Blogger Widgets | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, October 13, 2012


Waislamu wakasirishwa na kukashifiwa Qur'ani  nchini Tanzania.
Jana Ijumaa tarehe 12 Agosti 2012, jeshi la Polisi mjini Dar es Salaam Tanzania lilipata kazi ya ziada ya kutulia ghasia baada ya kijana mmoja wa Kikristo anayejulikana kwa jina la Emmanuel Josephat kuutemea mate na kuukojolea Msahafu huko Mbagala na hivyo kuamsha hasira za Waislamu wenye uchungu na dini yao.

Polisi wametua mabomu ya machozi kuwatawanya Waislamu wenye hasira ambao walikuwa wanataka polisi iwakabidhi kijana huyo aliyeivunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Makanisa kadhaa yamechomwa moto baada ya polisi kukataa kuwakabidhi Waislamu kijana huyo aliyevunjia heshima matukufu ya dini yao tukufu.
Taarifa zinasema kuwa polisi wanawashikilia zaidi ya Waislamu 100 kufuatia ghasia hizo. Waislamu wanaendelea kushinikiza kuachiliwa huru wenzao hao.
Juhudi za viongozi wa Kiislamu za kujaribu kuwatuliza Waislamu zilishindwa jana licha ya viongozi hao kuafikiana na Polisi kushirikiana kutuliza hali ya mambo.
Bwana Hamis Salum Mzazi wa kijana ambaye alipokonywa Msahafu huo amenukuliwa akisema: Kijana wangu alikuwa anatoka Madrasa alipofika katika maeneo ambayo huwa wanapenda kucheza mpira akaja huyu kijana akamwambia wewe una mapepo, hii Qur'ani ni kitu gani, mnapoteza muda tu, kule kuna mashetani, majini na uchawi... halafu yule kijana akachukua Msaafu akaufunua wakatokea watoto wengine wakamwambia utadhurika, utageuka mjusi... akaufunua na kuutemea mate na kisha baadae akaukojolea"
Polisi wameripoti kutumia nguvu za ziada zilizowakumba hata wasio Waislamu.


No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.