Blogger Widgets pangani sasa kupata matunda ya mbunge wao | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Sunday, September 30, 2012

pangani sasa kupata matunda ya mbunge wao


MBUNGE wa Pangani Bw Salehe Pamba ametoa msaada wa bati 80 kwa Shule ya msingi Kilimangwido kutokana na shule hiyo kuchakaa paa lake na kuleta adha kubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Hatua hiyo ya Mbunge inakuja kufuatia ziara zake za hivi karibuni kubaini uchakavu wa shule hiyo ambapo awali wanafunzi walikuwa wakinyeshewa na mvua nyakati za masika na kudumaza kiwango cha elimu.
Alisema juhudi hizo ni utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwasihi wananchi wa Pangani kuendelea kukiunga mkono chama hicho kwani kinatekeleza ahadi zake kwa vitendo kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
Akikabidhi msaada huo jana kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw Albert Bukulu  Mbunge huyo aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuendelea na mshikamano walionao katika kuchangia shughuli  ikiwemo elimu ili kupiga hatua kubwa  za maendeleo ya jimbo hilo.
Bw Pamba alisema wakati umefika wa wananchi kuthamini elimu kwani ndio chimbuko la maendeleo ya jamii hiyo na kuwasisitiza wazazi umuhimu wa kupeleka shule watoto wao.
Akipokea msaada huo Bw Bukulu alisema umekuja wakati muafaka ambapo wanafunzi walikuwa wakipata tabu kutokana na uchakavu wa majengo hayo na kushukuru juhudi za MBunge huyo kuthamini elimu.
Alisema kitendo cha Mbunge huyo kutoa msaada huo ni wazi anatambua kuwa elimu ndio msingi wa maendeleo ya jamii na kumhakikishia kuwa msaada huo utasaidia kuchochea kasi ya elimu katika shule hiyo.
Mbunge huyo anaendelea na ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuendelea kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo yanayofanywa na wananchi wa jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.