WAKULIMA WA MKONGE KAENI MKAO WA KULA TANGA
mkonge ni zao linalo stamili magonjwa na halidhuriwi kirahisi ma wadudu hivyo sasa wakulima wa zao hilo la mkonge wameaswa kuongeza nguvu katika uzalishaji wa zao hilo kwani kwa sasa mkonge unamatumizi mengi ukiacha kutumika kutengenezea kamba.
Mkonge pia hutumika kutengenezea composite ambayo hutumika kutengenezea bidhaa mbalimbali za thamani,Mkonge kwa sasa unatumika katika katika tasinia ya magari,ndege,meli,na ujenzi wa nyumba za bei nafuu.
pichani kulia ni Mkurugenzi mkuu wa bodi ya mkonge Tanzania Bwana Hamisi Mapinda akiwa na meneja wa kituo cha redio Mwambao Fm kilichopo Jijini Tanga Bwana Hashim Fadhili.
Zao la Mkonge linaweza kuchanganywa na mazao mengine ya msimu kama kunde, mahindi, maharage, alizeti, njegere, karanga, n.k. Hii inamuwezesha mkulima kupata mazao ya chakula na biashara kwa kipindi ambacho mkonge unakuwa bado haujakomaa. Hivyo, kumpatia mkulima kipato cha ziada kwa eneo moja. Kutokana na uchanganyaji wa mazo mkulima anapunguza kiasi cha wafanyakazi watakao hitajika kulima mazao ya chakula na biashara. Kwalugha nyingine, mkulima anaongeza tija kwa eneo
ReplyDelete