jina la wizara likiandikwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Alisema katika mtihani huo wa hisabati,ambao wanafunzi wa darasa la saba walitakiwa kufanya kwa saa mbili, mtaalamu wa aligebra aliufanya kwa saa 2:10 na profesa saa 2:03 huku yeye akifanya kwa saa 2:19.

“Matokeo haya ni kuwakatisha tamaa na kuwaua wanafunzi kabla ya kufanya mitihani, ni lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuokoa mapigo haya ya moyo wa Taifa ambayo yakizimika, Taifa linakufa,” alisema.

Mbatia alitoa mapendekezo yake ili kuokoa janga hili la elimu ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Tume ya Kudumu ya Elimu, itakayoshughulikia kuhakikisha ubora wa elimu nchini. Tume hiyo kwa mujibu wa Mbatia, inatakiwa kuwa na mamlaka ya kuhakiki utendaji wa taasisi mbalimbali za elimu, ambazo hadi sasa zimeonekana kutotimiza vyema wajibu wake.

“Ninaamini kwamba,tume hiyo itakapoundwa itasaidia kubainisha wazi nini falsafa na malengo hasa ya utoaji wa elimu nchini, kulingana na wakati tulionao, jambo ambalo halitakuwa geni kwani katika uongozi wa awamu ya kwanza, kulitungwa falsafa na miongozo mbalimbali,”alisema

Alisema kwa mamlaka aliyonayo Rais na na kwa mujibu wa katiba na kwa kadri anavyoona inafaa, anaweza kuunda tume na kuipatia majukumu ya utendaji stahiki, ikiwemo kutoa idhini ya matumizi ya mitaala mingine.

Pia alipendekeza tume hiyo ihariri na kupitia vitabu vya kiada kwa shule nchini na kufanya utafiti za kisayansi kuhusu masuala mbalimbali ya elimu kwa lengo la kuinua ubora wa elimu.

Akizungumza na Blog hii , Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bunyanzu Ntambi alikiri kuwa jinala wizara limekosewa katika mitihani hiyo. Alipoulizwa kuhusu uozo uliopo katika mitihani hiyo ya majaribio, alisema atafuatilia na atatoa taarifa kwa gazeti hili baadaye.

Wednesday, August 7, 2013

WAZAZI WAKATAZA WALIMU WASIWAFUNDISHE WATOTO WAO JINSI YA KUTUMIA CONDOM

Imeelezwa kuwa Baadhi ya wazazi na walezi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamekuwa wakiwazuia walimu kutoa elimu ya njia ya kujikinga na ukimwi kwa watoto wao wa sule za msingi ikiwemo matumizi sahihi ya condom. 

Hayo yamebainika leo katika semina iliyoandaliwa na shirika la UNESCO iliyojumisha wakuu wa shule za msingi na sekondari pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika katika ukumbi wa Golden Valley Mjini Kahama.

Akichangia hoja katika semina hiyo Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Korogwe Bi Ashura Rugakingira amesema kuwa wamekutana na tatizo hilo toka kwa baadhi wazazi hao licha ya kuwa somo hilo lipo katika mtaala wa Serikali.

Rugakingira amesema kuwa changamoto hiyo inawafanya walimu wengi kukata tamaa ya kutoa elimu hiyo ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa wanafunzi hao.

Awali akifungua semina hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Bi Isabela Chilumba amewataka walimu hao kuvunja ukimya na kuwa wawazi kuzungumza na wanafunzi wao kuhusu Maambukizi ya virusi vya ukimwi na UKIMWI.

Sambamba na hayo Chilumba ametoa angalizo kwa wananchi kutodanganyika na takwimu za maandishi zinazotolewa na kwamba kila mtu awe mstari wa mbele kupima afya yake mwenyewe.

Naye Msimamizi wa mradi huo wa Elimu ya Afya ya UKIMWI, uzazi na maadili kwa vijana kutoka UNESCO Mathius Herman amesema lengo la mradi huo ni kujenga mahusiano rasmi kati ya Mashirika yasiyo ya serikali na shule.

