Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Thursday, August 16, 2012


Messi: ‘Sina bifu na Ronaldo!


ChapishaToleo la kuchapisha
EL_CLASICO_PART_1Lionel Messi ameiponda ile dhana kwamba yeye na Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo wana bifu kubwa kati yao.
Messi, Miaka 25, ametoboa msimamo wake huo leo wakati akiongea na Wanahabari kabla ya Nchi yake Argentina kucheza Mechi ya Kirafiki na Germany huko Frankfurt.
Alipoulizwa uteuzi wake kwenye kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, Ballon D’Or, na uhusiano wake na Ronaldo, Messi aliponda ile dhana kwamba kuna uhasama mkubwa kati yao.
Alisema: “Na Cristiano hatuna tatizo. Yote haya yanatoka kwenye Vyombo vya Habari. Sijashindana na Cristiano au kugombana nae!”
Aliongeza: “Hamna hasira kati yetu, ni heshima lakini ningependa Iniesta au Xavi, ambao kwa Miaka mingi wamepata mafanikio makubwa kama vile Kombe la Dunia na Ubingwa wa Ulaya, washinde Tuzo ikiwa mimi nitashindwa. Ni wazi Ronaldo ni Mchezaji Bora na pia Iker Casillas wametajwa kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo hiyo lakini urafiki wangu na Wachezaji wa Klabu yangu ndio uko mbele.”
Messi pamoja na Iniesta na Ronaldo ndio walioingia hatua ya mwisho ya kugombea Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora Ulaya kwa Mwaka 2011/12 ambayo Mshindi wake atatangazwa Agosti 30 na kupewa Tuzo yake huko Monaco.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.