PALACE HOTEL
Vumbua Hazina chini ya kizibo
Monday, October 29, 2012
TFF YASAKA MILIONI 225 ZA KUIPELEKA MOROCCO SERENGETI BOYS
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inahitaji zaidi ya Sh Milioni 225 kwa ajili ya kampeni yake iliyobakia ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya TFF, Ilala, Dar es Salaam, Tenga alisema kwamba shirikisho lake kwa sasa halina fedha hizo, kwa sababu hiyo haina mdhamini, zaidi ya kutegemea misaada ya wadau.
Tenga alisema tayari Kamati ya Vijana ya TFF imekwishakutana kuweka mikakati ya kuiwezesha Serengti kushiriki vema kampeni hizo, ikiwemo kuunda Kamati ya kuisaidia timu hiyo.
Hata hivyo, Tenga hakuitaja Kamati iliyoundwa kwa sababu bado hawajazungumza na Wajumbe walioteuliwa.
Alisema kocha wa timu hiyo, Mdenmark Jacob Michelsen ameomba mechi za kujipima nguvu kabla ya kucheza na Kongo Brazaville kuwania tiketi ya Morocco na Kamati ya Vijana inahangaikia suala hilo kwa sasa.
Alisema tayari kuna mwaliko kutoka Botswana wa Serengeti kwenda kucheza, lakini kutokana na ukosefu wa fedha wanashindwa hadi sasa kutoa jibu.
Kikosi cha wachezaji 25 cha Serengeti Boys kipo kambini mjini Dar es Salaam tangu Oktoba 21, mwaka huu kujiandaa na mechi hiyo, ya kwanza ikichezwa nyumbani Novemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.
Tanzania imefuzu bila jasho hadi kufika hatua hiyo, baada ya wapinzani wake wa awali, Kenya na Misri kujitoa katika Raundi ya Kwanza na ya Pili.
Kama Tanzania itafuzu kushiriki Fainali hizo za mwakani, itapoza machungu ya mwaka 2005 walipofuzu kucheza Fainali za Vijana wa umri huo kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, lakini baadaye kwa sababu ya ‘kufoji’ umri wa Nurdin Bakari, ikaondolewa mashindanoni.
Zaidi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 1980 na CHAN 2009, katika soka ya wanaume, Tanzania haijashiriki fainali nyingine zozote za Afrika tangu iingie kwenye soka ya kimataifa.
mama chiku Gallawa kuwa mgeni rasmi taifa cup Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mama Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michuano ya Kombe la Taifa ya mpira wa Kikapu, Taifa Cup mwaka 2012 yanayotarajiwa kuanza kesho kwenye viwanja vya Mkwakwani na Harbours Club vilivyo jijini Tanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanga (TRBA), Hamisi Jaffary alisema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na waamuzi kumi na mbili ambao watachezesha mashindano hayo tayari wameshawasili jijini hapa tokea mwishoni mwa wiki.
Jaffary alisema mashindano hayo yataanza Octoba 29 na kufikia tamati Novemba 5 mwaka huu na kushirikisha mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo mpaka juzi mikoa kumi na sita ilikwisha kuthibitisha kushiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti huyo aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar ,Arusha,Moshi,Iringa, Mbeya,Mara, Lindi,Shinyanga,Tabora,Dodoma na Tanga ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo ambapo alisema timu nyengine huenda zitathibitisha katika shirikisho la mipira wa kikapu Taifa ikiwemo Zanzibar ,Unguja na Pemba.
Alisema mkoa wa Kigoma walijitoa dakika za mwishoni kushiriki mashindano hayo ambayo msimu huu idadi ya washiriki imeongezeka kutokana na kuongezwa kwa idadi ya mikoa.
