Blogger Widgets wavamizi wa maeneo wilayani kilindi na handeni kutakiwa kuondoka haraka | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Sunday, September 30, 2012

wavamizi wa maeneo wilayani kilindi na handeni kutakiwa kuondoka haraka

MKUU wa mkoa wa Tanga lutein mstaafu Chiku Gallawa amewataka watu waliohamia wilayani Kilindi na Handeni mkoani Tanga kuondoka katika wilaya hizo, ili kupisha walengwa ambao ni wazawa wa wilaya hizo, nakwamba amefikia uwamuzi huo kutokana na wahamiaji hao kuhodhi aridhi kinyume na taratibu za kisharia.
Uamuzi huo ameutoa katika kikao cha kamati ya ushauri mkoa wa Tanga RCC kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi ya mkuu wa mkoa
Aidha mkuu huyo wa mkoa lutein Gallawa amesema kwamba Kilindi na Handeni sio shamba la wavamizi hivyo ni vema wakazi hao ambao wamehamia kinyume na utaratibu wa kisharia kuondoka katika maeneo hayo haraka iwezekanavyo kabla ya kufika mwezi Januari mwakani  ili kuepusha vurugu na migogoro ya aridhi siokuwa na tija mkoani hapa.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Tanga amewataka wakurungenzi wa halmashauri zote mkoani hapa kusimamia majukumu yao ipasavyo ili kukomesha hali hiyo kwa kuwatambuwa wazawa halali katika halmashauri zao.
Na katika hatua nhyingine amewataka wakurungenzi hao watumie wanasheria wao katika Halmashauri zao ili kutambua sharia za uchimbaji wa Madini kuliko kuchimba madini kiholela bila kuwa na utaalamu jambo ambalo mara nyingi limekuwa likileta athari kubwa kwa wananchi bila kupata faida yeyote katika maeneo husika.
Kufuatia hali hiyo lutein Gallawa wamewashauri wakurungenzi na wakuu wa wilaya kuwa na idadi maalumu ya wachimba madini ili kuondoa fujo kwa wananchi ikiwemo kuwapa vibali maalum pamoja na risiti.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.