Blogger Widgets kaliya mwaka wadauuu kwa vijana wetu walio maliza darasa la saba | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Friday, September 21, 2012

kaliya mwaka wadauuu kwa vijana wetu walio maliza darasa la saba

Msichana huyo [14] jina limehifadhiwa, ambaye alikuwa akifanya mtihani wake wa darasa la saba, alianzwa na hali ya uchungu akiwa katika chumba cha mtihani na hatimaye kujifungua mtoto

Awali ilidaiwa kuwa, mwanafunzi huyo alimuomba msimamizi wake aende msalani akajisaidie na msimamizi huyo alimruhusu, hivyo kudaiwa baada ya dakika chache alimuomba tena msimamizi huyo ruhusu aende nje lakini ilidaiwa msimamizi hakumruhusu kwa kudhani huenda mwanafunzi huyo alikuwa anafanya ujanja wa kupata majibu ya mitihani

Imedaiwa msimamizi huyo alimzuia mwanafunzi huyo asitoke lakini baadae msimamizi huyo alianza kuingiwa na wasiwasi kwa kuona binti huyo anajinyonga zaidi na kumuuliza anasumbuliwa na nini na mwanafunzi kudaiwa alimjibu anasumbuliwa na tumbo

Lakini jibu hilo halikumtosheleza msimamizi huyo kwa kuona msichana huyo anazidi kujinyonga nyonga, aliendelea kumuuliza linamuuma vipi ndipo mwanafunzi huyo alimwambia ukweli msimamizi huyo kwa kumwambia anaumwa na uchungu

Msimamizi huyo ndipo alipoanza kufanya juhudi za kutafuta msaidizi ili wamsaidie binti huyo lakini baadae binti huyo alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume akiwa katika chumba hicho

Taarifa hizi zimethibitishwa na uongozi wa shule ikiwemo Afisa Elimu wilayani humo akiwemo Mkurugenzi Halmashauri ya Kagera

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.