BUTTENER SASA KUTUA OLD TRAFFOD KWA VIPIMO!
LEO Alexander Buttner amesafiri kutoka Schipol Airport huko Amsterdam kwenda Manchester ili kupima afya yake na kukamilisha Uhamisho wake kutoka Klabu ya Vitesse Arnhem ya Holland kwenda Manchester United.
Buttner, Miaka 23, ni Fulbeki wa kushoto ambae hivi karibuni amekuwa akiwindwa na Southampton, Fulham na Queens Park Rangers.
Akisimulia Uhamisho wake huu ambao utagharimu Euro Milioni 5, Buttner amesema: “Kama Wiki moja iliopita ungeniambia ntakuwa nikicheza pamoja na Robin van Persie ndani ya Manchester United, ningekupeleka moja kwa moja Hospitali ya Wenda wazimu!”
Aliongeza: “Mwezi mmoja uliopita, Manchester United ilituma Barua pepe ikionyesha nia yao kunichukua lakini katika Siku 4 zilizopita mambo yalikamilika. Sijaongea na Sir Alex Ferguson lakini mambo yakienda sawa itatokea tu.”
Buttner amekuwa na mgogoro na Klabu yake Vitesse Arnhem kuhusu hatima yake ya baadae na alikuwa amezuiwa kufanya mazoezi na Timu ya Kwanza huku suala lake likiwa mbele ya Vyombo vya Usuluhisho na mwenyewe amesema: “Kwa kuzuiwa kucheza na Timu ya Kwanza na Kesi yangu dhidi ya Vitesse Arnhem ikiwa kwenye Vyombo vya Sheria, Uhamisho huu ni zawadi nzuri kwangu!”
Manchester United wamekuwa wakisaka Fulbeki wa kushoto ili kumsaidia Patrice Evra kwenye nafasi hiyo baada ya mbadala wake, Fabio da Silva, kupelekwa QPR kwa mkopo.
No comments:
Post a Comment