Mashindano hayo wa mara ya kwanza yalifanyika jijini Tanga 1989 na mara ya mwisho ili kuwa ni 2005 msimu huu shamra shamra zimeonekana kuwa ni muda kubwa kutokana na kuwa maandalizi ya maandalizi yanayofanywa na mikoa shiriki huku viwanja ambazo zitatumika mashindano zimefanyiwa ukarabati wa hali ya juu.
Mkoa wa Tanga unatarajiwa kuwa na wageni watapao 450 ikiwemo wachezaji na viongozi wa timu ambazo zitashiriki michuano hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo.
Aliongeza kuwa timu zilianza kuwasili jijini Tanga tokea Jumamosi na Jumapili ambapo kesho ndio ufunguzi rasmi wa mashindano hayo.
Sunday, October 28, 2012
mama wa mtoto aliye kojolea kitabu takatibu cha Qurani aomba razi kwa waisilamu
Mama wa kijana aliyekojolea kitabu kitukufu cha Quran na kusababisha tafrani kubwa hapa nchini hatimaye amejitikeza na kuomba radhi i kwa kitendo hicho na kusema hakikupaswa kufanywa na jamii yoyote ulimwenguni.
Katika mahojiano maalumu aliyofanya na gazeti moja siku ya jumamosi bi Teresia Josephat amesema hakuwa kutegemea kama kitendo hicho kingelifanywa na mwanae Emmanuel Josephat (14
kwa kuwa hakumkuza katika malezi aina hiyo
Wiki mbili zilizopita ,katika mabishano ya rika kati ya kijana huyo na wenzake yalimfanya kijana huyo kukidhihaki kitabu kiutufu cha kuruani kwa marai kwamba angelifanywa hivyo angeweza kugeuka mnyama
Kitendo ambacho kilisababisha mlolongo ghasia kati ya vijana wa kiislamu na polisi na kukupelekea kuharibiwa kwa mali pamoja na uchomaji wa makanisa katika eneo la Mbagala jijini dar es salaam
Saturday, October 27, 2012
KAULI YA BWANA MISOSI KWAWOTE WANAOMPA USHIRIKIANO WAKATI HUU WAMSIBA WA KAKA YAKE MAREMU Emanuel Gabriel Rushahu!
Mambo
vipi ndugu zangu asanteni kwa kunifariji' najua wapo wengi wangependa
kuhudhuria mazishi ila kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao
watashindwa kuhudhuria mazishi leo siku ya ijumaa tar 26 oct, ila kwa rambi
rambi zao kwa marehemu kaka yangu Emanuel Gabriel Rushahu wanaweza
kutumia na hii M pesa 0763558855 nitaiwakilisha kwa familia katika daftari
la michango na mwili tutauaga hapahapa nyumbani kinyerezi mida ya saa
sita mchana pia misa ya mazishi ni saa nane mchana katika kanisa katoliki
segerea na tutampumzisha katika makaburi ya hapohapo segerea..
SIRI YANGU YA KUTUMIA LAFUDHI YA KIMASAI
HATIMAYE msaani maarufu wa vichekesho nchini, Gilliady Severine a.k.a Masai Nyotambofu, ametoa siri yake ya kutumia lafudhi ya jamii ya Kimasai katika kazi yake ya sanaa ya maigizo na vichekesho.
