Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Tuesday, August 21, 2012


Hatimaye Mali yaunda serikali mpya

Hatimaye Mali yaunda serikali mpya

Mali imetangaza serikali mpya, karibu miezi mitano tangu yalipotokea mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'oa madarakani Rais Amadou Toumani Toure.

 Rais wa serikali ya mpito ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika, Dioncounda Traore, jana alitangaza serikali mpya yenye mawaziri 31 wakiwemo mawaziri watano ambao ni wafuasi wa karibu na kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi, Kepteni Amadou Haya Sanogo. 

Tarehe 22 Machi mwaka huu, maafisa walioasi jeshini wakiongozwa na Kepteni Sanogo walimpindua Rais Toure na kuchukua madaraka ya nchi hiyo kwa madai kuwa Toure ameshindwa kukabiliana na waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo. 

Hata hivyo wanajeshi hao hawakufanya chochote cha maana cha kukabiliana na waasi kiasi kwamba waasi hao walitumia fursa hiyo kuteka maeneo zaidi ya kaskazini mwa nchi hiyo na kutangaza uhuru wa eneo la Azawad.

 Ingawa Kepteni Sanogo amekabidhi rasmi madaraka kwa serikali ya mpito ya wananchi huko Mali, lakini bado anadhibiti mambo kwa nyuma ya pazia.



No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.