Blogger Widgets Maandamano dhidi ya filamu chafu ya kumkashifu mtume yaendelea duniani kote | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Friday, September 21, 2012

Maandamano dhidi ya filamu chafu ya kumkashifu mtume yaendelea duniani kote

Maandamano ya kupinga filamu ya Kimarekani na vijikatuni vya Kifaransa vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) yameendelea kufanyika katika nchi mbalimbali duniani.
Mjini Tehran maelfu ya watu waliandamana jana mbele ya ubalozi wa Ufaransa wakipiga nara za "mauti kwa Marekani", "mauti kwa Israel"  "mauti kwa Ufaransa" na "mauati kwa Uingereza".
Maandamano makubwa kama hayo yamefanyika pia nchini Afghanistan kupinga vijikatuni hivyo na filamu ya Kimarekani inayomtusi Mtume wa Mwenyezi Mungu. Waandamanaji hao wametaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya watengenezaji na watayarisha wa filamu na katuni hizo.
Huko Pakistan maelfu ya Waislamu wameandamana katika miji ya Islamabad na Lahore wakilaani hujuma za Wamagharibi dhidi ya Uislamu. Polisi wa Pakistan walizuia waandamanaji hao kuvamia ubalozi wa Ufaransa na inaripotiwa kuwa karibu waandamanaji hamsini wamejeruhiwa.
Maandamano makubwa ya kulaani filamu ya Kimarekani na vijikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu yanatazamiwa kufanyika leo katika maeneo mbalimbali ya dunia kabla na baada ya swala za Ijumaa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amejaribu kutuliza hasira za Waislamu akisema kuwa filamu ya Kimarekani ya "Innocence of Muslims" inaaibisha na kukera. Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuwekwa mipaka ya uhuru wa kujieleza na kusema unaotumiwa vibaya kushambulia itikadi na matukufu ya Kiislamu.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.