Akizungumza na blog hii jijini hapa juzi, Nyotambofu alisema kuwa, yeye aliamua kutumia lafudhi ya Kimasai baada ya kubaini kuwa ni ngumu na hata waliyokuwa wakijaribu kuitumia katika sanaa mbalimbali, hawakuweza kukidhi mahitaji ya lafudhi ya lugha hiyo. Msanii huyo amekuwa akisikika katika matangazo mbalimbali yanayorushwa na vituo vya radio hapa nchini, hasa ya uhmasishaji wa kuacha pombe, yaani ‘ulevi noma’ lilitolewa na Idara ya Ustawi wa Jamii wakishirikiana na Jeshi la Polisi. “Ndugu mwandishi, niliamua kutumia lafudhi ya Kimasai, kwani nilishafanya utafiti na kubani kuwa, lugha hii ni ngumu kuiga, pia niliangalia wasanii ambao walikwisha kujaribu kuitumikia lafudhi ya Kimasai, nikaona hawajakidhi kabisa ndipo nikaamuua kuitumia na mpaka sasa najivunia nimeweza,” alisema Masai Nyotambofu. “Hata hivyo, ilibidi niongeza juhudi na kujituma katika kuitumia lafudhi hii baada ya kupewa zawadi ya fimbo na mgolole na wazee katika Wilaya ya Ngorongoro, baada ya kuona nimeweza kuimudu lafudhi yao tofauti na wasanii waliokwisha kuwahi kuitumia katika maigizo na muziki,” alisema na kuongeza: “Kilichonitia moyo na kuongeza juhudi katika kutumia lafudhi hii, mwaka 2010 nilikwenda Ngorongoro kufanya onyesho na mwanamuziki Banana Zoro, ilikuwa sikukuu ya wafanyakazi, ndipo wazee wa Kimasai wakaridhika na kazi yangu wakanizawadia huo mgolole na fimbo, mpaka sasa ndivyo ninavyovitumia,” alisema Masai Nyotambofu. Msanii huyo maarufu, ambaye ni Muha kutoka Kigoma, yupo jijini Mbeya kwa ajili ya kurekodi vipindi vya ‘Vituko Show’ vinavyorushwa na kituo cha televesheni ya Channel Ten.
Tuesday, October 23, 2012
shirika la mfuko wa taifa wa bima ya afya lashauriwa kuongeza ufanisi katika kuboresha huduma zake
picha ni wakina mama washiriki wilayani Muheza wakiwa wanafatilia mafunzo kwa umakini
(hao pia ni mingoni mwa washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya unyanyasaji yanayoendeshwa kwa ufadhili wa Shirika la INUKA na SWAT )
SHIRIKA la Mfuko wa taifa wa Bima ya afya limeshauriwa kuongeza ufanisi kwa kuboresha huduma zake zaidi ili kuondoa usumbufu na malalamiko kwa wanachama wake.
(hao pia ni mingoni mwa washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya unyanyasaji yanayoendeshwa kwa ufadhili wa Shirika la INUKA na SWAT )
SHIRIKA la Mfuko wa taifa wa Bima ya afya limeshauriwa kuongeza ufanisi kwa kuboresha huduma zake zaidi ili kuondoa usumbufu na malalamiko kwa wanachama wake.
Hayo yalielezwa na washiriki
wa mafunzo ya siku tatu ya unyanyasaji yanayoendeshwa kwa ufadhili wa Shirika
la INUKA na SWAT na kufanyika kwenye ukumbi wa kanisa la Elimu
Pentacost la Masuguru Mjini Muheza.
Washiriki hao ambao wengi
wao ni walimu, walilalamika kuwa huduma za bima ya afya bado hazijatengemaa
vema na kwamba kuna haja kwa wahusika kujipanga na kuhakikisha kuwa wanachama
wake wanapata wanachotarajia ipasavyo.
Walidai kuwa licha ya
kukatwa fedha nyingi kila mwezi lakini fedha wanazotozwa haziendani
na huduma zinazotolewa jambo walilolieleza kuwa linawafanya wakate tama
na kujutia michango yao.
Kwamujibu wa washiriki hao
ni kwamba wanalazimika kutoa michango yao kila mwezi lakini hawapati huduma
wanayotarajia na badala yake wanapokwenda hospitali wanatakiwa kulipia
dawa na vipimo vingine na hivyo kupata gharama kubwa.
Mambo mengine yaliyojitokeza
kwenye mafunzo hayo ni pamoja na malalamiko zidi ya Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Muheza kudaiwa kutoa siri kwa
kuwataja kwa waharifu watu wanaojitoa kupeleka taarifa za makosa
hayo katika ofisi zao.
