Zoezi la kuliapisha bunge jipya la Somalia lilimalizika salama jana Jumatatu ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipopinduliwa dikteta Siad Bare, zaidi ya miaka 20 iliyopita huku nchi hiyo ya Pembe ya Afrika ikiendelea na juhudi zake za kumaliza mgogoro wa ndani uliodumu kwa zaidi ya miongo miwili.
Wabunge 250 wa Somalia walikula viapo vyao jana Jumatatu mbele ya Jaji Mkuu wakiwa wameshika nakala za Qur'ani Tukufu.
Sherehe hizo zimefanyika chini ya ulinzi mkali wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika. Nafasi ya serikali ya mpito ya Somalia itachukuliwa na bunge dogo lenye wajumbe 257 na bunge kubwa litakalokuwa na wajumbe wasiozidi 54 ambalo litachaguliwa baadaye chini ya mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Mbunge mmoja mpya wa bunge la Somalia, Siyad Shire Mahmoud amenukuliwa akisema kuwa, wabunge wapya wa Somalia wamefurahi sana kuona kuwa wamekula viapo vyao wakiwa ndani ya nchi yao.
Jana pia bunge la Somalia liliakhirisha uchaguzi wa rais kwa muda usiojulikana kutokana na kusuasua zoezi la kuwaapisha wabunge wapya pamoja na uchaguzi wa spika.
KWA MATANGAZO MBALIMBALI KUHUSU BIASHARA YAKO USISITE KUJITANGAA KUPITIA (KIKWATOJR.BLOGSPOT.COM) WASALIANA NASI KWA SIMU NAMBA +255718991013.+25575433520
No comments:
Post a Comment