Blogger Widgets LINAH ajitoa rasmi THT! | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Friday, September 28, 2012

LINAH ajitoa rasmi THT!

Baada ya kupata mafanikio makubwa toka nyumba ya vipaji Tanzania msanii Lina Sanga, ‘Linah’ amesema kwa sasa atakuwa nje ya Taasisi hiyo baada ya kufanikisha kumuweka juu kimuziki.
Akizungumza na Darhotwire jana Linah alisema atafanya kazi zake peke yake, ingawa atakuwa mwepesi kupata ushauri kutoka kwa walioibua na kuendeleza kipaji chake.
Alisema kujiweka kando kwa taasisi hiyo, ni sababu ya kuwapa nafasi wasanii wengine wachanga waliokuwa ndani ya THT ili waendelezwe na kuwa kama yeye.
Alisema ni kweli THT imemlea vizuri hadi kufikia alipokuwa sasa, hivyo kwa kuwa ameshafika hatua nzuri, ni sababu ya kuleta chachu kwa wasanii wengine waliokuwa na malengo ya kuwika katika nyanja za Kimataifa.
“Nimekuwa nje ya THT kama mwanzo mzuri wa kujitegemea katika ulimwengu wa muziki hapa nchini, ingawa naamini bado nitakuwa mwepesi kuomba ushauri na mabosi wangu hao au kupata kazi kutoka mahali popote.
“Nimeondoka kama sehemu ya utaratibu wa THT kuwapa uhuru wasanii waliofanikisha ndoto zao ili kutoa nafasi kwa wasanii wengine, ukizingatia taasisi hiyo imesheheni waimbaji wachanga wengi na wenye ndoto za kufikia malengo,” alisema.
Wasanii wengine waliofikia malengo yao wakiwa ndani ya taasisi hiyo ni pamoja na Barnabas, Mataruma, Amini, Mwasiti, Linex na  Ditto.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.