WAZAWA NA WAWEKEZAJI SASA KULA NUSU KWA NUSU KATIKA MIKATABA YA MADINI.
Serikali ipo mbioni kubadili mikataba ya madini kati ya wazawa na wawekezaji na kuifanya kuwa nusu kwa nusu yaani asilimia 50%kwa50% ili kuchangia pato la taifa na kuifanya rasilimali ya madini kusaidia kukuza uchumi .
Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Bw. Eliakim Maswi wakati akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wadogo wa vito jijini Arusha Maswi alitanabaisha kuwa kwa kuanzia na mkataba wa kampuni ya Tanzanite one ya wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambao upo mwishoni mwa mkataba wake.“Kampuni ya TANZANITE ONE mkataba wake umefika kikomo hivyo wakishailipa serekali mrahaba na kama watahitaji kuendelea basi mkataba wetu ni nusu kwa nusu”alisema Maswi.
Aliongeza katibu mkuu huyo kuwa kuanzia sasa watajitahidi ili sekta hiyo ichangie pato la taifa kama nchi nyingine zenye rasilimali hiyo zinavyo nufaika na sekta ya madini.
Nae Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo wadogo wa madini hapa nchini Sammy Mollel alisema kuwa wanataka kuifanya Tanzania kuwa kituo cha uuzaji,ukataji na ununuzi wa madini na vito katika bara la Afrika na kuitaka serekali kuwapa ushirikiano kwenye hilo.
Mollel alisema kuwa wao watatoa ushirikiano kwa serekali kuweza kuwadhibiti wale wote wanaokwepa kuilipa serekali mapato na kuwafichua wafanyabiashara wakubwa wanaokwenda moja kwa moja migodini.
KWA MATANGAZO MBALIMBALI KUHUSU BIASHARA YAKO USISITE KUJITANGAA KUPITIA (KIKWATOJR.BLOGSPOT.COM) WASALIANA NASI KWA SIMU NAMBA +255718991013.+25575433520
No comments:
Post a Comment