Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Sunday, October 28, 2012

mama wa mtoto aliye kojolea kitabu takatibu cha Qurani aomba razi kwa waisilamu


Mama wa kijana aliyekojolea kitabu kitukufu cha Quran  na kusababisha tafrani kubwa hapa nchini  hatimaye amejitikeza na kuomba radhi i kwa kitendo hicho na kusema  hakikupaswa kufanywa na jamii yoyote ulimwenguni.

Katika mahojiano maalumu aliyofanya na gazeti moja siku ya jumamosi bi Teresia Josephat  amesema hakuwa kutegemea kama kitendo hicho kingelifanywa na mwanae Emmanuel Josephat (14
kwa kuwa hakumkuza katika malezi aina hiyo

Wiki mbili zilizopita ,katika mabishano ya rika kati ya kijana huyo na wenzake  yalimfanya kijana huyo kukidhihaki kitabu kiutufu cha kuruani  kwa marai kwamba angelifanywa hivyo angeweza kugeuka  mnyama

Kitendo ambacho kilisababisha mlolongo ghasia  kati ya vijana wa kiislamu na polisi na kukupelekea kuharibiwa kwa mali pamoja na uchomaji wa makanisa katika eneo la Mbagala jijini dar es salaam

Saturday, October 27, 2012

KAULI YA BWANA MISOSI KWAWOTE WANAOMPA USHIRIKIANO WAKATI HUU WAMSIBA WA KAKA YAKE MAREMU Emanuel Gabriel Rushahu!

Mambo vipi ndugu zangu asanteni kwa kunifariji' najua wapo wengi wangependa kuhudhuria mazishi ila kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao watashindwa kuhudhuria mazishi leo siku ya ijumaa tar 26 oct, ila kwa rambi rambi zao kwa marehemu kaka yangu Emanuel Gabriel Rushahu wanaweza kutumia na hii M pesa 0763558855 nitaiwakilisha kwa familia katika daftari la michango na mwili tutauaga hapahapa nyumbani kinyerezi mida ya saa sita mchana pia misa ya mazishi ni saa nane mchana katika kanisa katoliki segerea na tutampumzisha katika makaburi ya hapohapo segerea..

SIRI YANGU YA KUTUMIA LAFUDHI YA KIMASAI



 HATIMAYE msaani maarufu wa vichekesho nchini, Gilliady Severine a.k.a Masai Nyotambofu, ametoa siri yake ya kutumia lafudhi ya jamii ya Kimasai katika kazi yake ya sanaa ya maigizo na vichekesho.
Akizungumza na blog hii jijini hapa juzi, Nyotambofu alisema kuwa, yeye aliamua kutumia lafudhi ya Kimasai baada ya kubaini kuwa ni ngumu na hata waliyokuwa wakijaribu kuitumia katika sanaa mbalimbali, hawakuweza kukidhi mahitaji ya lafudhi ya lugha hiyo. Msanii huyo amekuwa akisikika katika matangazo mbalimbali yanayorushwa na vituo vya radio hapa nchini, hasa ya uhmasishaji wa kuacha pombe, yaani ‘ulevi noma’ lilitolewa na Idara ya Ustawi wa Jamii wakishirikiana na Jeshi la Polisi. “Ndugu mwandishi, niliamua kutumia lafudhi ya Kimasai, kwani nilishafanya utafiti na kubani kuwa, lugha hii ni ngumu kuiga, pia niliangalia wasanii ambao walikwisha kujaribu kuitumikia lafudhi ya Kimasai, nikaona hawajakidhi kabisa ndipo nikaamuua kuitumia na mpaka sasa najivunia nimeweza,” alisema Masai Nyotambofu. “Hata hivyo, ilibidi niongeza juhudi na kujituma katika kuitumia lafudhi hii baada ya kupewa zawadi ya fimbo na mgolole na wazee katika Wilaya ya Ngorongoro, baada ya kuona nimeweza kuimudu lafudhi yao tofauti na wasanii waliokwisha kuwahi kuitumia katika maigizo na muziki,” alisema na kuongeza: “Kilichonitia moyo na kuongeza juhudi katika kutumia lafudhi hii, mwaka 2010 nilikwenda Ngorongoro kufanya onyesho na mwanamuziki Banana Zoro, ilikuwa sikukuu ya wafanyakazi, ndipo wazee wa Kimasai wakaridhika na kazi yangu wakanizawadia huo mgolole na fimbo, mpaka sasa ndivyo ninavyovitumia,” alisema Masai Nyotambofu. Msanii huyo maarufu, ambaye ni Muha kutoka Kigoma, yupo jijini Mbeya kwa ajili ya kurekodi vipindi vya ‘Vituko Show’ vinavyorushwa na kituo cha televesheni ya Channel Ten.