Aidha washiriki hao
walilalamikia unyanyasaji katika jeshi la polisi.Mahakama pamoja na
watendaji mbalimbali katika maofisi ya serikali na binafsi na kwamba
wamekuwa wakipata manyanyaso kwenye ajira kwa upendeleo wenye mazingira ya
rushwa.
Awali mkufunzi wa mafunzo
hayo Nestory Ngwega alitumia muda mwingi kueleza haki za msingi za binaadamu
ambazo zisipofuatwa ndipo tendo la unyanyasaji hutokea na kwamba haki hizo zipo
kwenye makundi mawili ambayo ni haki ya kikatiba na ile ya kibinaadamu ambayo
haiondolewi na mtu yeyote Yule kwa nafasi yake ama uwezo wa kifedha.
Mengine yaliyojadiliwa
katika mafunzo hayo ni unyanyasaji ndani ya familia na kwa wanandoa
pamoja na vyanzo vyake na jinsi ya kukabiliana navyo.
Monday, October 22, 2012
wakulima wadogo wadogo wa mkonge sasa kupatiwa mashine itakayo wasaidia
Hapa ni mashine hiyo mya kwajili ya wakulima wadogo wadogo itakayo wawezesha kulima na kutengeneza singa zao wenyewe pasipo kupeleka korona
picha ni jinsi mashine hiyo itakavyo kuwa ikizaliwa wakati ikiwa inajaribiwa kabla ya kutolewa maelekezo ya tamati na kufikishwa kwa wakulima
picha ni mkurugenzi mkuu wa bodi ya mkonge taifa akikagua singa zilizo toka katika mashine hiyo mya itakayo tumika na wajasiria mali wadogo wadogo wa kilimo hicho cha mkonge
mkurugenzi wa bodi ya mkonge taifa akiwa na kaimu mkurugenzi wa kituo cha utafiti kilimo MLINGANO wakiwa wanatazama kwa pamoja jinsi gani mashine hiyo inavyo zalisha singa hizo za mkonge .
picha na mkurugenzi wa blog kikwatotojr kwa habari mbali mbali na matukio tunaweza kuwasiliana kwa namba 0718991013 au 0754335020
picha ni jinsi mashine hiyo itakavyo kuwa ikizaliwa wakati ikiwa inajaribiwa kabla ya kutolewa maelekezo ya tamati na kufikishwa kwa wakulima
picha ni mkurugenzi mkuu wa bodi ya mkonge taifa akikagua singa zilizo toka katika mashine hiyo mya itakayo tumika na wajasiria mali wadogo wadogo wa kilimo hicho cha mkonge
mkurugenzi wa bodi ya mkonge taifa akiwa na kaimu mkurugenzi wa kituo cha utafiti kilimo MLINGANO wakiwa wanatazama kwa pamoja jinsi gani mashine hiyo inavyo zalisha singa hizo za mkonge .
picha na mkurugenzi wa blog kikwatotojr kwa habari mbali mbali na matukio tunaweza kuwasiliana kwa namba 0718991013 au 0754335020
Sunday, October 21, 2012
mfadhili wa ccm mkoa wa dodoma ndugu sheleli ajiunga na chadema .
Chadema jana ilifanya Mkutano wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Mpwapwa kamanda Baharia.
Mkutano huo ulikuwa na umati mkubwa sana watu. Shangwe, hoihoi na nderemo vililipuka pale mfadhili mkubwa wa CCM mkoani Dodoma ndugu Shelali alipoamua kujivua gamba na kujiunga na CHADEMA. Alipopewa nafasi ya kusema chochote kwa umati ule ndugu Shelali alisema amekuwa mfadhili wa CCM tangu mwaka 1983.
