MBUNGE wa jimbo la Korogwe vijijini Stephen Ngonyani alimarufu majimarefu amemtaka Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bungu Mohamed Kalaghe kuweza kuvitumia vifaa vya ujenzi alivyotoa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi katika tarafa ya Bungu.
Mh Ngonyani aliyasema hayo wakati alipotembelea kijiji hicho akiwa maeambatana na mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo kwa lengo la kukagua ujenzi wa kituo cha polisi ambacho ametoa vifaa kwajili ya ujenzi huwo.
Akizungumza katika mkutano kijijini hapo Mh majimarefu amesema kuwa anahitaji ushirikiano na viongozi mbalimbali katika jimbo hilo ili aweze kutatua kero na kukamilisha ahadi alizozitoa wakati akiwa anawaomba kura mwaka 2010 .
Vifa alivyotoa mbunge huyo kabla ya ukaguzi huwo ni pamoja na mifuko 40 ya saruji, makopo ya ya mafuta ya rangi yeneujazo wa lita 40, nondo 20 za milimita 12 pamoja na shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya malipo ya fundi atakayekarabati jengo hilo amabalo amelikuta likiwa halija fanyiwa kazi yeyeote, alikuta havijafanya jambo lolote.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya korogwe bwana Mrisho Gamba ameliomba jeshi la polisi kuweza kuwachukulia hatua haraiwezekanavyo mtendaji wa kijiji hicho pamoja na mwenyekiti wa kijiji kwa kwakuhujumu maendeleo ya wananchi.
No comments:
Post a Comment