MKUU
wa mkoa wa Tanga lutein mstaafu Chiku Gallawa amewataka watu waliohamia
wilayani Kilindi na Handeni mkoani Tanga kuondoka katika wilaya hizo,
ili kupisha walengwa ambao ni wazawa wa wilaya hizo, nakwamba amefikia
uwamuzi huo kutokana na wahamiaji hao kuhodhi aridhi kinyume na taratibu
za kisharia.
Uamuzi
huo ameutoa katika kikao cha kamati ya ushauri mkoa wa Tanga RCC
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi ya mkuu wa mkoa
Aidha
mkuu huyo wa mkoa lutein Gallawa amesema kwamba Kilindi na Handeni sio
shamba la wavamizi hivyo ni vema wakazi hao ambao wamehamia kinyume na
utaratibu wa kisharia kuondoka katika maeneo hayo haraka iwezekanavyo
kabla ya kufika mwezi Januari mwakani ili kuepusha vurugu na migogoro ya aridhi siokuwa na tija mkoani hapa.
Hata
hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Tanga amewataka wakurungenzi wa halmashauri
zote mkoani hapa kusimamia majukumu yao ipasavyo ili kukomesha hali hiyo
kwa kuwatambuwa wazawa halali katika halmashauri zao.
Na
katika hatua nhyingine amewataka wakurungenzi hao watumie wanasheria
wao katika Halmashauri zao ili kutambua sharia za uchimbaji wa Madini
kuliko kuchimba madini kiholela bila kuwa na utaalamu jambo ambalo mara
nyingi limekuwa likileta athari kubwa kwa wananchi bila kupata faida
yeyote katika maeneo husika.
Kufuatia
hali hiyo lutein Gallawa wamewashauri wakurungenzi na wakuu wa wilaya
kuwa na idadi maalumu ya wachimba madini ili kuondoa fujo kwa wananchi
ikiwemo kuwapa vibali maalum pamoja na risiti.