Blogger Widgets MTUHUMIWA WA UBAKAJI AHENYESHA POLISI... | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, September 14, 2013

MTUHUMIWA WA UBAKAJI AHENYESHA POLISI...



KATIKA hali isiyo ya kawaida, kijana Faizi Haji Juma (22), mkazi wa Mchanga wa Kwale Wilaya ya Chakechake, Pemba aliwashangaza wananchi baada ya kuwatoroka askari waliokuwa wamemdhibiti ndani ya jengo la mahakama ya wilaya hiyo.
Kijana huyo anayekabiliwa na makosa mawili katika mahakama mbili tofauti, likiwemo la ubakaji na shambulio la mwili kwa lengo la kutaka kubaka, aliwachomoka askari na kukimbilia baharini katika Soko la Katari.
Baada ya kukimbia kwa muda, askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Agustino Awe na Koplo Mohamed Hamza, walilazimika kumkimbiza kwenye matope na kuhakikisha wanamtia mikononi mtuhumiwa huyo na kumrudisha mahakamani.
Baada ya kurudishwa ndani ya viunga vya mahakama ya wilaya, mtuhumiwa huyo alitakiwa kuieleza korti sababu zilizomfanya akimbie lakini akaishia kubabaika.
Hakimu Omar Mcha Hamza alihamaki baada ya kushuhudia tukio hilo ambapo aliporejeshwa, aliamuru mtuhumiwa huyo kurudishwa rumande.



No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.