SHIRIKA la Nyumba la Taifa jijini Tanga NHC limewaeleza wapangaji kuwa upandishaji wa kodi za nyumba katika shilika hilo ni kwa lengo la kukarabati na kuboresha nyumba hizo.
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake mapema hii leo Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tanga Bw. Isaya Mshamba amesema kuwa changamoto kubwa inayo wakabili kwa sasa ni kuwa elimisha wapangaji wao sababu zilizopelekea kupandisha kodi hizo.
Aidha, ameendelea kusema kuwa imekuwa ni vigumu kuweza kuwafikia wapangaji wake wote kwalengo la kuwaeleza sababu zilizopelekea kupandisha kodi hizo hivyo amewaomba wapangaji wa shilika hilo kuweza kukubaliana na hali hiyo kwalengo la kuboresha shilika.
Hata hivyo, Bw. Mshamba ameendelea kusema kuwa mikakati waliyo nayo ni kujenga nyumba nyingine za bei nafuu na kuwauzia wananchi wote hivyo amewataka wakazi wa jijilatanga kuweza kushirikiana nao kwa pamoja.
Sambamba na hayo ameeleza kuwa Shirika la Nyumba la Taifa NHC kwa Mkoa wa Tanga lina mpango wa kuanza zoezi lo la kujenga nyumba hizo mpya katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tanga na kwakuanzia na wilaya ya Mkinga.
No comments:
Post a Comment