Blogger Widgets IAMOND AUKANA U FREEMASON, AWASHANGAA WANAOENEZA KUWA KABADILI DINI | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, December 29, 2012

IAMOND AUKANA U FREEMASON, AWASHANGAA WANAOENEZA KUWA KABADILI DINI


Msanii anaye Ng'ara katika Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva hivi sasa, Diamond Plantum amekana kushiriki wala kujihusisha na imani inayousishwa na nguvu za giza ya "Freemason", na kusikitishwa sana na watu wanao sambaza maneno ya kuwa yeye amebadili dini.

"Mimi sijawahi kujiusisha na imani ya Freemason na wala sijui juu ya hilo kabisaa, Nimelelewa katika imani ya Kiislamu na ninacho juwa nikuwa Mungu ni mmoja....Siwezi Kuwa Freemason Hata siku moja"Alisema Diamond.


Akiongea na Campasvision Diamond, alisema Zaidi ameumizwa sana na kusikitishwa sana na habari zinazo zagaa kuwa yeye kabadili dini, kitu ambacho sio kweli..alisisitiza kuwa awezi kuiacha dini yake na kuwa na imani tofauti na aliyo lelelwa na kudai kuumizwa na watu wanao eneza habari hizo, Alisema Diamond


Vijana wanaoiga na Kukopi kazi zangu, kimsingi nafrahishwa sana tena inanipa nguvu yakuwa kazi zangu zinakubaliwa  hata nawasanii wenzangu, Swala ambali linanifanya niongeze juhudi zaidi katika kuboresha kazi yangu. Alisema Diamond


Akiongelea juu ya Video Mpya ya Kesho Diamond alisema, amefurahishwa sana na Wimbo huo kwani ni miongoni mwa nyimbo ambazo Mashahiri yake hayakumpa shida kutunga kabisa kwa ilikuwa kama masihara lakini kilichotoka nikitu ambacho kimesimama. Alimalizia Diamond

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.