Tuesday, July 16, 2013

UTAFITI: WANAUME HUVUTIWA ZAIDI NA SURA WANAPOTAFUTA MKE LAKINI HUVUTIWA NA UMBO WANAPOTAFUTA MWANAMKE WA "KUCHEZEA"




hili ni jambo la kuchunguza sana na lakulifatilia kwa umakini zaidi ili usije ukafanya kama hivi na wewee

  • Mabinti: Siri imeshafichuka na inavyoonekana wanasayansi tayari wameshafumbua lile fumbo tata la nani mwoaji na nani mbabaishaji tu mtaka uroda.
  • Siku nyingine mpenziyo mpya akikuambia kwamba sababu yake kuu ya kukupenda ni miguu yako, macho, kiuno, matiti, umbo namba nane au sababu zingine za kiumbo, kuna uwezekano mkubwa kwamba huyo njemba si mwoaji bali ni mtafuta uroda tu.
  • Utafiti mpya uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Texas, Austin unaonyesha kwamba wanaume hutumia vigezo tofauti wanapotafuta mwenzi.
  • Kama lengo ni kutafuta mwenzi wa kudumu (mf. mke) basi wanaume wengi hupendelea wanawake wenye sura nzuri lakini kama lengo ni uhusiano wa muda mfupi tu (mf. kutimiza tamaa za ngono za muda mfupi) basi wanaume wengi hutafuta wanawake wenye maumbo mazuri wayatamaniyo
     
    Watafiti hawa wamegundua kwamba, japo umbo ni muhimu kidogo katika mahusiano ya muda mrefu, uso ni muhimu zaidi kwa sababu ndicho kiashiria kizuri cha umri na “rutuba” ya mwanamke.

Monday, July 15, 2013

BINTI ABAKWA MPAKA KUFA MBELE YA NYUMBA YA IBADA

Binti mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Mariam umemkuta umauti baada ya kubakwa mpaka kufa,vijana hao waliokosa utu na kushindwa kumuogopa Mungu walifanya kitendo hicho mbele ya eneo la kanisa huko Nachingwea Lindi.Marehemu akitoka Nachingwea Resort  katika muziki siku ya ijumaa.Inasadikika kuwa marehemu alikuwa amelewa na watu walio mbaka alitoka nao kwenye muziki.


Emungu tunusuru na hili kadhia mana tunakoelekea kwa sasa siko jamani tubadilike

CHAMA CHA TIBA ZA ASILI(ATME) WABARIKI MATUMIZI YA MAFUTA YA UBUYU, WASEMA HAYANA MADHARA YOYOTE KWA AFYA YA BINADAMU...!!

Sasa ni kati ya Chama cha Tiba Asili (ATME) na  TDFA.  ATME kinadai hayana madhara wagonjwa wake wameyatumia kwa zaidi ya miaka 20.
Dar es Salaam. Mratibu wa Chama cha Watabibu wa Dawa za Asili Tanzania (ATME), Boniventure Mwalongo amesema taarifa zilizotolewa hivi karibuni na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TDFA) kuhusu matumizi ya mafuta ya ubuyu zinaweza kuleta madhara kwa jamii kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiyatumia.
Akitolea mfano watumiaji wakubwa  wa mafuta hayo, Mwalongo alisema, wenye magonjwa kama ya moyo na wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wamekuwa wakiyatumia mafuta hayo kwa muda mrefu na kudai yamewasaidia.
Mwalongo ameyasema hayo jana baada ya hivi karibuni kuibuka utata kuhusu ubora na usalama wa mafuta hayo na kudai kuwa wao kama ATME walianza kuyatumia kama dawa kwa wateja wao siku nyingi na hawajawahi kupata malalamiko yoyote na kuwahakikishia watumiaji kuwa hayana madhara.
 
 
 
 
 Yametumika kwa zaidi ya miaka 20 na sisi tunazo kumbukumbu za wagonjwa tuliowapa mafuta hayo kama dawa na hatujawahi kupata ripoti yoyote ya madhara kwa wale waliotumia,” alisema Mwalongo.   TFDA ilitoa taarifa kwamba mafuta hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu kwa sababu yana kiwango kikubwa cha tindikali ya mafuta aina ya cyclopropenoic fatty acids.

