Blogger Widgets kamote-arejea-nyumbani-na-ubingwa tanga | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, October 6, 2012

kamote-arejea-nyumbani-na-ubingwa tanga

ERIKALI imeshauriwa kuwaangalia kwa jicho la pekee wanamichezo hapa nchini hasa kwa kuwapa motisha wanapokuwa wakifanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kuwakilisha nchini zao kama zilivyo katika zinavyofanya nchi nyengine duniani.

Pambano hilo lilifanyika nchini malawi hivi karibuni ambapo bondia huyo alimpiga ngumi kali katika raundi ya nne na kufanikiwa kumwangusha mpinzani wake huyo ambaye alishindwa kuendelea na mpambano huo.
(Bondia Allan Kamote akihojiwa na wahandishi wa Habari baada ya kurejea nyumbani)

Kamote alisema licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali katika mchezo huo lakini anamshukuru mwenyezi mungu kwa kumuwezesha kufanikiwa kunyakua mkanda wa ubingwa huo ambapo alikuwa akiufikiria kwa muda mrefu.

Akizungumza wakati wa halfa hiyo,Meya wa Jiji la Tanga,Omari Guledi amesema amefarijika kutokana na ushindi wa kamote  na kuwashukuru viongozi wa chama cha ngumi kuhamasisha mchezo huo.

 "Bondia Kamote amelipa heshima ya kutosha jiji la Tanga na mkoa kwa ujumla hiyo atahakikisha anafikisha salamu zake kwa baraza la madiwani"amesema Guledi.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Ngumi za Ridhaa mkoa wa Tanga,Hemed Aurora "Mpiganaji"anaelezea furaha walionayo kuhusu ushindi huo..............

(Mw/kiti wa chama cha ridhaa mkoa wa Tanga Hemed Aurora katikati akibadilishana mawazo na wandishi wa habari,kulia ni Hassan Hasheem wa Ch.10 na kushoto ni mwandishi osca asenga)

Kwa upande Mwengine,Promota wa mchezo wa ngumi mkoa wa Tanga,Abbas Mwazoa yeye anasifu juhudu zinazofanya na Meya wa Jiji la Tanga katika kuhamasisha mchezo wa ngumi jijini hapa.

Kwa upande wake,Meya wa Jiji la Tanga MH;Omar Guled amehaidi kulishughulikia tatizo la kukosekana ukumbi wa mazoezi kwa mabondia wote waliopo jijini hapa.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.