SWALA YA IDDI KITAIFA KUFANYIKA MKOANI RUVUMA WASILAMU TUJIANDAE
Swala ya Eid El Fitr na Baraza la Eid kitaifa mwaka huu vitafanyika Masjid L-huda Msikiti wa Bakwata Songea katika Mkoa wa Ruvuma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania Suleiman Lolila, Swala hiyo itafanyika kati ya tarehe 19 au 20 Agosti, 2012 kutegemea mwandamo wa mwezi.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa Baraza la Eid litafanyika kati ya tarehe hizo hizo kuanzaia saa kumi kamili alasiri.
Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Said Mwambungu.
No comments:
Post a Comment