Katika kuthibitisha hilo alikuja na nakala za barua za kuombwa fedha na mzee Malechela pamoja na tuzo nyingi za heshima kutoka CCM. Mzee Shelali alisema ameamua mwenyewe kujiunga na CHADEMA kwani ndicho chama pekee kinachoonyesha nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania na kuwaomba wananchi wa Mpwapwa kujiunga na Chadema.
Katika mkutano huo ngugu Shelali alijitolea kuwanunulia kadi za CHADEMA wananchi wote watakaotaka kujiunga na CHADEMA wilayani mpwapwa. Baada ya mkutano huo wananchi na viongozi wa CHADEMA walielekea nyumbani kwa shelali kushusha bendera ya CCM na kupandisha ya CHADEMA ambapo mzee Shelali alijitolea kuipa CHADEMA ofisi.
Katika mkutano huo wananchi wa Mpwapwa walichanga zaidi ya sh. laki tano kwa ajili ya kusaidia kampeni.
Kilichonifurahisha ni kitendo cha wananchi kuingia barabarani licha ya kuzuiwa na polisi waliojaribu kuzima maandamano yao.
Mkutano huo ulihutubiwa na Benson Kigaila, Diwani Ali Issa Biringi na Kamanda Nicholaus Ngowi
Mkutano huo ulikuwa na umati mkubwa sana watu. Shangwe, hoihoi na nderemo vililipuka pale mfadhili mkubwa wa CCM mkoani Dodoma ndugu Shelali alipoamua kujivua gamba na kujiunga na CHADEMA. Alipopewa nafasi ya kusema chochote kwa umati ule ndugu Shelali alisema amekuwa mfadhili wa CCM tangu mwaka 1983.
Katika kuthibitisha hilo alikuja na nakala za barua za kuombwa fedha na mzee Malechela pamoja na tuzo nyingi za heshima kutoka CCM. Mzee Shelali alisema ameamua mwenyewe kujiunga na CHADEMA kwani ndicho chama pekee kinachoonyesha nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania na kuwaomba wananchi wa Mpwapwa kujiunga na Chadema.
Katika mkutano huo ngugu Shelali alijitolea kuwanunulia kadi za CHADEMA wananchi wote watakaotaka kujiunga na CHADEMA wilayani mpwapwa. Baada ya mkutano huo wananchi na viongozi wa CHADEMA walielekea nyumbani kwa shelali kushusha bendera ya CCM na kupandisha ya CHADEMA ambapo mzee Shelali alijitolea kuipa CHADEMA ofisi.
Katika mkutano huo wananchi wa Mpwapwa walichanga zaidi ya sh. laki tano kwa ajili ya kusaidia kampeni.
Kilichonifurahisha ni kitendo cha wananchi kuingia barabarani licha ya kuzuiwa na polisi waliojaribu kuzima maandamano yao.
Mkutano huo ulihutubiwa na Benson Kigaila, Diwani Ali Issa Biringi na Kamanda Nicholaus Ngowi
wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari arusha ajtc watembelea chuo cha walemavu usa riva
walimu wa chuo cha uandishi wa habri AJTC na basdhi ya viongozi wa chuo cha walemavu cha usa riva jijini arusha katika picha ya pamoja ya furaha huku aliye kaa chini mwenye shati jeupe ni moja wa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habri na utangazaji kwa levo ya diploma bwana Amani James
Presenter wa matukio yote, wa AJTC akipata machache toka kwa wanachuo cha ulemavu cha Usar-River Arusha AMBAE PIA NI KIONGIZI WA BURUDANI KATIKA KIKUNDI CHA WAKAGUZI CREW KILICHOPO KATIKA CHUO CHAO BWANA SAM.
Madam Neema Ezekiel akipiga picha na wanachuo cha ulemavu cha Usar-River Arusha
Presenter wa matukio yote, wa AJTC akipata machache toka kwa wanachuo cha ulemavu cha Usar-River Arusha AMBAE PIA NI KIONGIZI WA BURUDANI KATIKA KIKUNDI CHA WAKAGUZI CREW KILICHOPO KATIKA CHUO CHAO BWANA SAM.
