uamuzi wa Rio wasikilizwa kinyemela>
Kesi inayomkabili Beki wa Manchester United Rio Ferdinand aliyofunguliwa na Chama cha Soka England, FA, kwa kosa la mwenendo mbovu na kuaibisha mchezo kufuatia kauli yake kwenye Mtandao wa Twitter iliohusishwa na asili na rangi ya Mtu na kuashiria Ubaguzi wa Rangi ilisikilizwa kwa siri kubwa Ijumaa iliyopita huku mwenyewe Rio akiwepo kutoa ushahidi wake na hukumu yake itatolewa baadae leo au ikichelewa ni kesho.
Rio Ferdinand alikana Mashitaka hayo na kuomba aruhusiwe kufika mwenyewe mbele ya Jopo la Nidhamu ili atoe maelezo na utetezi wake.
Baada ya kuisikiliza Kesi hiyo hapo Ijumaa, Jopo la Nidhamu limechukua Siku tatu kuijadili Kesi hiyo.
Tukio linalomhusisha Rio Ferdinand lilitokea mara tu baada ya Nahodha wa Chelsea John Terry kuachiwa huru na Mahakama kwa kosa la kuvunja amani kwa kumkashifu kibaguzi mdogo wake, Anton Ferdinand, kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Loftus Road Oktoba Mwaka jana kati ya QPR na Chelsea.
Kufuatia uamuzi wa Mahakama hiyo, kuna Mtu alimtumia Rio ujumbe wa Twitter ambao ulimtaja Mchezaji wa Chelsea, Ashley Cole, ambae alikuwa Shahidi wa Terry Mahakamani, kama ‘choc-ice’, askirimu ya chokoleti, na Rio akajibu kwenye Twitter akicheka na kuisapoti kauli hiyo.
Msemo huo wa kumfananisha Mtu kama askirimu ya chokoleti unamaanisha Mtu ambae ‘nje ni Mweusi lakini ndani Mweupe’ na hilo lilimlenga Cole ambae Mahakamani alidai hakumsikia Terry akimkashifu kibaguzi Anton Ferdinand.
Baadae Rio, akatoa ufafanuzi kwenye Twitter kuwa alichokisema si ubaguzi bali ni msemo unaotumika na wengi kumsema Mtu ambae hana ukweli.
No comments:
Post a Comment