  Katika taarifa ya TFDA iliyotolewa juma lililopita ilisema athari zinazoweza kutokea kutokana na matumizi ya mafuta hayo ni pamoja na kuathiri vimeng’enyo vinavyosaidia katika uchakataji wa tindikali za mafuta mwilini.
  Pia ilisema ili yaweze kukidhi vigezo vya ubora na usalama ni lazima yafanyiwe usafishaji wakati wa usindikaji na kwamba kwa sasa nchini hakuna aina ya usindikaji unaofanyika wenye uwezo wa kuondoa tindikali hiyo ya cyclopropenoic fatty acids katika mafuta ya mbegu za ubuyu.
 Hata hivyo Mwalongo alikemea usambazaji holela wa mafuta hayo hasa baada ya kubainika kuwa yanatibu maradhi mbalimbali ambapo baadhi ya wajasiriamali wamekuwa wakiyasambaza wakati siyo wataalamu wa tiba asili.
  Mratibu huyo alizishauri mamlaka zinazohusika na suala zima la afya ya binadamu nchini kutoa majibu yatakayosaidia kuondoa mgawanyiko uliopo sasa kutokana na mafuta hayo badala ya kutoa taarifa za kutisha.
   Hata hivyo alipoulizwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Tiba Asili kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Paul Mhame, alisema hawana taarifa zozote kama kuna tafiti zimefanyika kuhusiana na matumizi ya mafuta hayo.

.MACHANGUDOA DAR WASEMA "MCHANA TUNAFUNGA, USIKU TUNAJIUZA TUPATE HELA YA FUTARI NA DAKU"....

OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na mapaparazi wa Global Publishers inazidi kufichua ‘madudu’ kwenye jamii, safari hii imekutana na machangu ambao wamecharuka kuendeleza biashara hiyo kwa kisingizio cha kutafuta fedha za kununulia futari.


‘Askari’ wa OFM, wiki iliyopita alifanya uchunguzi katika viunga mbalimbali maarufu kwa biashara hiyo na kukuta machangudoa wakifanya biashara yao kama inavyokuwa katika miezi ya kawaida.
Maeneo ambayo yalionekana kushamiri zaidi kwa biashara hiyo ni Barabara ya Mwananyamala Hospitali, American Chipsi, Makaburi ya Kinondoni, Viwanja vya Leaders Club, Taasisi ya Moyo, Jolly Club (Masaki), Hospitali ya Agha-Khan, New Maisha Club (Masaki) na Coco Beach.

Saturday, February 23, 2013

matokeo kidato cha nne wawili wajiua, wawili wanusurika

KUFUATIA kupata matokeo mabaya ya matokeo yao ya kidato cha nne yaliyotangazwa wiki iliyopita jumla ya wahitimu wawili tayari wameshapoteza maisha kwa kujinyonga huku wawili wakiwa wameokolewa wakiwa katika harakati za kujiua 

Kati ya waliojinyonga ni Barnaba Venant [18] mkazi wa Mbagala ambaye alihitimu katika shule ya Sekondari ya Debrabant Mbagala ya jijini Dar es Salaam Akielezea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiyondo, alisema tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa 4 asubuhi huko maeneo ya Nzasa, Mbagala

Amefafanua kuwa, marehemu huyo alichukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na matokeo yake ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalibainishwa alipata daraja la nne point 27 kinyume na matarajio yake

Amesema kijana huyo alijinyonga kwa kutumia kamba ya manila, aliyokuwa ameitundika kwenye dari ndani ya stoo ya nyumba yao. Katika tukio lingine la aina hiyo, Michael Fidelis[19] aliyehitimu Shule ya Sekondari ya Kanyenye mjini Tabora

Imedaiwa kuwa, mhitimu huyo alipogundua amepata daraja sifuri aliporudi nyumbani alichukua maamuzi ya kujinyonga hadi kufa akiwa chumbani kwake kwa kutumia kamba ya manila.

Na kuacha ujumbe uliosomeka “Mama usitafute mchawi, uamuzi niliouchukua ni sababu ya matokeo yangu mabaya, nakutakia maisha mema, nisamehe sana mama.”

Kufuatia matokeo hayo mabaya yaliyoleta historia vijana wengine wawili mmoja mkazi wa Kimara Temboni jijini Dar es salaam amenusurika kutoa uhai wake kwa kutoridhishwa na matokeo hayo

Mwingine aliyefahamika wka jina la Hoseph Hoseah [18] mkazi wa mkoani Pwani alikimbizwa zahanati akwia aktika jaribio la kutoa uhai wake baada ya matokeo yake kuonyesha amepata daraja la nne jambo ambalo lilimfanya asiwe na raha tokea apokee matokeo hayo

Imedaiwa na mmoja wa ndugu wa kijana huyo kuwa ndugu yao huyo alikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi watano ambao shule ilikuwa ikiwatarajia wataleta sifa kwa kuleta daraja la kwanza shuleni hapo

Matokeo yaliyotangazwa mwanzoni mwa wiki hii na Waziri wa Elimu yanaendelea kuleta migogoro kwa wadau huku waziri huyo akitakiwa kujiuzuru
Powered by Blogger.