Hatimaye kikosi cha pili cha mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba ya jijini kimefanikiwa kutwaa taji la michuano ya BankABC Sup8R 2012 baada ya kuichapa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mabao 4-3 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 3-3 huku mabao ya Simba yakiwa yamewekwa nyavuni na Christopher Edward mawili na Haroun Athumani na kwa upande wa Mtibwa mabao yao yakifungwa Shabani Kisiga mabao mawili na Hasan Seif.
Bao muhimu kwa Simba ambalo limewapa ubingwa limewekwa kimiani na Edward Christopher ndani ya dakika 30 za muda wa nyongeza.
Mfungaji bora wa michuano hiyo amekuwa ni Edward Christopher aliyefunga mabao 9 na amepewa tuzo ya ufungaji bora.
atu peke yake na kufikisha jumla ya mabao tisa, hivyo kujinyakulia tuzo ya ufungaji bora wa michuano hiyo na kuzawadiwa Sh. Milioni 2.
Abuu Hashim ametajwa kuwa mchezaji bora wa Mashindano na kuzawadiwa Sh. Milioni 2.5.
Simba kwa kuwa mabingwa wa michuano hiyo mipya ya BancABC imezawadiwa hundi ya mfano yenye thamani ya shilingi milioni 40 nao Mtibwa Sugar kwa kuibuka washindi wa pili wamezawadiwa Hundi ya mfano yenye thamani ya shilingi milioni 20.
KWA MATANGAZO MBALIMBALI KUHUSU BIASHARA YAKO USISITE KUJITANGAA KUPITIA (KIKWATOJR.BLOGSPOT.COM) WASALIANA NASI KWA SIMU NAMBA +255718991013.+25575433520
No comments:
Post a Comment