Tuesday, October 23, 2012

shirika la mfuko wa taifa wa bima ya afya lashauriwa kuongeza ufanisi katika kuboresha huduma zake

picha ni wakina mama washiriki wilayani Muheza wakiwa wanafatilia mafunzo kwa umakini
(hao pia ni mingoni  mwa  washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya unyanyasaji yanayoendeshwa kwa ufadhili wa Shirika la INUKA na SWAT )

 SHIRIKA  la Mfuko wa taifa  wa Bima ya afya limeshauriwa kuongeza ufanisi kwa  kuboresha huduma zake zaidi ili kuondoa usumbufu na malalamiko kwa wanachama wake.
Hayo yalielezwa na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya unyanyasaji yanayoendeshwa kwa ufadhili wa Shirika la INUKA na SWAT  na kufanyika  kwenye ukumbi wa kanisa la Elimu Pentacost la Masuguru Mjini Muheza.
Washiriki hao ambao wengi wao ni walimu, walilalamika kuwa huduma za bima ya afya bado hazijatengemaa vema na kwamba kuna haja kwa wahusika kujipanga na kuhakikisha kuwa wanachama wake wanapata wanachotarajia ipasavyo.
Walidai kuwa licha ya kukatwa fedha nyingi kila mwezi lakini  fedha wanazotozwa  haziendani na huduma zinazotolewa  jambo walilolieleza kuwa linawafanya wakate tama na kujutia michango yao.
Kwamujibu wa washiriki hao ni kwamba wanalazimika kutoa michango yao kila mwezi lakini hawapati huduma wanayotarajia na badala yake wanapokwenda  hospitali wanatakiwa kulipia dawa na vipimo vingine na hivyo kupata gharama kubwa.
Mambo mengine yaliyojitokeza kwenye mafunzo hayo ni pamoja na malalamiko zidi ya Taasisi ya  Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  Wilaya ya Muheza kudaiwa kutoa siri kwa kuwataja  kwa waharifu watu wanaojitoa kupeleka  taarifa za makosa hayo katika ofisi zao.
Aidha washiriki hao walilalamikia unyanyasaji katika jeshi la polisi.Mahakama pamoja na watendaji  mbalimbali katika maofisi ya serikali na binafsi na kwamba wamekuwa wakipata manyanyaso kwenye ajira kwa upendeleo wenye mazingira ya rushwa.
Awali mkufunzi wa mafunzo hayo Nestory Ngwega alitumia muda mwingi kueleza haki za msingi za binaadamu ambazo zisipofuatwa ndipo tendo la unyanyasaji hutokea na kwamba haki hizo zipo kwenye makundi mawili ambayo ni haki ya kikatiba na ile ya kibinaadamu ambayo haiondolewi na mtu yeyote Yule kwa nafasi yake ama uwezo wa kifedha.
Mengine yaliyojadiliwa katika mafunzo hayo ni unyanyasaji ndani ya familia na kwa wanandoa  pamoja na vyanzo vyake na jinsi ya kukabiliana navyo.




