Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, August 18, 2012


 BAAADA YAN TANZANIA KU8FANYA VIBAYA KWENYE OLIMPIKI WAZIRI ATAKA RIPOTI MALUM 



WAZIRI ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imevitaka vyama ambavyo wachezaji wake waliiwakisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki kuwasilisha ripoti kuanzia jinsi walivyojiandaa, kushiria hadi matokeo waliyopata.
Agizo hilo limetolewa juzi usiku na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo, katika hafla ya kuikaribisha timu ya Olimpiki ya Tanzania na kurejesha bendera ya taifa serikalini.
Akitoa maagizo hayo ya Waziri, Dk. Fenella Mukangara, Mkurugenzi huyo alisema, Waziri ameagiza viongozi wa vyama hivyo na vile vilivyokuwa katika mpango wa kusaka viwango vya kushiriki michezo hiyo, waandae tathimini ya ushiriki wao kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), na kuiwakilisha kwake.
“Viongozi wa vyama, muandae tahmini ya ushiriki wenu wa Olimpiki, nini kimetokea ndani ya miaka  minne, mlifanya nini, mlikwama wapi na nini kifanyike,” alisisitiza Thadeo kwa Niaba ya Waziri, ambaye alikuwa akihusdhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma na kuongeza.
Kama mlivyosema, maandalizi yanakiwa yaanze kesho, sasa ili twende Brazil 2016 lazima tuwe tumejipanga kwa kutambua tatizo kwa kufanya tahmini na kuweka mipango ya pamoja ikiwashirikisha washika dau mbalimbali, sio tunataka twende Brazil wakati vikwazo bado vipo palepale.
Pia Mkurugenzi huyo, aliwasilisha salamu za pongezi kwa wanamichezo hao, kwani kushiriki kwao kulitokana na kufuzu vigezo na wala si kupendeleana wala urafiki, hivyo wamejitahidi kwa kadri ya uwezo wao, hivyo wakaribie nyumbani.
“Mheshimiwa Waziri, anawakaribisheni  na kuwa pongeza sana, mmekutana na mengi sana ya ‘kuwa- discourage’ lakini mmepambana, mengi yametokea, hamkwenda huko kwa utashi wa mtu, mmepita katika vigezo, ni jambo la kujivunia mevipita vigezo na si urafiki, tuchukulie kama chachu tukifanua vizuri tutapongezwa tu,” alisema.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Rais wa TOC, Ghulam Rashid, matokeo hayo yametokana na aina ya maandalizi yaliyofanywa na vyama kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki (TOC), huku akiwataka Watanzania kutatambua kwamba ili kupata mafanikio katika mashindano ya kimataifa, inahitajika maandalizi na vifaa vya uhakika, vitu ambavyo viko juu ya uwezo wao, hivyo kila Mtanzania anatakiwa kusaidia kwa hali na mali.
“Tunaomba Watanzania waelewe, ili mchezaji afanye vizuri inahitajika maandalizi ya uhakika nay a muda mrefu na vyama vyetu ni malofa, haviwezi pekee yao, hivyo tuna wajibu wa kuvisaidia ili viweze kuwaandaa vema na hatimaye kuja kufanya vema,” alisema Ghulam.
Katika Olimpiki London 2012, Tanzania iliwakishwa na wanamichezo sita, ambao ni wanariadha, Samson Ramadhani ambaye alikuwa nahodha, Faustine Mussa, Zakia Mohamed na Mxsenduki Mohamed ambaye hata hivyo hakukimbia baada ya kushikwa na nimonia, bondia Selemani Kidunda, waogeleaji Magdalena Moshi na Amaar Ghadhiar.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.