Blogger Widgets Agost26 | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Sunday, August 26, 2012

Agost26

                        TANGA SENSA KWAPAMAZUKA.

Zoezi la sensa ya watu na makazi limeanza rasimi usiku wa mkuamkia leo kote nchi ambapo katika mkoa wa Tanga hususani katika wilaya ya Mkinga mandalizi ya kuandaa zoezi hilo yamekwisha kamilika .


Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mkinga bi Mboni Mgaza wakati akizungumza na wandishi wa habari mapema hii leo alisema kuwawananchi wa wilaya hiyo wako tayari kwa ajili ya kuhesabiwa kutokana na zoezi hilo kwenda sambamba na uandikishaji wa vitambulisho vya taifa.


Mkuu huyo wa wilaya ya Mkinga alisema kuwa wananchi wa wilaya hiyo hawana budi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hilo kwani manufaa yake ni makubwa sana hasa wakati huu taifa likiwa linaandikisha vitambulisho vya ukazi na aliwasihi viongozi mbalimbali wa dini na vyama vya siasa kuendelea kuhamasisha watu wao kuweza kushiriki kikamilifu zoezi hilo .


Huku hayo yakiendelea jeshila polisi mkoa wa Tanga nalo limetoa tamko lake kwa yeyete atakae kwamisha zoezi hili la sensa kwa kuwashawishi watu wengine wasishiriki zoezi hilo basi sheria kali itachukuliwa juu yao.


Hayo yameelezwa na kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantin Masawe kuhusiana na watu ambao wanasambaza vipeperushi kwa wananchi ilikuzuiwa kuhesabiwa kwa itikadi za kidini na kuahidi kuwa hata mara baada ya zoezi hili la sensa kumalizika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale ambao walikuwa wakiwashawishi watu kukataa kuhesabiwa kwani kwasasa wanaendelea na uchunguzi ilikuweza kuwabaini watu hao.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.