Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Tuesday, August 21, 2012


KWA MASHABIKI WA LIGI KUU YA  UJERUMANI KUANZA IJUMAA

Mabingwa Borussia Dortmund na Werder Bremen watafungua msimu wa 50 wa ligi kuu ya Ujerumani Bundeslifa Ijumaa (24.08.20012), ikiwa ni miaka 49 baada ya timu hizo mbili kukutana katika siku hiyo ya Agosti 24 mwaka 1963.
Timo Konietzka alifunga bao la kwanza la ligi hiyo mpya lakini hakuna ushahidi wowote wa picha za gazeti wala televisheni za kuonyesha bao hilo lililofungwa katika dakika ya kwanza.

mechi ya Ijumaa hii, itarushwa moja kwa moja kwenye televisheni za ujeruman, pamoja na kompyuta, vifaa kama vile simu. 

Ligi ya Bundesliga imekuwa ni taasisi ya kitaifa ikiwa na rekodi ya wastani ulimwenguni ya uhudhuriaji wa mashabiki tangu ilipoanza kwa mwendo wa pole, kuponea sakata za kupanga mechi katika mika ya sabini na kuwatengeneza mashujaa kama vile Franz Beckenbauer, Gerd Mueller, Wolfgang Overath na Guenther Netzer.
Msimu wa kwanza wa Ligi ulikuwa na timu 16 kabla ya ligi kukua hadi tmu 18 na kwa kipindi kifupi timu 20 katika miaka ya mapema ya tisini ili kuzijumuisha timu za Mashariki ya Ujerumani baada ya muungano wa nchi hiyo. 

Bayern ambayo ilijiunga na ligi hiyo katika mwaka wa 1965, ndiyo iliyoshinda mataji 21 ikilinganishwa na matano kila mmoja ya mahasimu wake wa karibu Borussia Dortmund na Borussia Moenchengladbach.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.