BAADA YA SIMBA KUMKOSA BEKI WA KIMATAIFA MBUYU TWITE SASA WAMGEUZIA KIBAO
SIMBa imesema beki wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC na mahasimu wao wa jadi Yanga, Mbuyu Twite si mchezaji bali ni tapeli.
Hatua hiyo inafuatia nyota huyo kuwaingiza mjini Simba ambao awali walimsajili, kabla ya Yanga nao kuingilia kati na kumsajili.
Msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba kitendo cha Twite kuwakilishwa na timu mbili tofauti, FC Lupopo ya DRC na APR ya Rwanda katika kurudisha fedha zao za usajili kinaonesha ni utapeli.
"Ndiyo maana tumeamua kuacha naye kwani hajulikani anachezea timu gani...pia kwa hilo la kutaka kurejesha Simba inaonyesha ni kweli alisaini mkataba na kwetu, sasa huyu si tapeli?alihoji Kamwaga.
Kamwaga ameongeza kwamba kutokana na kitendo hicho, mchezaji huyo ni lazima achukuliwe hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria na taratibu za soka.
Aidha, Kamwaga amesema kwamba bado wapo katika msimamo wa kutopokea hela zao za usajili wa Twite mpaka pale atakapowakabidhi mwenyewe.
No comments:
Post a Comment