KOFI alilo mpiga dem kwenye video lamfanya Linex aombe radhi!
Siku chache baada ya msanii Linex kutoa video ya wimbo wake (AIFOLA), ametambaa na ukurasa wake wa kuuzia sura (Facebook), akiomba radhi kwa wanawake wote kutokana na kipande cha video yake ikimuonyesha akimtandika kibao demu aliyekuwa anaigiza nae katika video hiyo kutokana na kupata malalamiko mengi yanayodai kuichochea jamii katika vitendo hivyo hasa kwa wanaume.
"Naomba radhi kwa kila mwanamke Duniani kofi nililompiga video gal wa kwenye video yangu ya 'Aifola', sikua nakusudia uchochezi wa mwanamke kupigwa na mwanaume wake natumai wanaume wenzangu mmenielewa lengo ilikua kutafuta uhalisia wa matukio kwenye video yangu..mwanamke hapigwi analiwazwa na kubembelezwa..." amesema linex
No comments:
Post a Comment