JAMANI KUENI MACHO UTAPELI WA KUTUMIA SIMU WAINGI BAADHI YA VIONGOZI WALIZWA
Viongozi watatu wa ngazi ya juu wa Serikali ya Mkoa wa Katavi wametapeliwa na watu wasiojulikana baada ya kuelezwa kuwa wameshinda promosheni ya Airtel ya Shilingi milioni 50.
Waliotapeliwa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajabu Rutengwe, Katibu Tawala wa Mkoa, Emmanuel Kalobelo na Mganga Mkuu wa Mkoa, Yahaya Hussein.
Viongozi hao walitapeliwa kwa nyakati tofauti na watu waliojitambulisha kwao kwa simu kuwa ni watumishi wa Kampuni ya Simu ya Airtel.
Tukio la kwanza lilikuwa ni la Mkuu wa Mkoa kuambiwa ameshinda zawadi ya Sh. milioni 50 na aliombwa awatumie namba za simu za watu watano aliozungumza nao mara ya mwisho na baada ya kufanya hivyo simu yake ya mkononi ikafungwa na matapeli hao.
Akieleza mkasa huo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Yahaya alisema yeye baada ya kupigiwa simu na matapeli hao hakuwa na shaka nao kutokana na kauli yao ilivyokuwa ya ustaarabu. Alisema baada ya kuwapa majina ya watu watano alizungumza nao mara ya mwisho kwenye simu yake na kuombwa awatajie namba zake za siri za akaunti ya Benki ya NMB ili wamtumie zawadi ya Sh. milioni 50. Baada ya kuombwa namba yake ya siri, Dkt. Yahaya hakuwa na shaka yoyote na hivyo akawapatia namba hiyo ya siri. Hata hivyo hakuweza kuibiwa fedha zozote kwa vile akaunti yake haikuwa na salio la kutosha.
Meneja wa Wawi la NMB Wilaya ya Mpanda, Erick Luhanda alisema amepokea malalamiko kutoka kwa viongozi hao. Alisema kiongozi wa mwisho kumpa taarifa alikuwa ni Katibu Tawala wa Mkoa, Kalobelo. Luanda alisema tayari taratibu za kibenki zimefanyika hivyo hakutakuwa na hujuma kwenye akaunti za viongozi hao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alithibitisha kutokea matukio hayo.
KWA MATANGAZO MBALIMBALI KUHUSU BIASHARA YAKO USISITE KUJITANGAA KUPITIA (KIKWATOJR.BLOGSPOT.COM) WASALIANA NASI KWA SIMU NAMBA +255718991013.+25575433520
No comments:
Post a Comment