Madam Neema Ezekiel akipiga picha na wanachuo cha ulemavu cha Usar-River Arusha
Saturday, October 20, 2012
YANGA YAIAZIBU RUVU SHOTING 3-2
Mchezaji wa timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam, mpira umekwisha timu ya Yanga imeifunga Ruvu Shooting magoli 3-2, Goli la tatu la timu ya Yanga limepatikana katika kipindi cha pili cha mchezo huo baada ya kutoka uwanjani kwa mapumziko zikitoshana nguvu kwa kufungana magoli mawili kwa mawili katika kipindi cha kwanza
Mchezaji wa Yanga Jerrison Tegete akishangilia mara baada ya kufunga goli la pili katika mchezo huo na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika timu zikitoshana nguvu kwa magoli, mpaka kipindi cha pili ambapo Yanga iliongeza goli la tatu na kufanya matokeo hayo kuwa 3-2
Mchezaji wa Yanga Jerrison Tegete akishangilia mara baada ya kufunga goli la pili katika mchezo huo na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika timu zikitoshana nguvu kwa magoli, mpaka kipindi cha pili ambapo Yanga iliongeza goli la tatu na kufanya matokeo hayo kuwa 3-2
Friday, October 19, 2012
HABARI NDO HIYO: AUNTY EZEKIEL AMEOLEWA..MLISEMA HAOLEWE SASA HAYO.!!!
Mashallah bi Rahma kapendezajeee
Haya habari ndo hiyo mliosema haolewi yako wapi? Bibie huyo mkwe wa Demonte.
Sheikh akimuyonyesha Aunty mahali pakuweka saini
Haya habari ndo hiyo mliosema haolewi yako wapi? Bibie huyo mkwe wa Demonte.
Sheikh akimuyonyesha Aunty mahali pakuweka saini
waislamu wapiga stop kuandamana jijini dar es salam
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekutana na kutoa tamko la kuzuia waislamu kuacha kuandamana mara moja.
Katika taarifa ya waliyoitoa mapema leo asubuhi wakuu na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo wa dini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick, (picha ya chini) aliwatoa hofu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani wamejipanga kulinda hali ya amani.
Akitoa tamko hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kumekuwapo na taarifa za waumini wa Kiislamu kuandamana na kufanya fujo mara baada ya swala ya Ijumaa na baadala yake amewataka kuacha kufanya hivyo na warejee majumbani kwa amani na suala hilo linashughulikiwa kisheria.
Hata hivyo kwa upande wao viongozi wa dini waliokutana na Mkuu wa mkoa juu ya kutolea tamko hilo waliwaasa waumini wote kutoingia mitaani na kuandamana kwani wakifanya hivyo ni kukiuka misingi mbalimbali ya kisheria iliyopo kihalali na watakapofanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa bin Salum amewataka wakuu wa misikiti mkoa wa Dar es Salaam kuwakataza waumini hao kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kukiuka misingi iliyopo.Aidha, aliwaomba waumini warejee majumbani kwa amani.
Askofu Makunda aliwataka watanzania kuendelea kufuata misingi ya kiimani bila chuki wala kufanya fujo.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova (pichani juu) alitoa onyo kali kwa waislamu kuacha kufanya hivyo hii leo kwani kwa atakaekiuka atachukuliwa hatua kali. Kova aliwataka waumini kurejea majumbani mwao kwa amani bila kufanya maandamano na pia aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kupuuza tishio hilo la fujo kutoka kwa waislamu.
“Jeshi limejipanga kuakikisha hali ya amani na usalama inakuwepo hivyo taadhari kwa waislamu kuacha kufanya maandamano mara moja” alisema Kova kwenye kikao hicho ambacho kinaendelea hivi sasa.
waislamu wachache kuandamana dar lengo ni kutimba ikulu
wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi
hapa kiwa anaulizwa na jeshi la polisi imekuwaje wakafanya madhamano hayo mmoja wa wandamnaji
Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu.
Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha.
hapa kiwa anaulizwa na jeshi la polisi imekuwaje wakafanya madhamano hayo mmoja wa wandamnaji
Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu.
WATU sita waliokuwa na nia ya kuandamana kuelekea Ikulu wamekamatwa na Jeshi la Polisi.
kwa mujibu wa waandishi wa habari waliopiga kambi katika viunga vya Ikulu watu hao walifika mmoja mmoja kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano.
kwa mujibu wa waandishi wa habari waliopiga kambi katika viunga vya Ikulu watu hao walifika mmoja mmoja kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano.
Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha.
Thursday, October 18, 2012
kiongozi wa polisi zanzibar anena na wandishi kuhusiana na vurugu
Kamishna wa Polisi Mussa Ali Mussa akifafanua jambo katika Mkutano na Waandishi wa Habari akielezea juu ya Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.
vurugu zilizofanywa na wananchi wachache, Waziri Mohamed Aboud alisema vikundi vya vijana vinavyosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Sheikh Farid Hadi walifanya vurugu hizo katika mitaa ya Darajani, Michenzani, Muembeladu,Magomeni,Amani wakidai Sheikh wao haonekani na kudhani amekamatwa na vyombo vya Dolan a kuwekwa ndani.
wakwanza kulia ni bwana mustapha musa moja kati ya wandishi wa habari waliohudhuria katika kikao hicho cha wandishi wa habari kilicho fanyika ziwani mjini unguja.
picha ni badhi ya maeneo ya jiji la zanzibara wakatio wa vurugu ya kikundi cha UAMSHO na polisi wa zanzibar
Tuesday, October 16, 2012
MWILI WA ALIEKUWA RPC MKOANI MWANZA ASCP LIBERATUS BARLOW WAAGWA LEO MKOANI HUMO
hapa akiwa anaingizwa katika viwanja vya nyamagana jijini Mwanza kwajili ya salamu za mwisho kwa waombolezaji
Shughuli ya kuuaga mwili wake ilifanyika leo kuanzia saa Nne asubuhi hadi saa Kumi jioni katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza, ikihudhuriwa na mamia ya watu kutoka jiji hilo na viunga vyake pamoja na watu kutoka mikoa ya jirani.
warembo wa bongo muvi wajichafua ili wajisafishe
wema sepetu akiwa na mwenzake ant ezekiel mbele ya wandishi wa habari wakiomba razi kwa picha zao za kuonesha hali ya utupu walizo pigwa wakati wa tamasha la serengeti fiesta
Awali ya yote tunawapongeza kwa jitihada zenu za kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu kazi zetu za Filamu na Sanaa kwa ujumla.
Kiukweli sisi tukiwa sehemu ya wahusika katika Wahusika wengi ndani ya tasnia ya Filamu Tanzania, hatuna hiari isipokuwa ni lazima kuwapongeza na kuwashukuru katika harakati na kwa mchango wenu wa kukuza tasnia ya filamu kupitia habari mbalimbali zinazohusu tasnia ya hii pamoja na kwamba ni wajibu wenu.
Lakini Pongezi zaidi za dhati tunaziwasilisha kwenu leo hii (15 .10.2012) moja kwa moja ,kwamba kazi yenu ya uandishi imetusaidia kwa kiasi kikubwa kufikia maendeleo haya machache tuliyo nayo, lakini mchango wenu pia si umetusaidia kupata mafaniko tu lakini pia umetusaidia kujifunza mambo mbalimbali kuhusu filamu za wenzetu na pia kutuonya katika mambo mbalimbali .
