Blogger Widgets Aliyetengeneza Filamu ya Kumkashifu Mtume aingia machimboni | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Tuesday, September 18, 2012

Aliyetengeneza Filamu ya Kumkashifu Mtume aingia machimboni

Nakoula Basseley Nakoula, ambaye ni tapeli mwenye kujipa majina mbalimbali mwenye umri wa miaka 55 ambaye alihukumiwa kwenda jela miezi 21 nchini Marekani kwa makosa mbalimbali ya utapeli mwaka 2010, ameingia mafichoni pamoja na familia yake baada ya maandamano ya kuipinga filamu aliyoitengenza kuzidi kupamba moto.

Nakoula alijiita jina la Sam Bacile wakati wa utengenezaji wa filamu ya "The Innocence of Muslims" ambayo trela lake liliwekwa kwenye YouTube na video zake zikimuonyesha mtu aliyeigiza kama mtume Muhammad, akifanya mapenzi, akibaka na akiamuru kuuliwa kwa watu.

Nakoula aka Sam Bacile hajaonekana tangu jumamosi baada ya polisi kwenda nyumbani kwake kumhoji na familia yake ya watu wanne nayo jana jumatatu iliihama nyumba yao na kwenda mafichoni kujiunga na Nakoula.

Polisi wa Los Angeles waliwasili majira ya alfajiri kabla jua halijachomoza na walimchukua mke wa Nakoula na watoto wake watatu na kuwasindikiza kwenye maficho ya siri ambako Nakoula amejificha.

Familia yake ilizificha sura zao wakati wakisindikwa na polisi toka kwenye nyumba yao iliyozungukwa na waandishi wa habari wengi waliokuwa wakikesha mbele ya nyumba hiyo.

"Waliona kuwa watakuwa salama sehemu ambayo wataweza kutoka nje na kuishi maisha ya kawaida", alisema msemaji wa polisi na kuongeza "Tulichokifanya sisi ni kuwachukua na kuwapeleka sehemu ambayo Nakoula amejificha".

Nakoula aliwahi kutupwa jela miaka miwili iliyopita kutokana na utapeli wa cheki za watu kwa kutumia majina mbalimbali feki. Alikaa jela mwaka mmoja kabla ya kutolewa kwa masharti kumalizia kifungo chake uraiani.

Vyombo vya habari vya Marekani vimekuwa vikiripoti kuwa kujihusisha kwake kutengeneza filamu hiyo kunaweza kukawa kumevunja masharti aliyopewa hivyo anaweza kurudishwa jela.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.