BONANZA-la nguvuu lapamba idi pili jijini TANGA.
Timu ya Now Camp leo imefanikiwa kuibuka mabingwa katika bonanza LA KUGOMBEA MBUZI lililofanyika katika uwanja wa ndani shule ya sec.Galanosi baada ya kuichabanga Mikoroshini 1-0.
katika mchezo huo wa wafainali uliopigwa majira ya saa 11 za jioni, goli la mabingwa likifungwa na FRED DASTAN kunako dk ya 15 kipindi cha kwanza..
mpaka dk 90 zina malizika Now Camp 1-0 Mikoroshini.
Katika mchezo wa awali wa kutafuta mshindi wa tatu,Timu ya LEVOLOSTI iliibuka na ushindi mbele ya KIRARE kwa pen.4-2 baada ya kumaliza sare ya bila kufungana.
Awali bonanza hilo lilishirikisha timu 6 nazo ni ,SHASHAA,MKOROSHINI,NOW CAMP,LEVOLOST,KIRARE NA BUCHER zote kutoka Nguvumali.
mgeni rasmi alikuwa ni Mjumbe wa kamati ya utendaji wa TFF Taifa Khaleed Abdallah,akiwa ameambatana na mmoja wa waandaaji na mwenyekiti wa vasco dagama BERNAD GORIAMA.
katika bonanza hilo Mshindi wa kwanza ameibuka na mbuzi Dume,mshindi wa pili kreti mbili za soda na mshindi wa tatu kreti moja ya soda.
No comments:
Post a Comment