Monday, October 22, 2012

wakulima wadogo wadogo wa mkonge sasa kupatiwa mashine itakayo wasaidia

Hapa ni mashine hiyo mya kwajili ya wakulima wadogo wadogo itakayo wawezesha kulima na kutengeneza singa zao wenyewe pasipo kupeleka korona
picha ni jinsi mashine hiyo itakavyo kuwa ikizaliwa wakati ikiwa inajaribiwa kabla ya kutolewa maelekezo ya tamati na kufikishwa kwa wakulima
picha ni mkurugenzi mkuu wa bodi ya mkonge taifa akikagua singa zilizo toka katika mashine hiyo mya itakayo tumika na wajasiria mali wadogo wadogo wa kilimo hicho cha mkonge
mkurugenzi wa bodi ya mkonge taifa akiwa na kaimu mkurugenzi wa kituo cha utafiti kilimo MLINGANO wakiwa wanatazama kwa pamoja jinsi gani mashine hiyo inavyo zalisha singa hizo za mkonge .
     picha na mkurugenzi wa blog kikwatotojr  kwa habari mbali mbali na matukio tunaweza kuwasiliana kwa namba 0718991013 au 0754335020

Sunday, October 21, 2012

mfadhili wa ccm mkoa wa dodoma ndugu sheleli ajiunga na chadema .

Chadema jana ilifanya Mkutano wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Mpwapwa kamanda Baharia.

Mkutano huo ulikuwa na umati mkubwa sana watu. Shangwe, hoihoi na nderemo vililipuka pale mfadhili mkubwa wa CCM mkoani Dodoma ndugu Shelali alipoamua kujivua gamba na kujiunga na CHADEMA. Alipopewa nafasi ya kusema chochote kwa umati ule ndugu Shelali alisema amekuwa mfadhili wa CCM tangu mwaka 1983.

Katika kuthibitisha hilo alikuja na nakala za barua za kuombwa fedha na mzee Malechela pamoja na tuzo nyingi za heshima kutoka CCM. Mzee Shelali alisema ameamua mwenyewe kujiunga na CHADEMA kwani ndicho chama pekee kinachoonyesha nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania na kuwaomba wananchi wa Mpwapwa kujiunga na Chadema.

Katika mkutano huo ngugu Shelali alijitolea kuwanunulia kadi za CHADEMA wananchi wote watakaotaka kujiunga na CHADEMA wilayani mpwapwa. Baada ya mkutano huo wananchi na viongozi wa CHADEMA walielekea nyumbani kwa shelali kushusha bendera ya CCM na kupandisha ya CHADEMA ambapo mzee Shelali alijitolea kuipa CHADEMA ofisi.

Katika mkutano huo wananchi wa Mpwapwa walichanga zaidi ya sh. laki tano kwa ajili ya kusaidia kampeni. 

Kilichonifurahisha ni kitendo cha wananchi kuingia barabarani licha ya kuzuiwa na polisi waliojaribu kuzima maandamano yao.

Mkutano huo ulihutubiwa na Benson Kigaila, Diwani Ali Issa Biringi na Kamanda Nicholaus Ngowi

wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari arusha ajtc watembelea chuo cha walemavu usa riva

walimu wa chuo cha uandishi wa habri AJTC na basdhi ya viongozi wa chuo cha walemavu cha usa riva jijini arusha katika picha ya pamoja ya furaha huku aliye kaa chini mwenye shati jeupe ni moja wa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habri na utangazaji kwa levo ya diploma bwana Amani James
Presenter wa matukio yote, wa AJTC akipata machache toka kwa wanachuo cha ulemavu cha Usar-River Arusha AMBAE PIA NI KIONGIZI WA BURUDANI KATIKA KIKUNDI CHA WAKAGUZI CREW KILICHOPO KATIKA CHUO CHAO BWANA SAM.
Madam Neema Ezekiel akipiga picha na wanachuo cha ulemavu cha Usar-River Arusha
Powered by Blogger.