Blogger Widgets Mke wa Mjukuu wa Mandela Apewa Mimba na Kaka Yake | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Tuesday, September 18, 2012

Mke wa Mjukuu wa Mandela Apewa Mimba na Kaka Yake

Mjukuu wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazimika kumuacha mkewe baada ya mke wake huyo kupata mimba na baadae kujifungua mtoto kufuatia uhusiano wa siri wa kimapenzi na kaka wa mjukuu huyo wa Mandela.

Mandla Mandela ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amemfukuza mke wake mrembo wa Ufaransa, Anais Grimaud baada ya kugundulika kuwa mtoto aliyejifungua mwezi septemba mwaka jana si wa kwake.

Vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa mtoto huyo hakuwa mtoto wa Mandla hivyo kupelekea familia ya Mandela kuamua mwanamke huyo arudishwe kwao kwa kuitia aibu familia hiyo.

Kali ya yote ni kwamba Anais anadaiwa kupewa  mimba hiyo na kaka yake Mandla kufuatia uhusiano wao wa siri wa kimapenzi wakati Mandla alipokuwa safarini.

"Familia ya Mandela imeamua kumrudisha Nkosikazi Nobubele Mandela (nee Anais Grimaud) kwa familia yake baada ta kugundulika kuwa alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa kaka zangu".

"Nathibitisha kuwa uhusiano huo nje ya ndoa ulipelekea kuzaliwa kwa mtoto Qheya mwezi septemba mwaka jana" ilisema sehemu ya taarifa ya mjukuu huyo wa Mandela.

Baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyo mwaka jana, Mandla na Mkewe walimkabidhi mzee Mandela mtoto huyo na Mzee Mandela alimpa jina mtoto huyo katika sherehe iliyofanyika septemba 16 mwaka jana.

Wakati Mandla Mandela akidai kuwa mtoto huyo ni wa mmoja wa kaka zake, Ndaba Mandela ambaye ni mshukiwa mkubwa wa kutembea na mke wa mdogo wake alikanusha kuwa mtoto huyo si wake.

"Hakuna mtu anayemjua baba wa mtoto huyu, naweza kuongea kwa kujiamini kuwa mimi sio baba wa mtoto huyu", alijitetea Ndaba Mandela.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mandla alisema kuwa amehuzunishwa sana na kugundulika kwa mkewe kutembea nje ya ndoa.

"Kugundulika kwa mapenzi haya nje ya ndoa kumekuja kama mshtuko mkubwa sana kwangu na familia yangu. Nimehuzunishwa zaidi kwakuwa kaka yangu mwenyewe ndio mtuhumiwa mkubwa wa kunisaliti", alisema Mandla Mandela katika taarifa yake.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.