Blogger Widgets chupu chupu kufa | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Wednesday, October 3, 2012

chupu chupu kufa

ABIRIA waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Dar Express  aina ya
Scania  wamenusurika kufa baada gari hilo kuteketea kwa kuungua na
moto wakati likiwa kwenye mwendo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Constantine Massawe amesema
kuwa ajali hiyo ilitokea jana jumatatu saa 5.30 asubuhi katika
barabara ya Segera –Chalinze eneo la Kijiji cha Segera Wilayani hapa.

Amesema gari hilo aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na dereva
aliyetambulika kwa jina la John Mwakihaba (41) lilikuwa likitokea
Rombo Mkoani Kilimanjaro kuelekea Jijini Dar es salaam.

Kamanda huyo amesema lilianza kwa kutoa moshi upande wa mbele karibu
na mlango wa dereva ndipo akasimamisha na kuwaamuru abiria wote
kusalimisha maisha yao kwa kutoka nje.

Amesema baada ya kutoa taarifa polisi ndipo ikawasiliana na kikosi cha
zimamoto cha Mji wa Korogwe ambacho kilipeleka gari lake na kufanya
jitihada za kuuzima moto kazi iliyowachukua muda wa saa moja kuizima.

Hata hivyo abiria wa basi hilo hawakupata majeraha wala hakikutokea
kifo kwani abiria walipoelezwa walitoka ndani ya basin a kukaa kando
wakilishuhudia likiteketea licha ya kwamba gari hilo liliteketea lote.

“Ni jambo la kushukuru kwani hakuna majeruhi wala kifo katika ajali
hiyo kwani abiria waliweza kutii amri ya dereva aliywataka kutoka ili
kunusuru maisha yao.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.