Blogger Widgets Mali za Sharo Milionea zasalimishwa | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, December 1, 2012

Mali za Sharo Milionea zasalimishwa

Baadhi ya vitu vya marehemu Sharo milionea vilivyokamatwa baada ya msako mkali baina ya Polisi na wananchi wa Kijiji Songa Kibaoni vikiwa katika kituo cha polisi chumbageni  jijini Tanga.

vitu hivyo  vilivyoporwa na watu wasiojuliana katika ajali ya msanii mahiri wa 

filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo 

Milionea’ eneo la Songa Kibaoni wilayani Muheza mkoani Tanga, vimesalimishwa na wananchi wanaosadikiwa ni wezi.

Kwani alikuwa akitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea kijijini kwao Lusanga 

Muheza, kwa dhumuni la kwenda kuwasalimia wazazi wake pamoja na kuwapelekea fedha za matumizi.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, jana

 alithibitisha kupatikana vitu hivyo, ambako alisema upatikanaji wake ulitokana 

na msako mkali uliofanywa na uongozi wa serikali Muheza wakishirikiana na
Jeshi la Polisi wilayani humo.

Alisema kwamba baada ya kutokea kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Tanga, liliweka mtego na kutangaza kuinunua simu ya mkononi ya msanii huyo aina ya 

‘blackberry’ ndipo moja kati ya wanaodaiwa vibaka waliohusika kwenye tukio hilo, alipojitokeza na kuipeleka kwa ajili ya kuiuza.

Kwani walipofika eneo ambalo walikubaliana, walikabidhi simu hiyo kwa ajili ya kuikagua, lakini baadaye wezi hao walishtukia mtego huo na kukimbia huku
 wakiiacha simu hiyo.

Aidha, Kamanda Massawe alivitaja vitu ambavyo vimesalimishwa kwa jeshi hilo 

kuwa ni simu ya mkononi aina ya blackberry, Betri la gari, tairi la akiba, radio 

ya gari, begi ambalo lilikuwa na nguo za marehemu, saa ya mkononi na nguo 

ambazo alikuwa amevuliwa na vibaka wa eneo hilo mara baada ya kutokea ajali hiyo.

Mpaka kufikia sasa, msako unaendelea na wamebaini baadhi ya washukiwa wa 

uhalifu huo wamezikimbia nyumba zao kwa hofu ya kukamatwa.

Polisi wako kwenye uchunguzi mkali ili kuhakikisha wanawatia mbaroni wale 

wote ambao waliohusika na kitendo cha kinyama, alichofanyiwa msanii huyo.



No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.