COAST UNION WAGOSI WA KAYA WAFANYA UCHAGUZI MDOGO WA CLAB HIYO
Hatimaye wagosi wa kaya timu ya COAST UNION hii leo imefanya uchaguzi uliokuwa na lengo la kukamilisha uongozi wa timu hiyo yenye maskani yake jijini Tanga.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwa uwazi na huru ulikuwa na lengo la kujaza nafasi za wajumbe wa kamati pamoja na makamu mwenyekiti ambapo katika nafasi ya wajumbe awaligombea wajumbe wawili ambao ni ndugu TAITASI BANDAWE naDR AHMEDI TWAHA ambapo wote waliweza kuchaguliwa kwa kupata kura zaidi ya 26 kwa mujibu wa sheria za WAGOSI HAO WA KAYA.
Katika uchaguzi huo TAITASI alipata kura 41 na DR TWAHA alipata jumla ya kura 44 kati ya 49 za wajumbe wote walio huzulia katika uchaguzi huo.
Na kwa nafasi ya makamu mwenyekiti ilikuwa na mgombea mmoja ambaye ni STEAVEN MNGUTO ambaye ndiye mshindi wa nafasi hiyo ya makamu mwenyekiti ambapo alipata jumla ya kura 46 kati kura 49 za wajumbe walio huzulia katika kikao hicho cha uchaguzi.
Sasa wajumbe haowanatambulika kihalali na tayari kuanza majukumu yao kwa kuwa tayari ni wana coastal union.
Kabla ya uchaguzi huo kufanyika wajumbe walipata nafasi ya kuzinadi sera zao mbele ya wajumbe ambapo wote walionekana kuwa na nia moja ya kuipeleka mbele kimafanikio timu yao kwa kusisitiza ummoja na mshikamano na kuwataka kuondoa makundi na kuweka mbele maslahi ya timu ili iweze kupata mafanikio zaidi katika soka la ndani na katika medani za kimataifa.pia wamesema kuwa wameweka malengo ya kunyakuwa ubingwa msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara au nafasi ya pili itakayo wawezesha kucheza michuano ya kimataifa hivyo wamewaomba wanachama pamoja na vingozi kuziondoa tofauti zao na kuukumbatia umoja wati mu.
Naye mwenyekiti wa timu hiyo ya wagosi wa kaya AHMEDI AURORA amewashukuru wajumbe wote kwa kufanya uchaguzi huo kwa uhuru na haki na amewataka wote kwa pamoja kuifanya timu hiyo ifanye vyema kwa kutimiza majukumu yao bila kusukumwa.
Timu hiyo ipo katika maandalizi ya ligi kuu na inatarajia kucheza mechi za kirafiki na timu za Mafande wa polisi Moro,KJT Oljoro ya Arusha na baadaye watacheza na timu ya BANDARI ya nchini Kenya.
KWA MATANGAZO MBALIMBALI KUHUSU BIASHARA YAKO USISITE KUJITANGAA KUPITIA (KIKWATOJR.BLOGSPOT.COM) WASALIANA NASI KWA SIMU NAMBA +255718991013.+25575433520
No comments:
Post a Comment