Blogger Widgets TANGA SASA KUPANDISHIWA BILI ZA SHILIKA LA NYUMBA NHC LAKINI WAULA UJENZI WA NYUMBA MPYA | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Wednesday, August 22, 2012

TANGA SASA KUPANDISHIWA BILI ZA SHILIKA LA NYUMBA NHC LAKINI WAULA UJENZI WA NYUMBA MPYA

SHIRIKA la Nyumba la Taifa jijini  Tanga NHC limewaeleza wapangaji kuwa upandishaji wa kodi  za nyumba katika shilika hilo ni kwa lengo la kukarabati na kuboresha nyumba hizo.
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake mapema hii leo Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tanga Bw. Isaya Mshamba  amesema  kuwa changamoto kubwa inayo wakabili kwa sasa ni kuwa elimisha wapangaji wao sababu zilizopelekea  kupandisha kodi hizo. 
Aidha, ameendelea kusema kuwa imekuwa ni vigumu kuweza kuwafikia wapangaji wake wote kwalengo la kuwaeleza sababu zilizopelekea kupandisha kodi hizo hivyo amewaomba wapangaji wa shilika hilo kuweza kukubaliana na hali hiyo kwalengo la kuboresha shilika.
Hata hivyo, Bw. Mshamba ameendelea kusema kuwa mikakati waliyo nayo ni kujenga nyumba nyingine za bei nafuu na kuwauzia wananchi wote hivyo amewataka wakazi wa jijilatanga kuweza kushirikiana nao kwa pamoja.
Sambamba na hayo ameeleza kuwa  Shirika la Nyumba la Taifa NHC kwa Mkoa wa Tanga lina mpango wa kuanza zoezi lo la kujenga nyumba hizo mpya katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tanga na kwakuanzia na wilaya ya Mkinga.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.