Ndugu Waandishi wa Habari, tasnia ya filamu ni moja kati ya fani zinazokuwa kwa kasi na kuleta mafanikio na maendeleo ya baadhi ya vijana wengi wa Tanzania, kutokana na hilo tasnia imekuwa ni moja kati ya maeneo mapya ya ajira kwa raia wa Tanzania na serikali yao kwa ujumla, ni eneo ambalo kwa kiasi kikubwa limechukua rika na jinsia zenye elimu tofauti kwa kusudio la uzalishaji wa filamu bila ya kuzingatia elimu ya muhusika .
Ndugu Waandishi kutokana na kukua huko, tasnia hii imezalisha Wasanii wa Tanzania ambao sasa wana majina yanayosikika kila pembe ya nchi yetu, hali hii imesababisha kuvutia vyombo vya habari kutaka kujua Wasanii wetu wanafanya nini sehemu mbalimbali walizopo.
Ndugu Waandishi mtakumbuka kwamba hivi karibuni kulikuwa tamasha la muziki lililojulikana Serengeti Fiesta ambalo liliandaliwa na kampuni ya Prime Time Promotion kwa pamoja na Clouds Entertainment za mjini Dar es Salaam,
Katika matamasha hayo Wasanii kutoka Bongo Movie Club tulialikwa kama wasindikizaji ili kupamba matamsha hayo katika sehemu yalikofanyika. Katika tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika Dodoma baadhi ya Waandishi ambao walihudhuria tamasha lile walifanikiwa kupiga Picha tofauti tukiwa jukwaani.
Baadhi ya picha zilizopigwa katika tamasha lile hazikuwa nzuri kuoneshwa katika hadhara za watu iwe nyumbani au katika vyombo vya habari. Lakini katika hali isiyotarajiwa picha zile zilisambazwa katika mitandao mbalimbali pamoja na kutolewa katika baadhi ya magazetNdugu Waandishi tunapenda kujulisha umma wa Tanzania kwamba hatujakusudia kupiga tukiwa vile isipokuwa ni mambo ya kiutaalamu katika upigaji wa picha ambapo imechangia kuonekana vile lakini pamoja na upigaji wa picha kuwa wa kiutaalamu zaidi , kwa sababu nyingine ni ya jukwaa lenyewe lilikuwa refu zaidi sana.
Nasi tumeumia sana mioyoni mwetu baada ya kuonekana kwa picha zile kwa sababu sisi kama Wanawake katika jamii tuna Wazazi, ndugu, jamaa , marafiki pamoja mashabiki mbalimbali wa kazi zetu ambao wanatuheshimu kuliko baadhi ya watu wanavyofikiria , kiukweli hatujafurahia na tumeumia sana.
Ndugu Waandishi wa habari pamoja na yote yaliyo tokea tunachukua nafasi hii kuomba msamaha kwa Wizara Habari Utamaduni Vijana na Michezo na taasisi zake , Shirikisho la Filamu Tanzania,Bongo Movie Club na Wadau wake, Familia zetu na jamii kwa ujumla kutokana na picha zilizopigwa tukiwa katika onesho la fiesta ambazo zimesambazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali.
Watanzania na hasa Wanawake wenzetu kwa kadhia hiyo na tunaahidi kwamba jambo hilo halitajirudia tena aidha pia tunaomba waandishi sasa waanze kutazama mambo mazuri tuliyoyafanya na si kutuwinda kwa mabaya kwani sisi ni binadamu na wala si malaika .
Lakini pia tunapenda kutumia nafasi hii kuvijulisha vyombo vya habari kwamba kuanzia leo tunataka visitumie tena picha hizo na kuziondoa katika mitandao yao kwa sababu tunaamini kwamba hazileti mafunzo yoyote katika jamii zaidi tu kwamba zinazidi kupotosha jamii, na ukizingatia lengo kuu la vyombo vya habari kuelimisha na kuburudisha pia.
Mwisho ni matumaini yetu kwamba tutapewa ushirikiano katika mambo mbalimbali yanayotuhusu na tasnia ya filamu kwa ujumla.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Powered by Blogger.